Prof. Lipumba huifahamu Sheria, acha ichukue Mkondo wake

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,370
11,091
Makala ifuatayo meandikwa na HAPPINESS KATABAZI

KWA mara ya pili sasa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Professa Ibrahim Lipumba amekuwa akiitisha mikutano na waandishi wa habari kuzungumzia vurugu za kidini zilizotokea hapa nchini hususani jijini Dar es Salaam.

Profesa Lipumba pamoja na mambo mengine amekuwa akisema tena kwa ujasiri kuwa kesi ya jinai namba 245/2012 inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake 49 iliyofunguliwa na upande wa jamhuri Oktoba 18 mwaka huu, ambayo ipo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Victoria Nongwa na inendwa na wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka wakati upande wa utetezi unatetewa na wakili wa kujitegemea Mansoor Nassor ilipaswa iwe ya madai na siyo jinai na kwamba eti Ponda alistahili dhamana na kuwa anafanya mpango wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete amshauri serikali ifanye mazungumzo na Maimamu wa misikiti ili waweze kupata suluhu ya tatizo la vurugu hizo za kidini.

Binafsi ni mwandishi wa habari za mahakamani hapa nchini na kesi hii ni miongoni mwa kesi ambazo minaziudhulia siku ilipofunguliwa kwa mara ya kwanza ,na hata Novemba Mosi mwaka huu, kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kutajwa na wakili wa serikali Kweka aliieleza mahakama kuwa uplelezi wa shauri hilo umekamilika nilikuwepo tangu saa moja asubuhi mahakamani hapo, na hata hiyo Novemba 15 mwaka huu, panapo majaliwa ya mwenyezi mungu kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya upane wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa nitakuwepo ndani ya ukumbi namba moja wa mahakama hiyo kwaajili ya kuiripoti kesi hiyo kwa uweledi wa aina yake.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ya kesi hiyo inayomkabili Ponda na wenzake ambayo nakala yake ninayo, ina jumla ya mshitaka matano ambapo mashitaka yote matano yanamkabili Ponda na mashitaka manne yanamkabili mshitakiwa 2-50.

Kosa la kwanza ni la kula njama kutenda kosa kinyume na kifungu cha 384 cha Sheri ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, ambapo washitakiwa wote wanaidaiwa kuwa Oktoba 12 mwaka huu katika eneo la Chang'ombe Marksi walikula njama kwania ya kutenda kosa. Kosa la pili ni kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kinyume na kifungu cha 85,35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, kuwa Oktoba 12 mwaka huu, katika eneo la Chang'ombe Markasi ,kwa jinai na wasipokuwa na sababu waliingia kwenye kiwanja cha eneo hilo kinachomilikiwa na Kiwanda cha Agritanza.

Wakati kosa la tatu ni la kujimilikisha kwa jinai kiwanja hicho kinyume na kifungu cha 86 na 35 cha Sheria hiyo kuwa kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu, katika eneo hilo pasipo na uhalali washitakiwa wote katika hali ya kupelekea uvunjifu wa amani,walijimilikisha kwa nguvu ardhi ya kampuni ya Agritanza.

Shitaka la nne ni la wizi kinyume na kifungu cha 258 na 225 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 kuwa washitakiwa wote kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu, waliiba vifaa, malighafi kama nondo, matofali, kokoto zenye jumla ya Sh 59,650,000 mali ya Kampuni hiyo.

Aidha shitaka la tano ni kwaajili ya Ponda peke yake ambalo ni la uchochezi kinyume na kifungu cha 390 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 kuwa Oktoba 12 katika eneo hilo la Chang'ombe kwa maelezo kuwa yeye ni Katibu aliwashawishi wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao watende makosa hayo.Na washitakiwa wote walikanusha mashitaka hayo na Hakimu Nongwa akasema mashitaka yote yanadhamana kwa mujibu wa sheria na akatoa masharti ya dhamana kwa mshitakiwa 2-50.

Na kusema ili wapate dhamana nilazima kila mmoja awe na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini bondi ya milioni moja, licha Hakimu Nongwa alisema mahakama yake haiwezi kutoa dhamana kwa Ponda licha anastahili dhamana kwasababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kufunga dhamana ya Ponda kwa mujibu wa kifungu cha 148(4) cha Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.Na hati hiyo ya DPP inakuwa imeifunga mikono mahakama hadi hapo siku DPP atakapoona haja ya kuiondoa hati hiyo hivyo Ponda ataendelea kusota rumande hadi hati hiyo itakapoondolewa na DPP.

