uran
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 8,272
- 11,746
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chadema, Profesa Mwesiga Baregu, amesema viongozi wa chama hicho wanapaswa kulinda kauli zao ili kuepuka mvuragano unaoweza kutokea wakati huu.
Wakati huu ambao chama kimekuwa na mambo mengi, nawasihi viongozi kuchunga kauli zao ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.
Nimekuwa msuluhishi ndani ya chama, nakwambia ndani ya chama haiwezekani fikra moja ikaendelea kudumu, kwa msingi huo lazima watu watofautiane mtazamo, si kila jambo kupinga.
Katika hali hii, msimamo wangu ni kwamba changamoto inayotukabili tupunguze makali ya maamuzi, kwa sababu Watanzania wengi wanakitegemea chama hiki.
Hivi sasa Watanzania wanajiandaa kukikabidhi CHADEMA dola, ni wakati mzuri wa viongozi kufikiria maisha ya chama kwanza na baadaye ukweli wa mambo utajulikana, amesema.
source: wavuti.com