Profesa Baregu: Watanzania Wanajiaandaa Kukikabithi CHADEMA Dola.

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
8,064
11,354
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chadema, Profesa Mwesiga Baregu, amesema viongozi wa chama hicho wanapaswa kulinda kauli zao ili kuepuka mvuragano unaoweza kutokea wakati huu.

“Wakati huu ambao chama kimekuwa na mambo mengi, nawasihi viongozi kuchunga kauli zao ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.

“Nimekuwa msuluhishi ndani ya chama, nakwambia ndani ya chama haiwezekani fikra moja ikaendelea kudumu, kwa msingi huo lazima watu watofautiane mtazamo, si kila jambo kupinga.

“Katika hali hii, msimamo wangu ni kwamba changamoto inayotukabili tupunguze makali ya maamuzi, kwa sababu Watanzania wengi wanakitegemea chama hiki.

“Hivi sasa Watanzania wanajiandaa kukikabidhi CHADEMA dola,
ni wakati mzuri wa viongozi kufikiria maisha ya chama kwanza na baadaye ukweli wa mambo utajulikana,” amesema.

source: wavuti.com

Prof. Baregu pamoja kuwa nakuheshimu sana kwenye ili nakupinga tanzania hakuna chama mbadala wa CCM.
 
Kwani magamba huwa mnakiri ukweli? Wajuuzi wa mambo wanajua CDM mwakani inatimba magogoni.
 
Prof. Baregu pamoja kuwa nakuheshimu sana kwenye ili nakupinga tanzania hakuna chama mbadala wa CCM.

Tatizo hujui hata nini kinacho endelea CCM! Wengine tunaishi na kujadiliana na baadhi ya viongozi wako kwa faragha. Wanayo yasema pembeni ni tofauti kabisa na sura wanayo onesha hadharani. Bila madaraka ya dola hakuna CCM! Watu wajezana huko kwasababu ya kupata madaraka na pesa,si mapenzi ya chama wala taifa lao.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chadema, Profesa Mwesiga Baregu, amesema viongozi wa chama hicho wanapaswa kulinda kauli zao ili kuepuka mvuragano unaoweza kutokea wakati huu.

“Wakati huu ambao chama kimekuwa na mambo mengi, nawasihi viongozi kuchunga kauli zao ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.

“Nimekuwa msuluhishi ndani ya chama, nakwambia ndani ya chama haiwezekani fikra moja ikaendelea kudumu, kwa msingi huo lazima watu watofautiane mtazamo, si kila jambo kupinga.

“Katika hali hii, msimamo wangu ni kwamba changamoto inayotukabili tupunguze makali ya maamuzi, kwa sababu Watanzania wengi wanakitegemea chama hiki.

“Hivi sasa Watanzania wanajiandaa kukikabidhi CHADEMA dola,
ni wakati mzuri wa viongozi kufikiria maisha ya chama kwanza na baadaye ukweli wa mambo utajulikana,” amesema.

source: wavuti.com

CHADEMA hii hii ambayo imeanza kuuwa wanachama wake!!!!!

Au unazungumzia CHADEMA nyingine!!! Yaani unamaanisha itafika wakati tusema rais wa JMT dr. Slaa au mmachame dj baba freelady aka mzee wa starehe dubai!!!

Nadhani hii ni ndoto kivulini.
 
Prof Baregu huwa anajitambua. Ni mtu makini sana na muhimu.

Ni kweli prof,CHADEMA ndio tumaini la watanzania
 
Kama hakulazimishwa basi kawa mwanasiasa mazima sasa!!!!!!!
Hii kauli hawezi isema mbele ya wasomi wenzake katika mjadala wa kitaaluma!!!!!
 
CHADEMA hii hii ambayo imeanza kuuwa wanachama wake!!!!!

Au unazungumzia CHADEMA nyingine!!! Yaani unamaanisha itafika wakati tusema rais wa JMT dr. Slaa au mmachame dj baba freelady aka mzee wa starehe dubai!!!

Nadhani hii ni ndoto kivulini.
Hata kwenye kanga kuna maneno kama haya yako.
 
Touch-Log Out

Forum-New Posts-Settings-Search

->-Forum->-General Forums->-Jukwaa la Siasa

Topic:-nape wa ccm ni sawa na zito wa chadema

longinos-12:00 Today-

Ukifuatilia siasa za hawa dogo zinafanana, nape alipoleta ukorofi kuhusu jengo la uvcccm alijifanya ni mpambanaji, mtetezi wa vijana nakujifanya ccm anaijuwa kuliko akina EL eti kwa sababu baba yake alikuwa kwaya masta wa ccm(kama komba)kilichompa nafasi moses nnauye ni kuimba si weledi wa siasa.Nepi aliporudishwa kundini na jakaya alirudi na kauli mbiu KUFUKUZA MAGAMBA NDANI SIKU 90 naamini ni siku 90000.Kinachojitokeza ni kunenepeana kwa Nepi bila majibu ya siki 90.
Zito nae kaja na gear hiyo hiyo, nilijiunga cdm nikiwa na miaka16 so what oh wengine wametoka ccm wanajifanya wanakijua chama, hizi ni kauli na kijuha ambazo hazina mshiko sijui zito alitaka watu watokee mwandiga au kwa ndugu zake wa asili Bujumbura? Kama unakipeleka chama mahakamani unategemea huruma gani kwa wana cdm? Tamaa na kutaka sifa ndiko kunakowasumbua waili hawa na hawatafika popote kisiasz maana WANAFIKI walilaaniwa hata kwenye vitabu vya dini mwisho wa zito na nape 2015 sababu Kikwete akitoka Nepi inabini akajiunge na Frelimo ya msumbiji na MM Zito mahakama itakulinnda mpaka 2015 baada ya hapo utatupwa chali,
 
Labda wakabidhiwe dola za zimbabwe

ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!! umenichekesha sana. na hiyo AVATAR yako akiiona profesa atahamaki kweli kama siyo mvumilivu. binafsi nimeshazoea hizo kauli kwani zilizungumzwa sana mwaka 2010 na huyo huyo profesa kila alipopata nafasi.
 
Back
Top Bottom