Kauli ya Profesa Lipumba kuhusu kesi ya Ponda imenifanya nianze kuamini kuwa hata ukiwa msomi wa hali ya juu kama Profesa Lipumba unaweza pia kutoa maoni ya kipuuzi ambayo hayapaswi kutolewa na msomi wa aina yake mbele ya umma.

Tumuulize huyu Lipumba kabla ya kutoa kauli hizo aliwasiliana na wanasheria wa chama chake wakampa ushauri wa kisheria wa nini cha kuzungumza mbele ya umma kuhusu kesi ya Ponda inayooendelea pale katika Mahakama ya Kisutu?Naamini hakupata ushauri mzuri toka kwa wanasheria wa chama chake au kama alipata basi wanasheria huo waliamua kumpatia ushauri ambao umemdhalilisha Lipumba mbele ya jamii ya wasomi wa sheria na jamii inayoheshimu utawala wa sheria hapa nchini.

Profesa Lipumba kwanza kabla ya kutoa kauli hizo kuhusu kesi ya Sheikh Ponda kuwa kesi hiyo ya jinai namba 245 /2010 eti ilipaswa iwe ya jinai, ungeitafuta hati hati ya mashitaka ungeisoma vizuri na ungeweza kuelewa makosa wanayoshtakiwa nayo ni ya madai au jinai halafu ungeenda kuisoma Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code;2002),Sheria ya Mashauri ya Madai (Civil Procedure Code:2002) na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act, RE:2002) na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naamini vingekupa mwongozo mzuri sana kwa kufahamu mashitaka yanayowakabili, kifungu gani kimetumika kufunga dhamana ya Ponda na ni kwanini dhamana yake imefungwa na pia ungeweza kufahamu vyema majukumu ya mahakama ni ya pili nay a serikali ni yapi.

Na hapo ndipo ninapokubaliana na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa wiki ambayo inawataka wanasiasa waache unafki kwani wao wanaisasa wanaishi maisha kifahali na uhuru wakati wale wafuasi wao wanaishi maisha ya tabu na wamekuwa wakiwapandikisha uongo wafuasi wao.

Sasa kwa kauli hiyo ya Kikwete minaona katika matamko hayo ya Lipumba inamgusa pia, kwani uenda Lipumba anataka kujipatia umaarufu chee wa kisiasa kupitia kesi ya Ponda ila hafahamu kuwa mahakama haiendeshwi wala haisikilizi kauliza wanasiasa pindi inapofanyakazi zake kwa mujibu wa sheria.

Wewe Lipumba kwakuwa unasema kesi ya jinai ya Ponda ilipaswa iwe ni ya madai, hivi ni kwanini unashindwa kuomba kazi ya kuwatetea washitakiwa hao kama (Bush Lawyer )mahakamani hapo na siku kesi ikianza kusikilizwa ukawasilisha hilo pingamizi lako lakutaka kesi hiyo ya jinai ifutwe kwani imefunguliwa kimakosa ilitakiwa washitakiwa hao wafunguliwe kesi ya madai).
Maana unapozungumzia kesi hiyo kwenye majukwaa na mbele ya waandishi wa habari haimsaidii Ponda kwa lolote zaidi zaidi unazidi kumgandamiza Ponda bila wewe kujua?

Profesa mzima tena wa uchumi unayeheshimika nchi mbalimbali unashindwa kufahamu mtu anayetuhumiwa kwa kosa la wizi au kuingia kwa nguvu kwenye kiwanja au chochezi basi mtu huyo makosa hayo yataangukia kwenye jamii ya makosa ya jinai? Lakini wewe sijui kwa upotoshaji au unalako jambo unadiriki kujitokeza adharani kuuposha umma kwa kusema walipaswa washitakiwe kwa kesi ya madai?

