MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 592
Prof.Shivji ni mtu mtaalamu na anajua anachokizungumzia.Ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya watu ambao wengi hawajuwi hali halisi ya visiwani Zanzibar na wala hawaathiriki na vurugu za huko.
Watu hawa ni kama Makamba, Msekwa, Lula wa Ndali-Mwananzela na wengineo wengi kutumia nguvu za ziada kupotosha jitihada za kuleta amani, utulivu na siasa zenye afya visiwani humo.
Hapa nitakuachieni makala ya Jabiri na mwishowe barua kutoka kwa Prof.Shivji aliyomplekea Karume na Seif kuwapa mwongozo wafanye nini.Iko wazi kabisa kwa muongozo wa Prof.Shivji Zanzibar ina mamlaka halali ya kujibadilishia katiba yake kwa kutumia Baraza la Wawakilishi.Wala haoneshi kama kuweka kipindi cha mpito, na kufanya marekebisho kikatiba ni kosa la jinai.
Ni kipi haswa kinachopelekea CCM Bara na watu wengine wengi ambao si wazanzibari, kujitolea na kupoteza nguvu na muda wao kuvuruga jitihada hizi za kuleta amani visiwani humo?
Tukumbuke kuwa jitihada zilishafanyika nyingi na hazikufanikiwa, hii unaweza kusema ni kwa mara ya mwanzo kabisa zinaonesha kukubalika na kufanikiwa.Sasa hawa wanaojitokeza kubeza na kupotosha ili jitihada hizi zikwame, wanatuonesha wazi kuwa vikwazo vya jitihada za awali zilikuwa ni wao!
Nisiwachoshe...makala na barua hizo:
Makala ya Jabir
Barua ya Prof.Shivji kwa Karume na Seif
P:S
**Moderators unaweza kuzifanyia ukaratabati hizo text zikakaa vizuri zaidi, naona kuzipaste hapa kama itakuwa long scroll