Profesa Lipumba akutana na waandishi wa habari kukanusha kuhusu kuitishwa kwa baraza kuu Zanzibar

mjue kirahisi unaweza kumdharau huyu lipumba ila jamaa kikatiba ana haki na anayo sheria
CUF wasipoangalia kwel itasambaratika kwa ujinga wa maalik seif na mwenzio lipumba
 
Haya wazanzibar mpira huo kesho muucheze au ndo tujue mmekubali kumuachia chama Lipumba
 
Napendezwa na Professor Lipumba Genius huyu wa mambo ya Uchumi Na hisabati , Kiukweli ni Mwanasiasa anayepambana na Kundi la Mafisadi lakini anaonekana kuishinda CUF inayomilikiwa na Waziri Mkuu wa zamani Aliyejiuzulu kwa Kuiba mabilioni ya fedha za wananchi Kupitia mradi hewa wa Richmond.


Safari ya kisiasa ya Lipumba iliyokua inaonekana kufa imerudi katika uimara wake akiwa anaonekana mzalendo zaidi. ikumbukwe Professor Lipumba na Dr. Slaa walikataa kuwatumikia Mafisadi.

Namtakia Kila laheri katika Kujenga na kurudisha Nidhamu CUF.
Duh

Send by Nokia 3310 from mbalizi-mbeya
 
Hapa naanza kuona kuwa ni mahakama tu (pamoja na mapenzi ya wana CUF kwa CUF Maalim) yanayoweza kuiokoa CUF Maalim iweze kubakia kama CUF. Prof. ametia mguu ndani ya chama na kwa "kushirikiana" na state institutions anaiteka CUF taratibu kama mahakama haita nena vinginevyo CUF Maalim itafikia tamati kisheria na dola itasema inatekeleza utawala wa sheria. Huu ni wakati mgumu kwa chama hiki. CUF Maalim lazima waje na Plan B wapate pa kutokea hata kama watapoteza jina lakini fikra zao zinaweza kutekelezwa na chombo kingine. Wasisubiri 2020 watakuwa wamechelewa-hili jambo shurti lishe 2018 mwisho ili wajipange kwa 2020.
 


= Bernard Bashange ameitisha mkutano wa baraza kuu kesho lakini mimi Sina taarifa na sijahitisha baraza kuu hilo na halitakuwa halali kama mimi mwenyekiti sijaliitisha.

= Bashange nilishamuondoa kwenye ukurugenzi lakini sasa hivi ameamua kujiita kaimu naibu katibu mkuu wakati naibu katibu mkuu wa chama ni Mama Magdalena Sakaya.

= Amefanya kosa la jinai na kudanganya wajumbe hivyo Vyombo vya dola vinapaswa kumchukulia hatua kali kwa kuhitisha kikao cha dharura Zanzibar ambacho mwenyekiti wa taifa hana taarifa nacho na amekiuka sheria za katiba ya vyama vya siasa.

= Tangu septemba 26/2016 katibu mkuu hajawahi kufika ofisini kwa mwenyekiti. Nmempigia simu na kumtumia memo ili atimize majukumu yake ndani ya chama lakini hajajibu badala yake namuona kwenye ofisi za CHADEMA akizungumza na viongozi wa CHADEMA pamoja na sumaye. Maalim Seif anamuona Sumaye ni bora zaidi kuliko mwenyekiti wake

= Kazi za kiutendaji kwa sasa zinafanywa na kaimu katibu mkuu kwasababu katibu mkuu ameshindwa kutekeleza majukumu yake ndani ya chama.

= Wabunge wa viti maalum waliofukuzwa uanachama wamefukuzwa kwasababu wanakihujumu chama. Wao walijejenga mazingira ya Mbowe wa CHADEMA kuwa msemaji wa chama badala ya mwenyekiti wa taifa wa chama.

= Wamediriki kukaa na wabunge wa CHADEMA pamoja Sumaye kuzindua operation ya ''Ondoa msaliti Buguruni'' na kutoa vitisho.

= Sisi tunafuata taratibu na sheria hivyo tulitoa taarifa polisi kuhusu jambo hili.

= Bunge limetoa tamko na tunalishukuru kwa kuheshimu maamuzi ya chama chetu.

= Majina ya wabunge watakaochukua nafasi yalishapelekwa tangu 2015 hivyo ile orodha iliyopelekwa ndipo wabunge wengine wa viti maalum ndipo watakapopatikana.

= Kila wilaya ya chama imetoa mapendekezo na nafasi zipo 8 lakini mapendekezo ni mengi lakini hili lisipelekee tukagawana au kugombana. Sio lazima kila wilaya itoe mbunge wa viti maalum.

= Nasisitiza kuwa kikao cha baraza kuu zanzibar sio halali kama mimi mwenyekiti sina taarifa nacho na maamuzi yoyote yatakayofanyika ni batili.

Anapoteza muda wake na ubadhilifu wa Ruzuku ya chama kwanza ni gharama kuitisha uchaguzi pili sidhani km wanaweza pata hiyo idadi tena ya wabunge
 
MI nasubiri siku awaombe polisi wamuweke ndani maalim hapo ndio itakuwa mwisho wa insha za kina matatizo, maneno mengi vitendo sifuri
Kama hawawezi kupambana nae waungane nae lau wanyamaze tu sio kutuletea ngonjera tu

Sent from my Phillips Savy
 
Dunia nzima hakuna professor wa ajabu kama bwana yule bora hata RC bashite angekuwa prof..
 
Ni mtazamo Wangu lakini...Nina uhakika kwa elimu, uelewa mpana ,uzoefu na umri Wa mheshimiwa pasi shaka dhahiri shayiri anajua anachokifanya

Lakini dhamiri zetu huchunguzwa na Mungu,na ndio maana mara nyingi kwa nafasi zetu ama huenda faragha ama katika mikutano maalumu ya imani zetu katika makanisa au misikiti nk kuwasiliana na Mungu wetu

Imani zetu zote hizi zimekua zikahamasisha mambo mema na kuhimiza upendo katikati yetu...na Mara chache hasa bahati mbaya tunapoteleza katika kile kinachitwa dhambi ...huenda kwa to a

Profesa ni muumini pia wa dini ya kiislamu...
Binafsi namshauri aache kwenda msikitini yeye na wale wote walionyuma yake pia kama huwa wanaenda makanisani waache...Mungu anaona na kila mtu anajua Mungu huwa anatenda kwa namna yake ...ni Mungu Wa Haki



germve himself
 
Naona sasa Prof. Lipumba kaamua kusafisha chama. Katika mkutano wake leo na waandishi wa habari kaahidi kufukuza wabunge wengine 6 wa majimbo mbalimbali kutoka Tanzania Bara.

Pia kalipongeza bunge na Tume ya uchaguzi kwa kuchukua hatua haraka kwamba taasisi hizo zinaendana na kasi inayotakiwa kwa sasa...

Lipumba kawaonya wabunge wengine na viongozi wanaofikiri yeye ni wa mchezo. Anasema muda huu ni wa kujenga chama hivyo hatataka upuuzi wowote mbele yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom