TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
 
Loh
Apumzike kwa amani ndugu yetu.
Namkumbuka nimewahi kushiriki events kadhaa alizoshiriki kuziandaa. Alikuwa ni thinktank kweli kweli.

Poleni sana jamaa na familia
 
Mungu ampumzishe mahala pema mja wake... Halafu huyu si ndio alikua muundaaji wa drama ya Siri za familia???

NB.
Kama hutajali mkuu, kuna member tulikua nae kwenye jukwaa la Great Thinkers ghafla tu niliona status yake imebadilika ikawa RIP na haikutolewa ufafanuz juu ya kifo cha member huyu. Hivyo basi ikikupendeza utujuze chanzo cha kifo cha member huyu Mlenge
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Pole sana Max na wana JF.

Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather".

Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.

Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo aliyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.

Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.Iwe kwenye biashara za mitandao au hata majibizano ya hapa JF tu.

Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.
 
Pole sana Max na wana JF.

Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather.

Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.

Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo akiyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.

Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.

Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.
Muda umeshafika😞
 
Back
Top Bottom