Prof. Ndalichako, ni lini tutaanza kutumia Kiswahili kama lugha ya kujifunzia hadi Chuo Kikuu?

Sahihi,

Kwa kweli ni aibu sana kuona watu wanazungumza kuhusu 'utandawazi' na 'lugha' na kutetea lugha ya kiingereza eti kwa sababu ya juu juu kama vile 'kufanana' na kuwasiliana kwa mawili matatu...

Kutumia lugha mama ya Kiswahili ni jambo linaloweza kutujenga kwa kina zaidi kuliko kiingereza. Mimi ninatumia lugha ya kiingereza kwenye masomo ya jamii, mipango na maendeleo; na nitayajua manufaa yote ya rasilimali za mtandaoni na michango ya wataalam na wabobezi iliyotamalaki mtandaoni. Pia ninatokea kwenye taaluma za kiuhandisi. Pamoja na haya yote, sina hata chembe ya shaka kudai kwamba tunahitaji kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia masomo na kuendesha visomo vyote katika jamii yetu ya Kitanzania na labda hata ya majirani--pia Afrika.

Kuna namna ya kuchambua ukweli na umuhimu wa shauri hili kwa kina; pasi mdahalo wa hoja na fikra za juu juu kuhusiana na ukweli wa jambo lenyewe.

Binafsi natambua kuwa lugha yapaswa kuwa ni mapenzi na utamaduni wa mtu binafsi, siyo shurti ama kizingiti kwa mtu awaye radhi kufungua akili yake ili kutaamulika ama kuelimika.

Ndiyo tunaweza kurasimisha mikondo ya kielimu katika muktadha wa lugha zaidi ya moja--tatizo ni rasiimali fedha katika ngazi ya mifumo na tawala... Kwa hiyo ikibidi kutathmini lipi laweza kuwa na manufaa ya muda mrefu na tena endelevu, matumizi ya lugha ya Kiswahili linaweza kuwa shauri timilifu kujidhihirisha mbele ubora wa 'kweli ya kisayansi kabisa' -- kusimama nyuma ya tafiti na uchunguaji.

Matumizi ya Kiswahili kwa tija na maendeleo ya mipango kwa taifa ni suala linaloweza kuthibitishwa kwa tafiti na mapelekeo yatokanayo na hizo zenyewe. Si suala za malumbano na hoja za mitazamo ya juu juu.

Kwa kweli hata wateteaji wengi wa matumizi ya kiingereza wanazunguma kwa hoja mufilisi; na inakera mno kuona watu wanafikiri wanaongea jambo la maana na kumbe wanazungumza kwa uchunguaji wa juu juu mno.... Yaani inaweza hata kuleta fikra ya kushangaza, je hawa watu wanabidii hasa ya kupitia, kufanya visomo na kuchambua misingi ya visomo vya maendeleo--dhana na nadharia za maendeleo? Je, hawa watu wanadhani tunaishi kwenye mifumo adilifu ya uchumi, siasa na utandawazi?

Kuna mengi hata humu hayazungumzwi kwa kwa kina ufundi kuhusiana na ukweli wa mambo--mtu, mazingira, uchumi, ustaarabu na maendeleo...

Hebu tuwaachie wataalam na wajuvi wenye nia njema, mapenzi mema na mielekeo sahihi -- ya uono na mipango kwa nchi, na taifa watupatie miongozo na ufafanuzi wa mbinu na mikakati kwa maendeleo ya kweli na si maendeleo ya 'bendera ifuatayo upepo'...

Hmmm

Kipindi obama anakuja Tanzania, speech ya kikwete aliomba vitabu vya kugundishia masomo ya science mashuleni. Pia alipokuja Xijinping wa china pia katika hotuba za kikwete aliomba vitabu, sasa mimi nikawa najiuliza wasomi wengi tulionao Tanzania kweli tunashindwa kuandaa vitabu kwa ajiri ya vijana wetu vyuoni na high school? Wakati huo mimi nimesoma chuo vitabu vyote na vya science vimeandikwa na ma professor wa chuo, mwalimu hawezi shindwa kueleza kitu ambacho amekiandika, anakueleza hadi unaelewa vizuri , hiyo ndio elimu na maarifa tunayoyataka, tena inaongeza vipato kwa walimu maana wanafunzi wananunua vitabu vya professor wao.
Majanga: kitabu kimeandaliwa na professor USA, mwalimu bongo anakitumia kugundishia asipokielewa vipi?, tunajimaliza wenyewe, tiwape elimu vijana wetu ambayo wataelewa na ku logic kwa kina.

Nasema ukweli, nilikuwa sijawahi ona university mtu masomo yote anapiga mia, akifail zaidi ni 90 , nendeni nje mkasome hizoengineer au medicine muone watu university wanapiga mabanda miaka yote semister zote, lugha inawa support.

University of Dar, makelele, Nairobi, wanafundisha kwa english, angalieni rank zake duniani kama zinalingana na nchi ambazo hazifundishi kwa lugha hiyo, mfano bupt au tsingua hiku chuo kipo china kina rank no 1 duniani kwa computer science, matoto ya hapo hayajui hata english lipe computer uone. Tusipende kuangalia sijui kenya wanaongea nini, tuwape vijana maarifa kenya itakupeleka wapi hapa duniani?
 
Changamoto kwenye lugha ya kingereza ipo kwa walimu na sio wanafunzi. Lea asilimia zaidi ya 90 walimu wetu hawaimudu lugha ya kingereza. Hivyo wakati wa kufundisha walimu wanafundisha masomo yao kwa kiswahili ilihali watoto watatahiniwa kwa kingereza. Hivyo hata kwenye huo utafiti, bado walikosema wanafunzi walifundishwa kwa kingereza utakuta walifundishwa kwa kinge-kiswahili zaidi halafu wakapewa mitihani ya kingereza.

Kama tunataka hali hii ibadilike ni lazima tuanze kwanza na walimu tena wote (sio wale wa solo la kingereza tu) vinginevyo tutapiga porojo.
 
Akili za intaprinyuaa hizi!!! Nani aliyekwambia wachina hawajui Kiingereza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umetoa mchango bora sana. Huku ukifundisha kiswahili na watu wakianza kupata mabanda watasema elimu imeshuka nk. Watoto hawasomi vitabu vya ziada kwasababu kusoma ni adhabu kubwa kisa lugha. Na taifa halitaweza kuendelea tukiwa na wasomi waliokariri maarifa
 
Huu mjadala na tafiti hazijaanzq leo. Ulianza toka awamu ya kwanza. Na mara zote tafiti zilionyesha kiswahili ni bora kufundishia. Wakoloni walitugundisha kwa kiingereza siyo kwamba tuwe na maarifa bali waweze kututuma kirahisi. Leo hii nchi nzima inawasomi waliokariri, wasioelewa kitu. Kasi ya kujipatia maarifa ni ndogo mno sababu ya lugha.
Kwa hiyo hawa waasisi wa nchi hii walikariri, wakajenga barabara, wakarusha ndege bila ajali,majengo, wakatibu wagonjwa, wakaanzisha wizara, ofisi, viwanda, sheria na mengineyo. Tatizo kizazi hiki kinapenda mshuko. Kiingereza ndio kina elimu bora na utaalam wa fani zote. Kama kiswahili kina elimu ya Engineering zote, Maths eg logarithm, integration, calculus poa. Kuna sayansi ya shule za msingi hayo maneno sijui ni lugha ya kabila gani! Wanafunzi wasome Elimu kama ilivyo chuoni siyo kuichachua. Kuna Dictionary nyingi tu za kumsaidia student asipoelewa. Kiswahili ni lugha isiyoweza kutoa elimu ya Kizungu kwa walengwa.
 
Mahitaji ya kingereza bado makubwa sana duniani lakini pia Kiswahili ni dhana muhimu sana Afrika esp huku kwetu. Waangalie njia nzuri ya kubalance hapo
Nani aangalie?Kwanini usitoe maoni yako?Unasubiri watu wengine waangalie ndo wafanye maamuzi halafu baadaye unakuja kulialia!Wabongo bhna!
 
Sera ya elimu ya Tanzania miaka michache iliyopita ilisema kwamba kiswahili kitatumika kama lugha ya kujifunzia mpaka chuo kikuu. Ni lini hili jambo litatekelezwa?

Katika tafiti zote zilizowahifanywa zote zinaonyesha kuwa kiswahili ni bora mara nyingi sana kikitumika kama Lugha ya kufundishia shule za sekondari na chuo kikuu.

Hapa kuna utafiti nilikuwa naupitia nimesikitika sana kuwa kama taifa hadi leo tunafundisha wanafunzi wetu kwa lugha wasiyoielewa, hivi kuna ujinga zaidi ya huu!!!?. Baadhi ya matokeo ya huo utafiti ni haya hapa.

Hapa wanafunzi walifundishwa topic ya reproduction kwa kiswahili na kiingereza na kupewa mtihani. Kwenye hiyo shule ya Ungulu walipofundishwa kwa kiswahili A zilikuwa 32 na F 0. Walipofundishwa kwa kiingereza A zilikuwa 0 na F 25. Yaani hapa kuna wanafunzi kibao wenye akili wanaachwa sababu ya Lugha.

View attachment 985216

Hapa walimu wenyewe waliulizwa kama wakifundisha kwa kiingereza wanaeleweka na dhana inaeleweki? Mvomero walimu watano walisema wanaeleweka na 11 walisema hawaeleweki. Shule ya Mtibwa walimu 13 walisema hawaeleweki na 1 akasema anaeleweka.

View attachment 985219

Hapa wanafunzi walifundishwa historia kwa kiingereza na kiswahili na kisha kupewa mtihani. Walivyofundishwa kwa kiswahili A zilikuwa 35 na F 0. walipofundishwa kwa kiingereza A zilishuka hadi 8 na F 2.

View attachment 985220

Wazazi pia waliulizwa iwapo watoto wao waliomaliza form 4 wanarudi nyumbani na maarifa yoyote, asilimia 70 walisema hapana.

View attachment 985218

Nafikiri mchawi mkubwa wa elimu ya Tanzania ni lugha ya kufundishia sekondari na chuo kikuu.
Utafiti wote wa huyu jamaa ni huu hapa.
Jamani Watanzania tunawaomba commonsense itawale,kumbukeni kwamba we are not leaving in isolation.Tumefanya makosa watoto wetu hawajui Kiingereza,sasa mnataka kuwatenga moja kwa moja na jamii ya kimataifa?Nilidhani mngemuomba ahakikishe kwamba watoto wetu wanajua Kingeraza kwa udi na uvumba,including kufundishwa darasani kwa Kingereza.Badala yake mnamuomba amalizie kazi ilikwisha anzishwa na inayoendelea ya kuua Kingereza.Ajabu sana.Mnataka kupoteza ndoto kabisa ya watoto wetu ya kusomea nje na hata kuwa diaspora sikumoja?
 
Kuwa na ndoto ya kuwa Diaspora au kusoma nje ya nchi inaonyesha watu walivyokosa matumaini na elimu yetu. Yaani tutumie kiingereza ili watu wakawe madiaspora na kusoma nje!!? Katika wtz 55m unafikiri ni wangapi watapata hiyo chance? watu wakiwa na maarifa ya ukweli na si kukariri hata wakiongea kiingereza cha kuungaunga dunia itawaheshimu. Tumeona kwa wachina, madaktari wa Cuba etc.
 
Kwa hiyo hawa waasisi wa nchi hii walikariri, wakajenga barabara, wakarusha ndege bila ajali,majengo, wakatibu wagonjwa, wakaanzisha wizara, ofisi, viwanda, sheria na mengineyo. Tatizo kizazi hiki kinapenda mshuko. Kiingereza ndio kina elimu bora na utaalam wa fani zote. Kama kiswahili kina elimu ya Engineering zote, Maths eg logarithm, integration, calculus poa. Kuna sayansi ya shule za msingi hayo maneno sijui ni lugha ya kabila gani! Wanafunzi wasome Elimu kama ilivyo chuoni siyo kuichachua. Kuna Dictionary nyingi tu za kumsaidia student asipoelewa. Kiswahili ni lugha isiyoweza kutoa elimu ya Kizungu kwa walengwa.

Wewe ni mshamba...

Samahani nakuita hivyo si kwa kukudhalilisha... unaweza kufundisha hayo yote kwa lugha ya kiswahili na kutumia maneno mapya ya kuazimia matashi ya kibantu.

Je, unafikiri maneno kama 'kipeo' na 'kipeuo' yalikujaje kwa mfano?

Tupo watu wenye uwezo wa kutafsiri na kutunga maneno yenye ladha ya kibantu na tukafundisha lolote-- kuanzia sanyansi, metafizikia hata yapitayokawaida. Labda tunafanya haya kwa nafasi zetu, labda kitambo utakuja kuziona kazi zetu, inawezekana hata humu tunafanya hivyo?

Nakukumbusha tu, usipoteze busara yako kwenye ukandiaji... Labda unaendelea kukua na kujifunza... Siku moja utakuja kujua ilivyo bora.

Nina wasi wasi wengi wanaoweza kuwa wanabeza na kukandia misimamo hii ya kiutamaduni na ustaarabu aidha ni vijana waliochini ya miaka 30 ama watu wazima ambao maisha na mifumo ya maisha yao imetawaliwa ama straarabu za mikumbo...

Aidha wabezaji wote hamuoneshi uwezo wa mashauri na fikra tunduizi.

Je, mnaridhikaje na majibu mapesi kwa maswali magumu? Je, mnafikiri kweli lugha ni kitu chenye kuleta 'maendeleo'?

Je, ninyi mmeshawahi kutafakari kuhusu nafasi 'ujuzi wa mawasiliano' katika maisha yetu ya kila siku?

Tuna matatizo lukuki hata katika matumizi ya lugha ya Kiswahili, achilia mbali kiingereza... Hata tukipitia michango ya wengi, uzi huu kutumika kama sampuli kwa ushahidi--matumizi ya lugha hayadhihirishi viwango, usomi na ubora--ni wazi iwe kiingereza, iwe kiswahili; mawasiliano ni ujuzi kando ya yote.

Sasa kabla ya kuwa vishadadizi wa lugha iliyohadhiwa kwa makusudi na mapana; tafadhali mfikiriage na yanayopasa hasa kwa wakati, hata kwa lugha yetu mama...

Tusiwe na soga za waghairishaji...
 
Mimi nafikiri tunadanganyana kujifanya hatukijali sana English .
Kama kweli tunataka kuwa washindani duniani hatuwezi kukikwepa English

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati tunaanza form one tulikuwa tunaambiwa we kariri tu utaelewa baadaye. Huhitaji kujifunza physics kwa kiingereza ili ushindane duniani. Unahitaji tu kujua kiingereza.
 
Kwa hiyo hawa waasisi wa nchi hii walikariri, wakajenga barabara, wakarusha ndege bila ajali,majengo, wakatibu wagonjwa, wakaanzisha wizara, ofisi, viwanda, sheria na mengineyo. Tatizo kizazi hiki kinapenda mshuko. Kiingereza ndio kina elimu bora na utaalam wa fani zote. Kama kiswahili kina elimu ya Engineering zote, Maths eg logarithm, integration, calculus poa. Kuna sayansi ya shule za msingi hayo maneno sijui ni lugha ya kabila gani! Wanafunzi wasome Elimu kama ilivyo chuoni siyo kuichachua. Kuna Dictionary nyingi tu za kumsaidia student asipoelewa. Kiswahili ni lugha isiyoweza kutoa elimu ya Kizungu kwa walengwa.
Kwahiyo calculus na mambo ya engeneering yanaweza kufundishwa kwa kireno, kigiriki, kikorea,kichina, kiitaliano, kijerumani, kiholanzi, kijapan na si kiswahili!!!? kwasababu gani?
 
Changamoto kwenye lugha ya kingereza ipo kwa walimu na sio wanafunzi. Lea asilimia zaidi ya 90 walimu wetu hawaimudu lugha ya kingereza. Hivyo wakati wa kufundisha walimu wanafundisha masomo yao kwa kiswahili ilihali watoto watatahiniwa kwa kingereza. Hivyo hata kwenye huo utafiti, bado walikosema wanafunzi walifundishwa kwa kingereza utakuta walifundishwa kwa kinge-kiswahili zaidi halafu wakapewa mitihani ya kingereza.

Kama tunataka hali hii ibadilike ni lazima tuanze kwanza na walimu tena wote (sio wale wa solo la kingereza tu) vinginevyo tutapiga porojo.

Mkuu hapo umezungumza jambo la maana. Waalimu watarajiwa wa lugha ya Kiingereza shule za msingi na sekondari lazima serikali iwapelekwe kwa wingi vyuo vikuu vya nchi za Kusini mwa Afrika kusomea degree za lugha ya Kiingereza. Nchi hizo ni Malawi, Zambia, Zimbabwe n.k

Sharti hili la Waalimu wa lugha Kiingereza kuwa na degree ni la lazima ili waweze kufundisha lugha hii ya kigeni ktk shule zote za serikali / shule za kata.
 
Wewe ni mshamba...

Samahani nakuita hivyo si kwa kukudhalilisha... unaweza kufundisha hayo yote kwa lugha ya kiswahili na kutumia maneno mapya ya kuazimia matashi ya kibantu.

Je, unafikiri maneno kama 'kipeo' na 'kipeuo' yalikujaje kwa mfano?

