Propaganda za ccm na mustakabali wa taifa

mndeme

JF-Expert Member
Sep 2, 2008
323
57
Siku za hivi karibuni baada ya maandamano ya CDM chama tawala kupitia viongozi wake mbalimbali akiwemo rais wa nchi wametoa kauli ambazo zinaonesha wazi kuwa ni chama cha ubabaishaji kinachotumia propaganda na mipasho na kuficha ukweli halisi.

Katika sintafahamu hiyo sijasikia hoja yoyote ya msingi zaidi ya kukomalia amani na utulivu wa nchi.

Hoja: Je amani na utulivu ndo ngao ya ccm ya kutwaa haki miliki ya kutawala nchi hii kwa ufisadi? Je katika maandamano ya CDM kuna vurugu zozote ziliripotiwa?

Ndugu zangu nawaangalia kwa huruma sana watz ambao uelewa wao ni mdogo na kuchukulia kauli za viongozi hao juu juu huku wao wakiendelea kuteseka.
 
Mimi mwenyewe nawashangaa ccm maandamano ya chadema sehemu zote za kanda ya ziwa yamefanyika kwa amani bila vurugu zozote. Ukweli ni kwamba zama za ccm ziko mbioni kutoweka, hoja iliyopo mbele ni hali ngumu ya maisha, mfumuko wa bei, malipo ya dowans, mgao wa umeme n.k. CCM wanatakiwa kutimiza madai hayo siyo kukomalia uvunjifu wa amani. Wanachofanya chadema ni kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kitu ambacho ni kazi ya chama chochote cha kisiasa. CCM hawataki wananchi wafahamu ni jinsi gani nchi inatafunwa na wajanja wachache kwa sababu wanajua mtaji wao ni ujinga na umasikini wa watanzania kwa maana hiyo watanzania wakipata elimu ya uraia watawatosa katika uchaguzi ujao. Nawasilisha.........
 
Mimi pia nashangazwa na lawama zinazotolewa na viongozi mbalimbali wa CCM kuhusu maandamano ya amani yanayofanywa na CHADEMA.
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana hotuba zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa CHADEMA katika mikutano ya hadhara iliyofanyika huko kanda ya Ziwa. Sijawahi kusikia kauli yoyote ile inayochochea uvunjifu wa amani. Maanadamanao ambayo yamepangwa kufanyika nchi nzima ni kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa watanzania wote ambao kila kukicha wanakutana na ugumu wa maisha kwa kunyang'anywa kile kidogo walichonacho eti kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa na hapo hapo pesa zinazokusanywa kuishia katika mikono ya mafisadi wa serikali tawala ya CCM wakiongozwa na fisadi namba moja Rostam Azizi. Mimi nawaunga mkono CHADEMA kwa kuwa wanasimama imara kupinga ufisadi unaosimamiwa kwa nguvu zote na serikali ya Chama cha Mapinduzi. Wananchi walio wengi walitegemea swala la Dowans lingefikishwa na kujadiliwa katika vikao vya bunge lililopita. Chaajabu ni kwamba wabunge wa CCM walisimama imara kupinga hoja hiyo isijadiliwe bungeni kwa visingizio kadha wa kadha, mara hatuwezi kujadili hoja hiyo kwa kuwa iko mahakamani, huo ni unafiki mkubwa kwani bunge lina mamlaka ya kutengua sheria na kutunga sheria pia, iwaje leo waseme kwamba hawawezi kujadli hoja ambayo tayari iko mahakamani? Na vilevile kujadili hoja hakutengui sheria, kilichokuwa kinahitajika hapo ni kuwaeleza wananchi ukweli mzima wa mkataba feki serikali ulioingia na hao mapapa wa ufisadi. Basi kama serikali ya CCM imefanikiwa kubaka haki za msingi za wananchi wa Tanzani za kujua undani wa swala hili mimi sioni vibaya viongozi wa CHADEMA kuitisha maandamano nchi nzima kulaani na kupinga kulipwa kwa bilioni 94 kwa Dowans.:A S 13:
 
Back
Top Bottom