Mwenyekiti mzima wa chama kikubwa kama CUF,ambacho chama hicho chini ya uongozi wako ni miongoni mwa chama kilichokuwa kidai Tanzania iandike Katiba mpya kwa madai kuwa Katiba ya sasa imepitwa na wakati,na kwa maana hiyo unaifahamu vyema ibara za Katiba hiyo , unashindwa kuifahamu Katiba ya nchi ambayo Ibara ya 59B(1) inayosomeka hivi; "Kutakuwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye atateuliwa na Rais,kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoanishwa katika ibara ndogo (2) ya ibara 59 na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muad usiopungua miaka kumi.

Ibara ya 59(4) inasema; ‘Katika kutekeleza mamlaka yake,Mkurugenzi wa Mashitaka atakuwa huru ,hataingiliwa na mtu yeyote au mamlaka yeyote na atazingatia mambo yafuatayo; (a) nia ya kutenda haki, kuzuia matumuzi mabaya ya taratibu za utoaji haki na maslahi ya umma.

Na kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai, kina mpa mamlaka DPP kufunga dhamana ya mshitakiwa na ndiyo kifungu hicho kilichotumia na DPP kufunga dhamana ya Ponda.

Ni kweli dhamana ni haki ya kila mtu ila kuna baadhi ya makosa hayana dhamana na mfano kesi ya mauji, utakatishaji fedha haramu( Money Laundry),unyang'anyi wa kutumia silaha(Amry Robbery) mauji,uhaini na ugaidi (Terrorisms) lakini kama kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, kinampa mamlaka DPP kumfungua dhamana mshitakiwa anayekabiliwa na makosa yanayodhaminika.

Sasa kwa mtiririko huo ,misimwelewi Lipumba ana ajenda gani iliyojificha kwenye hii kesi ya Ponda.Kwani Ponda na wenzake bado ni watuhumiwa kama wengine tub ado hajaukumiwa.DPP ametumia madaraka aliyonayo kufunga dhamana ya Ponda na kuwafungulia mashitaka ya jinai washitakiwa hao ,sasa sijui tabu inatoka wapi.

Mbona viongozi wa iliyokuwa Taasisi ya Upatu (DECI) walivyofunguliwa kesi pale Mahakama ya Kisutu mwaka 2009, na makosa yanayowakabili yalikuwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria lakini DPP huyu huyu Dk. Feleshi aliwasilisha hati ya kuwafungua dhamana na vigogo ambao kesi yao iliyopo mbele ya Hakimu Stewart Sanga imefikia hatua ya wao wameanza kujitetea,aliwafungia dhamana na walisota gerezani kwa zaidi ya miezi mitatu, mbona hatukuwasikia wanasiasa wala waumini wa dini ya Kikristo au wewe Lipumba na wale wafuasi wengine mnaondamana kila Ijumaa kushinikiza Ponda aachiliwe huru, hamkuandamana kushinikiza waachiliwe huru na kwamba kesi yao vigogo wa DECI ni ya madia?

Tuachane na uhuni huu unaofanywa na wasiasa waliopoteza dira na mwelekeo na waliofirisika kisiasa ambao wao masuala hatarishi na yanayoingilia uhuru wa mahakama ambao uhuru wa mahakama umeainishwa wazi katika Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inasomeka hivi; "Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki ,mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na Sheria za Nchi'.

Na ibara 107A (1) ya Katiba ya nchi inasema "Mamlaka yenye mamlaka ya mwisho ya utoaji haki katika jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama.

Kwahiyo kama kesi inayomkabili Ponda ni ya madai , si jukumu la wewe Lipumba sasa kusema hilo ni jukumu la Mahakama siku ikifika itasema hivyo.

Mwisho napenda kuwaasa wale wanaojiita wafuasi wanaojiita wao ni wafuasi wa Ponda na sheikh Farid waache kushiriki kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kisingizo cha kuishinikiza serikali na mahakama imwachilie huru Ponda kwani kufanya hivyo ni wazi wakae wakijua watakuwa wanafunja sheria za nchi watajikuta wanaingia matatani na wao waishia kwa kufunguliwa kesi za jinai mahakamani na kutupwa jela.