Tupo watu wenye uwezo wa kutafsiri na kutunga maneno yenye ladha ya kibantu na tukafundisha lolote-- kuanzia sanyansi, metafizikia hata yapitayokawaida. Labda tunafanya haya kwa nafasi zetu, labda kitambo utakuja kuziona kazi zetu, inawezekana hata humu tunafanya hivyo?

Nakukumbusha tu, usipoteze busara yako kwenye ukandiaji... Labda unaendelea kukua na kujifunza... Siku moja utakuja kujua ilivyo bora.

Nina wasi wasi wengi wanaoweza kuwa wanabeza na kukandia misimamo hii ya kiutamaduni na ustaarabu aidha ni vijana waliochini ya miaka 30 ama watu wazima ambao maisha na mifumo ya maisha yao imetawaliwa ama straarabu za mikumbo...

Aidha wabezaji wote hamuoneshi uwezo wa mashauri na fikra tunduizi.

Je, mnaridhikaje na majibu mapesi kwa maswali magumu? Je, mnafikiri kweli lugha ni kitu chenye kuleta 'maendeleo'?

Je, ninyi mmeshawahi kutafakari kuhusu nafasi 'ujuzi wa mawasiliano' katika maisha yetu ya kila siku?

Tuna matatizo lukuki hata katika matumizi ya lugha ya Kiswahili, achilia mbali kiingereza... Hata tukipitia michango ya wengi, uzi huu kutumika kama sampuli kwa ushahidi--matumizi ya lugha hayadhihirishi viwango, usomi na ubora--ni wazi iwe kiingereza, iwe kiswahili; mawasiliano ni ujuzi kando ya yote.

Sasa kabla ya kuwa vishadadizi wa lugha iliyohadhiwa kwa makusudi na mapana; tafadhali mfikiriage na yanayopasa hasa kwa wakati, hata kwa lugha yetu mama...

Tusiwe na soga za waghairishaji...
Wewe na wenzako wote mnaolilia kisWahili ni vile tu hatujuani hapa....

Usikute wanao wote unawalipia mamilioni huko MaShule ya kizungu.

CCM tunajua akili zenu....mnataka muendelee kaa maofisini humo mje mrithishe watoto wenu... makapuku mnaowapamba kwa Kiswahili waendelee kupinda migongo mashambani.
Tunasema hivi ENOUGH IS ENOUGH...

MIAKA 55 YA KUCHEZA NA ELIMU ISHAWATOSHA.

TUTAPELEKA WATOTO HATA ZIMBABWE... TUKUTANE KWENYE INTERVIEWS.

PIMBI NYIE.
 
Kwahiyo calculus na mambo ya engeneering yanaweza kufundishwa kwa kireno, kigiriki, kikorea,kichina, kiitaliano, kijerumani, kiholanzi, kijapan na si kiswahili!!!? kwasababu gani?
Nenda kawaulize TUKI hili swali.
 
Wewe na wenzako wote mnaolilia kisWahili ni vile tu hatujuani hapa....

Usikute wanao wote unawalipia mamilioni huko MaShule ya kizungu.

CCM tunajua akili zenu....mnataka muendelee kaa maofisini humo mje mrithishe watoto wenu... makapuku mnaowapamba kwa Kiswahili waendelee kupinda migongo mashambani.
Tunasema hivi ENOUGH IS ENOUGH...

MIAKA 55 YA KUCHEZA NA ELIMU ISHAWATOSHA.

TUTAPELEKA WATOTO HATA ZIMBABWE... TUKUTANE KWENYE INTERVIEWS.

PIMBI NYIE.

Ndugu,

Umekosa 'kishamirisho' katika kulizungumzia jambo husika.

Bado haujaielewa 'kazi' ya elimu. Kupeleka watoto nje kwa minajili ya elimu si suluhu; vile vile kutumia gharama kubwa kusomesha mtoto shule ya gharama. Je, hivi wewe unauelewa walau kiasi, kuhusiana na uchumi? Unadhani kuna uwezekano ama nafasi kiasi gani kwa watu kugharamikia elimu ya gharama? Hivi, unauelewa wowote kuhusu dhana ya 'maendeleo endelevu'?

Basi hata kwa hicho kiingereza kidogo ulichonacho, nenda katafute mtandaoni 'Sustainable Development Goals'... Kwa taarifa yako, maendeleo na mipango ya nchi ni zaidi ya 'mawazo ya kujisikia sikia tu'.

Kuna kanuni na mbinu.

Fungua macho na masikio.
 
Back
Top Bottom