Btw ingawa kuna masuali yangu mengi umekwepa kuyajibu mtu mzima wewe na msomi wetu wa "kitanzania bara" nkugusie hili la mafuta na gesi ili ndo ujue kama SMT ni wezi na dhulma na wamekalia kula Mali za wazenji, kama watu wanavojidai suala la mafuta na gesi yameingizwa katika muungano, tangu ipatikane gesi ya songosongo mbona hakuna mgao wa mapato yakeee?!!! Yakhe waweza tupa jibu au znz ikilima bangi itakuw ya znz lkn mafuta ni ya SMT? Mifano yako chengu halafu inakurudia mwenyeo, Bobuk hujanipatia jibu la Almasi inapatikana wapi na je BIG BROTHER hatakiwi kuitumia iyo?
Hivi wewe Chilubi unaposoma majibu yangu akili zako unakuwa umeweka wapi? tatizo lako unafikiri Ki-Makunduchi ni sawa na Kiswahili!
Ngoja nianze na suala la Almasi ambalo nilishakujibu. Almasi inapatikana Tanganyika specifically Shinyanga. Big brother anaitumia kwa maendeleo ya Tanganyika, kwasababu madini sio suala muungano. Kama mnataka (Wa-ZNZ) madini liwe suala la Muungano basi leteni hoja kwenye Bunge la JMT. Hiyo itakuwa right direction kuelekea SERIKALI MOJA maana polepole kila jambo litakuwa la Muungano.
Kuhusu gas ya songosongo, hivi unafikiri hiyo 4% mnayopewa kila mwezi na SMT mapato yake yanatoka wapi? Au unataka mfungiwe pipe la gas kutoka Songosongo hadi Unguja na Pemba ndiyo ujue kwamba mnapata mapato yanayo tokana na gas ya Songosongo? Tumia akili kidogo basi hata kama ni za Madrassa.