Na wale wahuni wachache ambao ni wazi wamechoka kuishi Tanzania kwenye amani wanaoleta vurugu za kidini kwa kisingizio eti wanaitetea dini ya kiislamu, wakome mara moja na kwa uwezo wa mungu hiyo dhamira yao mbaya na kishetani ya kutaka kuingiza Tanzania kwenye machafuko haitafanikiwa nao mwisho wa siku wataambulia kipigo kutoka kwa wanausalama wetu na kufikishwa mahakamani na mwishowe kupelekwa kupumzika katika gereza la Segerea,Keko na kula ugali wa bure na kuwa chini ya ulinzi.

Naendelea kuvipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwadhibiti wahuni hawa wachache wanajaribu kutaka kuatarisha usalama wa taifa letu kwa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.Na ninaviomba vyombo vya dola viwashughulikie kikamilifu wale wote wanaoleta vurugu kwa kisingizio cha kutetea dini ya kiislamu wakati bado wakristo,waislamu na wapagani hapa nchini tunaishi kwa upendo,tunafanyakazi pamoja.

Mwisho nimalizie kwa kuwataka waandishi wa habari wenzangu na wanaharakati na wanasiasa ambao huko nyuma tulikuwa mstari wa mbele sana kushikilia bango hadi kuandaa maandamano na kutengeneza mabango na fulani za kulaani tuhuma za ufisadi katika Mkataba wa Dowans,Richmond, mauji ya mwanahabari mwenzetu David Mwangosi,kufungiwa kwa vyombo mbalimbali vya habari.

Mbona wanahabari wenzangu wengi,wanaharakati, na wanasiasa machahari mbona tumeonekana kuwa wapole sana katika matukio haya yanayotaka kuleta chochoko za kidini?

Hivi je matukio haya yanayoashiria chokochoko ya udini siyana madhara ya haraka,wazi ambayo yasingezibitiwaharaka na vyombo vya dola na hekima ya viongozi wa dini ya Kikristo na wale wa kiislamu leo hii Tanzania ingekuwa imeingia kwenye machafuko ya kidini?

Tuache unafki,amani ni kitu muhimu sana pote pale duniani na chenye kipaumbele halafu hayo mambo mengine yanafuata.Kwani bila ya kuwepo na amani huo ufisadi usingenyika.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

Source: Happiness Katabazi - Tanzania Daima

Mwana Mama huyu ana Shahada ya Sheria na ni Mwandishi wa Habari za Mahakamani.

Mimi nasema Hongera Mwandishi kwa kuona mbali kwani kuwa Professor wa Uchumi sio kujua kila kitu
 
huyu mama ni mdini, hakumuelewa prof Lipumba bali kilichomsukuma kumshambulia ni UDINI NDIO UNAOMSUMBUA, tena anaonekana mama huyu ni bwenga wa kule kashozi, aende akawashe koroboi auze nyata.
 
nilipo iona hii thread ilibidi nirudi kuangalia jina,aiseee jina linajeeleza la kikisto actually uliyoyatoa tuliyategemea yawe hivyo,eti mwandishi wa habari nenda kaandike habari za kanisani mdini mkubwa wewe.
 
huyu mama ni mdini, hakumuelewa prof Lipumba bali kilichomsukuma kumshambulia ni UDINI NDIO UNAOMSUMBUA, tena anaonekana mama huyu ni bwenga wa kule kashozi, aende akawashe koroboi auze nyata.

Nahisi profes LIPUMBA alikuwa bingwa wa kudesa siiamini hiyo doctorate yake pengine wazungu walimuita ili kuverify ni namna gani mtu aliyepata uprofesa wa kudesa anavyoweza kutoa mada za uongo uongo. HAJUI SHERIA KATANGULIZA HISIA ZA MOYONI NDIO SABABU HAWEZI KUWA HATA DIWANI KULE SIKONGE KWAO
 
Ifuatayo ni sehemu ya makala iliyoandikwa na Mwandishi Pascal Mayega kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo kuhusu uamuzi wa Professor Ibrahim Lipumba kuhaingikia dhamana ya wanaodaiwa Waislam walioshambulia makanisa na kufanya maandamano.............Endelea..........

Iweje leo magaidi waliochoma makanisa, wakaiba pombe na nyama ya nguruwe na kuharibu mali hata na za Waislamu wanatambulishwa kama waislamu?

Baba askofu Alex Malasusa alipokuwa akiomboleza kwenye majivu ya Mbagala alisema:

"Watu hawa wamepewa hadhi ya kuitwa ‘Waislamu" wengi hawakumwelewa. Ni kwamba baba Askofu Malasusa anaithamini dini ya Kiislamu na dini nyingine, lakini anaamini kuwa Mwislamu wa kweli hawezi kutenda uovu wa kikafiri kama ule uliofanyika Mbagala!
Siyo sahihi hata kidogo kuendelea kuwatambua watu wanaotuhumiwa kwa vitendo vya kigaidi kwa kutumia dini ya Kiislam.

Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, anapohangaika kutaka magaidi waachiwe anajionyesha alivyo. Waislamu walioumizwa kwa vitendo vya magaidi hawa wanamwelewaje Lipumba? Viongozi wetu sasa tuwapambanue.
Rais wangu ni jambo la busara sasa kutumia muda mwingi kuielimisha jamii ili ipate kutambua tofauti kubwa iliyopo kati ya dini ya Kiislamu na ugaidi. Tusipofanya hivyo sasa tutakuwa tunaielekeza nchi yetu kwenye machafuko ya kumwaga damu. Hali hii ni hatari lazima ishughulikiwe kwa uzito unaostahili.
Wanasiasa wanaodai wahalifu hawa waachiwe kwa kisingizio kwamba wanawatetea Waislamu ni wanasiasa uchwara.

Ni waishiwa ambao wako tayari hata kutumia vikundi vya kigaidi wakidhani kwamba watafanikisha malengo yao yaliyoshindikana ya kutwaa madaraka.
Ndugu Rais wapuuze wanasiasa uchwara hawa. Kama serikali itaendelea kuwashikilia wahalifu hawa viongozi wa vyama vya siasa walio nyuma ya ugaidi huu watafunguka wengi.

Inaogopesha kuona hata baadhi ya vyama vilivyoonekana kuwa makini vimetumbukia katika mtego huu wa kuamini kuwa waliochoma makanisa, kuiba na kuharibu mali za waumini wema walikuwa wanatetea Uislamu. Huu ni unafiki wa kisiasa wa kutaka kusaka kura kwa uchaguzi ujao. Kiongozi anayesaka kura hata za magaidi ni gaidi. Huyo hatufai!

Rais wangu ni nani ataipunguza kasi hii ya kuelekea Ikulu ili kwanza tutatue hili tishio la ugaidi? Anayedhani ugaidi unaweza kumsaidia kuingia Ikulu ana mawazo hafifu! Yampasa atambue kuwa kila kiingiacho kwa hila hutoka kwa hila! Viongozi wanaotetea ugaidi ni magaidi nao ndio wanaowadhamini magaidi.
 
Makala za Pascal Mayega huwa zinanivutia sana.

Jambo moja la kweli ni kwamba waliofanya uhalifu wa kuchoma makanisa hawana hadhi ya kuitwa waislam.
 
Lipumba kacheza karata zake vibaya katika siasa. Alitaka ku wa win waislamu lakini kakosea. Wale waliofanya yale sii waislamu kwa maana ya uislamu. Aliyemshauri kampoteza. Profesa umecheza garasha
 
Lipumba kacheza karata zake vibaya katika siasa. Alitaka ku wa win waislamu lakini kakosea. Wale waliofanya yale sii waislamu kwa maana ya uislamu. Aliyemshauri kampoteza. Profesa umecheza garasha......

Na hapo ndipo ninaposema kwamba Lipumba kapotoshwa vibaya na washauri wake.

Huwezi kusema eti wajinga waliochoma makanisa na kuiba pombe ni waislam.
 
Lipumba na Seif ni lao moja huku Lipumba akimtetea Sheikh ponda mwenzake seif anamtetea sheikh Halifa wote hao wanaowatetea inasemekana uraia wao ni questionable.Lipumba umetokota zaidi ya kuchemsha
 
Greenwhich Hapo kwenye nyekundu kafiri=asiye muislamu mf: mkristo
- kwahiyo mwandishi anataka kutuambia vitendo hivyo hufanywa na wakristo, wapagani na dini nyingine ndogondogo na si waislamu; kama tulivyo zoea dunia nzima.. Ktk hili mwandishi kaonyesha udhaifu mkubwa.
 
