Prof. Mbarawa umejiandaa baada ya uwaziri kuisha? Wenzio wawili wana kinga ya kutoshitakiwa

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,348
17,870
Nakukumbusha kaka yangu, mtanzania mwenzangu Bwana Makame Mbarawa kuna mawaziri wa zamani Bw. Yona na Bw. Mramba waliishia jela kisha wakaenda kufagia vyoo hospital za umma baada ya uwaziri wao.

Hili sakata la uwekezaji wa bandari za Tanganyika unaweza kuja kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma ukajikuta unapanda karandinga,au kosa la uhujumu uchumi kisha unaenda kulala saa 9 jioni ndani ya kuta za jela.

Yule aliyekupa kibali cha kuweka saini mkataba wa DP World ana kinga, kibaya zaidi hati ya ruhusa ya kumwakilisha kuingia mkataba ina makosa huenda ikaja kuthibitika ni batili kisheria.

Mchakato wa kuingia mkataba na mkataba wenyewe inadaiwa na wanasheria wasomi wenzio kuna makosa mengi ikiwamo kuvunja sheria za nchi na katiba ya nchi.

Nakukumbusha kwamba Spika wa bunge ana kinga na ndiyo maana ana kiburi cha kutukana hadi wazee.
Sijajua kama mwanasheria mkuu na wewe Waziri mnayo kinga ya kutoshitakiwa hapo baadae?

Nakukumbusha mamlaka ya juu iliyopo wakati huu haitakuwepo pale miaka yote kukulinda kama sasa. Wala wastaafu wale wengine hawataishi milele kukutetea na kukulinda. BEWARE of the jail, KATAA RUSHWA, KATAA JELA kiongozi wangu. Jela siyo mahali pazuri. Kule uende kwa bahati mbaya tu siyo kwa ajali za kisiasa za kujitakia.

Ukibisha muulize Bw. Sabaya. Bora ulindwe na Deep State utasalimika. Kwa nionavyo mimi huu mtego wa bandari hauna harufu ya kulindwa na Deep State.

Wanasheria humu JF mnisaidie majibu kuhusu AG kama anayo kinga na yeye.

Ni hayo tu.
 
Nakukumbusha kaka yangu, mtanzania mwenzangu Bwana Makame Mbarawa kuna mawaziri wa zamani Bw. Yona na Bw. Mramba waliishia jela kisha wakaenda kufagia vyoo hospital za umma baada ya uwaziri wao.

Hili sakata la uwekezaji wa bandari za Tanganyika unaweza kuja kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma ukajikuta unapanda karandinga,au kosa la uhujumu uchumi kisha unaenda kulala saa 9 jioni ndani ya kuta za jela.
Mwenye macho haambiwi tazama.
 
Back
Top Bottom