Prof Shivji na mihadhara ya katiba ITV

Kipindi hiki ni kizuri sana, nimefuatilia Lecture zote mbili, jambo nililogundua kwa haraka haraka ni muda hautoshi, kipindi kinahitaji saa moja kwa ajili ya lecture na saa moja kwa ajili ya majadiliano. Kuna kuna vipindi kama marumbano ya hoja vinapata masaa mawili sioni kwa nini kipindi hiki kisipate masaa mawili.

Ombi kwa wanaharakati, hakikisheni wananchi wanafaham uwepo wa kipindi hiki, hasa wilayani na vijijini. Kwamba, zinaweza anzishwa program kwenye kumbi mbalimbali na watu wakahamasishwa kuja kujifunza mambo ya katiba.

Ukimsikiliza Prof Shivj, hata kama una moyo mugum namna gani lazima uelewe kuwa mambo mengi huko nyuma yamekwenda ndivyo sivyo na sasa ni wakati wa kuokoa jahazi kabla halijazamishwa na waroho wachache ambao wao wana namna ya kupaa (mabawa) wakati jahazi linazama.
 
Back
Top Bottom