TANZIA Profesa Justinian Anatory afariki dunia

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,889
35,901
Aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu Mipango, Fedha na Utawala katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Profesa Justinian Anatory amefariki dunia.

IMG_20210810_104317_735.jpg

Profesa Anatory ameacha alama zake za kitaaluma UDSM na UDOM aliko pitia akilisukuma gurudumu la maendeleo mbele.

Bwana alitoa, bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

Apumzike kwa amani Profesa Anatory.

----

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimeeleza kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango, Fedha na Utawala katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Profesa Justinian Anatory na kusema kitaukumbuka na kuuenzi mchango wake.

Kifo cha Profesa Anatory kimethibitishwa leo Jumatatu, Agosti 9, 2020 na Baraza la Chuo, Menejimenti na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Limesema limepokea kwa masikito makubwa taarifa za kifo cha msomi huyo.

“Chuo Kikuu cha Dodoma kinaukumbuka na kitauenzi mchango wa Profesa Anatory alioutoa akiwa chuoni hapa akiwa kama Amidi wa Shule Kuu katika ndaki ya Sayansi ya Kompyuta na Elimu Angavu.

“Chuo Kinatoa pole kwa familia, ndugu jamaa, marafiki, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Chuo Kikuu cha Dodoma na wote walioguswa na msiba huu mzito,” imesema taarifa ya kifo cha mwanazuoni huyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom