Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu
SOURCE:MAJIRA
Ni heri kuwa na Msomi mmoja mwenye uelewa kama Profesa Safari kuliko kuwa na Watu Elfu kumi Vibaraka kama Ephrahim Kibonde. Hata kama ingekuwa kweli DC alikwenda pale kama Kiongozi wa Dini, the way wanavyoshabikia issue hiyo na kuiweka kwenye hali ya udini ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa. Inapofika mahali, kutokana na Ukibaraka wake na kujipendekeza kwa CCM Kibonde eti anadai hata Waislam wataanza kuwavua nguo Masista(kana kwamba DC ambaye ni mvunja sheria ni kiongozi wa dini), hii inaonyesha upeo wake mdogo ambao unaweza kuwashawishi wenye upeo mdogo kama yeye kuanza kutekeleza hayo ambapo sidhani kama wenzetu Wakristo nao watakubali na mwisho wake kila mtu anaujua utakuwaje.
Zamani ndio nilikuwa najua kwamba Waathirika huwa wanaweza kuzungumza mambo ambayo hawakuyatarajia lakini si baada ya kupatikana kwa ARV's.
Ni heri kuwa na Msomi mmoja mwenye uelewa kama Profesa Safari kuliko kuwa na Watu Elfu kumi Vibaraka kama Ephrahim Kibonde. Hata kama ingekuwa kweli DC alikwenda pale kama Kiongozi wa Dini, the way wanavyoshabikia issue hiyo na kuiweka kwenye hali ya udini ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa. Inapofika mahali, kutokana na Ukibaraka wake na kujipendekeza kwa CCM Kibonde eti anadai hata Waislam wataanza kuwavua nguo Masista(kana kwamba DC ambaye ni mvunja sheria ni kiongozi wa dini), hii inaonyesha upeo wake mdogo ambao unaweza kuwashawishi wenye upeo mdogo kama yeye kuanza kutekeleza hayo ambapo sidhani kama wenzetu Wakristo nao watakubali na mwisho wake kila mtu anaujua utakuwaje.
Zamani ndio nilikuwa najua kwamba Waathirika huwa wanaweza kuzungumza mambo ambayo hawakuyatarajia lakini si baada ya kupatikana kwa ARV's.
umesahau taasisi mpya inayoitwa clouds fm.hizi ni taasisi za ccm zilizoanzishwa baada ya uhuru.
1.uwt.
2.uvccm.
3.bakwata.
4jumuia ya wazazi.
5.sukita.
6.
7....................
baadhi ya taasisi hapo zimeshakufa zilizobaki ziko taaban kilichobaki ni mzazi ccm kufa kwani nayo iko icu.
taasisi zake zinatumika ki propaganda nyingfine hazina shida kwani matumizi mabaya yanaiathiri ccm yenyewe ila hii bakwata ni hatari sana kwani imeshikilia imani za watu wakati huohuo ikifanya shughuli za kisiasa.hatari iliyoje na waislamu wanaiona na wanakaa kimya.
katika makosa ya wazi bakwata iliyofanya ni hili.
ilitangaza wazi kuwa mwenye mamlaka ya kutangaza kuonekana kwa mwezi ni shehe mkuu.
haya mafundisho bakwata imeyapata wapi?
mtume alisema mtu yeyote akiuona mwezi kwa ushahidi wa watu wengine watatu basi ni halali kufungulia na kesho yake ni idd.
sasa bakwata wamepata wapi mamlaka ya kumteua shehe mkuu kuwa msemaji kwa jambo ambalo mtume ameliweka wazi?
ndugu waislam hawa watu ni wanafiki na hatari hata kwa uislam.
uganda hata kenya hatujawahi kusikia wakiwa na migongano kama hii ya kwetu,tuamke tuiambie ccm mambo ya waislamu yaendeshwa na kuamuliwa na waislamu kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu.
abdala safari ameeleweka vizuri naomba tuanzie hapo.
naomba tuelewe kwama wakristo ni watanzania ila watanzania si wakristo.
na waislamu ni watanzania ila watanzania si waislamu.
hii ni nyumba yetu sote tusiruhusu mmoja kati yetu aichome nyumba yetu kwa kisingizio cha kutetea kundi moja.
TAQ BiriiiiiiViongozi wa dini ya kiislamu kupitia taasisi mbili zilizotajwa hapo juu wameonyesha kukerwa na kitendo cha DC 'kuvuliwa sijui ni jalabibu ama ni mtandio katika kichwa cha mama wa kiislamu'. Hata mimi katika mazingira ya kawaida ningekerwa na tabia ya makamanda wale na naamini ingekuwa hivyo kwa kila mtu na viongozi wangu wa CDM ambao hujali sana mambo ya kijamii wangekuwa wa kwanza kuomba msamaha kwa niaba ya Chama.
Lakini katika hili naomba nitofautiane na viongozi wangu watukufu wa taasisi tajwa hapo juu. Kimsingi sasa hivi Igunga is political battle ground na mahala popote ambapo kuna mpambano waina yoyote sheria za kawaida huwa hazitawali bali kunakuwapo na sheria na taratibu ambazo zinaelekeza namna bora ya kutekeleza majukumu yetu.
Mkuu wa wilaya ya Igunga saa na wakati ule alikuwa ni mhalifu wa kijamii na alipaswa kushughulikiwa kwa namna ileile ya kiuhalifu. Bahati mbaya imetokea mama huyu aliyetakiwa kusimamia mpambano wa kisiasa wa vyama vya siasa, aliamua kuvaa daruga na kuingia uwanjani bila ya kibali na ruhusa ya refa na akaingilia upande wa goli la upinzani shughuli aliyopata anaijua mwenyewe na wapambe wake.
kujaribu kuingiza hoja ya uislamu kwa mama huyu ambaye alikuwa anavunja kanuni ya msingi ya kutoa haki haijarishi ni padri au sheik, au sista au mama wa kiislamu ni lazima ashughulikiwe kwa lugha ya kisiasa `ambayo ataielewa vizuri.
Kuvaa baibui, hijabu au kanzu, au nguo za usista na upadri ukaende kutenda ushetani utashughulikiwa kwa hasira za kishetani.Chadema walijitahidi kuzungumza lugha ambayo CCM na mama yule na mwajiri wake wangeielewa. Ni bahati mbaya kuwa tendo la muovu huyu limewafika vipofu wa maadili na sasa wamelivalia kanzu na kulibeba eti ni kukashifu uisilamu.
Ebu tumwogope Mungu, na tutende haki kwa kuzingatia imani zetu.CCM iliyopoteza dira inatupeleka pabaya inahubiri Tanzania isiyo na dini halafu inatugawa katika misingi ya imani zetu. Watanzania tumefika pahala pabaya ambapo mwizi anaulizwa dini yake kwanza na kama nikigundua ni mkrito mwenzangu nasema eti si mwizi, ukijua ni mwislamu unasema wanamuonea eti kwa sababu ya dini yake, jamani tunakwenda wapi? Jalabibu na uhalifu wa kisiasa vinahusiana nini? Uhalifu na imani vinahusiana namna gani?
Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padre aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusianao
Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu bali kinasubiri uamuzi wa mahakama utakaoamua iwapo Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario alivuliwa hijabu kwa makusudi alipokamatwa na wafuasi wa chama hicho.
Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (HAY AT) kukitaka chama hicho kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitaha yake na hivyo kumdhalilisha.
Akizungumza na wandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA Prof. Abdallah Safari alisema kuwa chama hicho hakiko tayari kujibizana na wanazuoni hao.
"Si vizuri kuzungumzia mambo ambayo yako mahakamani lakini mahakama itaamua kama DC Fatma alivuliwa hijabu na kama alivuliwa ni kwa makusudi gani, ni uamuzi wa mahakama pekee ndio utaokaomua," alisema Prof Safari.
Alisema kuwa Chadema haina sera ya udini kwa hiyo hakiwezi kushabikia mtu kuvuliwa hijabu kwa makusudi huku akionya viongozi wa dini kuacha kutoa taarifa zinazopotosha ukweli na zinazolenga kuvuruga mshikamano wa Watanzania.
Prof. Safari ambaye ni mwanasheria na mwanazuoni wa kiisalamu, alisema kauli hizo zina lengo la kufarakanisha umma wa waislamu na chama hicho ambacho kinalengo la kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kunuka ufisadi wa CCM
Helkopta kukata anga
Wakati huo huo Chadema kinategemewa kuanza kutumia helkopta kurudia kampeni katika Kata zote 26, lengo likiwa ni kuwakumbusha wananchi na kuwahamasisha kukichagua chama hicho zikiwa zimebaki siku tisa kufika uchaguzi.
SOURCE:MAJIRA
na dental formula yake ya ngiri.Huyu Kibonde ni wa kupuuzwa tu kwani inaelekea ule ugonjwa umeshagonga utosini sasa hana tofauti na chizi mwingine yoyote, siku si nyingi akiona jalala ataanza kuchekelea kujipatia mlo.Halafu mtu mwenyewe ni punga.
UBWABWA TU NDO MNACHOWAZA!!!!Mzee hata kiswahili kinakusumbua,kweli we ni chadema!! Sio kudharirisha ni kudhalilisha!! Ndo mnataka kuongoza nchi nyinyi na umbumbumbu huu