Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Oktoba, 2022
Mapendekezo 18 ya Ripoti yanasomwa na Prof. Rwekaza Mukandala
- Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe, pia mikutano ya ndani ya vyama hivyo
- Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho
- Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote.
- Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri ya yeyote, na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa mahakamani
- Wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi wateuliwe na kamati inayoongozwa na jaji mkuu wa Tanzania, akisaidiwa na jaji mkuu wa Zanzibar. Pia, nafasi itangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi
- Matokeo ya Rais jahojiwe Mahakamani
- Wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria na maadili
- Tume ya taifa ya uchaguzi ipewe fedha kwa wakati
- Itungwe sheria kusimania shughuli za tume ya uchaguzi, pia iwepo sheria moja ya kusimamia chaguzi zote, maafisa wa uchaguzi wanaoengua wagombea bila sababu maalumu wawajibishwe
- Matumizi ya tehama kwenye uchaguzi yaboreshwe
- Sharti ya uwepo wa sera ya jinsia liwepo kwenye sheria za vyama vya siasa, pia ushiriki wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi isipungue 40%
- Sheria zinazokwamisha ushiriki wa wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya
- Juhudi za ushirikishwaji wa vijana kwenye siasa ziongezwe
- Serikali iongeze utoaji wa elimu ya uraia, pia ifundishwe kwenye ngazi zote za elimu, pia mtaala wa elimu uzingatoe elimu ya uraia.
- Swala la rushwa litamkwe katika katiba ya nchi ili wananchi waelewe
- Kuanzishwe utaratibu wa mijadaa kila mwaka itakayohusisha viongozi wakubwa wa kitaifa na kisiasa ili kudumisha mshikamano, mahakama iwe ni mamlaka ya mwisho ya kuamua pindi maridhiano yanapokwama
- Wanahabari waunde chombo cha kusimamia wanahabari na vyombo vyao, vyombo vya umma vitoe muda sawa wa kutangaza habari za wagombea wa vyama vyote kwa usawa, uwepo mchakato wa wazi wa kuwajibisha vyombo vya habari badala ya kufungiwa pekee na mkurugenzi wa habari na mawasiliano
- Mchakato wa katiba mpya uendelee, hata hivyo mjadala wa kitaifa kuhusu katiba mpya uanze kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ili kujadili ajenda muhimu za muungano, mamkala ya Rais, Rushwa, tume ya uchaguzi n.k
Afadhali umeedit No18.
Ungeharibu thread.