Last edited by a moderator:
huyu mama ni mdini, hakumuelewa prof Lipumba bali kilichomsukuma kumshambulia ni UDINI NDIO UNAOMSUMBUA, tena anaonekana mama huyu ni bwenga wa kule kashozi, aende akawashe koroboi auze nyata.
Ingekuwa vizuri ungejibu hoja zake moja baada ya nyingine ili kudhihirisha kuwa ni mdini otherwise unaonekana mwenyewe ni kilaza usiyeweza kutetea hoja ila unabaki kusema mdini bila sababu/hoja.Jibu hoja zake ndo tujue ni mdini au lah!kama huwezi basi we ndo mdini this is my conclusion,nitaridhika sana ukijibu kwa hoja
 
huyu mama ni mdini, hakumuelewa prof Lipumba bali kilichomsukuma kumshambulia ni UDINI NDIO UNAOMSUMBUA, tena anaonekana mama huyu ni bwenga wa kule kashozi, aende akawashe koroboi auze nyata.

Mimi nafikiri ingekuwa busara kwako kutueleza kwa hoja tofauti ya wewe na H.K katika kumuelewa Lipumba badala ya kutuainishia kabila, dini na jinsia ya mwandishi ambavyo si sehemu muhimu ya mada.

Hapo kwenye bold ndio kunakonishinda mimi katika hii vita yenu ya dini. Ndio mafundisho yenu?
 
hata waislam, mkuu wa mkoa na viongoz wengine wanasema waliochoma makanisa na uharibifu mwingine ni WAHUNI
so Lipumba anataka kutuaminisha kuwa WAHUNI= WAISLAM kitu ambacho si kweli hata kidogo.
waislam wa kweli ni wema na hawana mambo ya k-i-p-u-m-b-a-vu kama yale.

nategema waislam wakweli watampinga Lipumba.
 
huyu mama ni mdini, hakumuelewa prof Lipumba bali kilichomsukuma kumshambulia ni UDINI NDIO UNAOMSUMBUA, tena anaonekana mama huyu ni bwenga wa kule kashozi, aende akawashe koroboi auze nyata.
nilipo iona hii thread ilibidi nirudi kuangalia jina,aiseee jina linajeeleza la kikisto actually uliyoyatoa tuliyategemea yawe hivyo,eti mwandishi wa habari nenda kaandike habari za kanisani mdini mkubwa wewe.
Demu mwenyewe anaitwa Happyness sasa unategemea nini, udini tu umemjaa na njaa zake......

Kama nyinyi ndio mawakili wa upande mnaouwakilisha, hivi kweli mna hoja mbele za watu?

Sioni mlichoandika zaidi ya kuonesha zao la malezi mliyopata kwa wazazi na viongozi wa dini zenu. Kama haya huu ndio utetezi wenu basi niwashauri msijihusishe na mambo ya siasa ama migomo yoyote ya kijamii kwani mbele ya mahakama mtakuwa asusa ya sheria.

Hii ni hoja inapaswa kujibiwa. Weledi wa mtu na uthabiti wa anachokitetea huonekana kwa hoja na sio hayo yaliyopo kwenye bold.

Mlipaswa kuonesha ni wapi na wapi hamkubaliani na mwandishi na kwa msingi upi. Yeye (mwandishi) ametueleza ni kwa nini na kwa msingi upi hakubaliani na hoja ya Lipumba na mimi binafsi nimemwelewa kwani ameweka ushahidi wa kubeba anachokitetea, nilitegemea ambaye haridhiki na maelezo yake naye angefanya hivyo.

Kwa kuwa tunawafahamu, nategemea maajabu zaidi watakapofika kaka zenu Ritz, Barubaru, Rejao, Malyenge, zomba, mpemba mbishi, Ami na wengineo.

Kwa wale wenye mawazo yenye akili hawatajadili mauongo ya mwandishi, kabila wala dini yake, hao watajikita kwenye mambo ya msingi yanayohusiana na mada hii
.
 
kwani imethibiti wapi na lini kuwa waliokuwa ndani ndio waliochoma makanisa??? Mbona walikamtwa wapagani cku zile na wakiristo na baada ya kuonekana si waislamu wakapewa dhamana na ndio imetoka hio, ponda yeye alikuwa chang'ombe kwenye uwanje au hayo makanisa yaliochomwa yako pale uwanjani chang'ombe???
 
Waislam nchini kote waungane na kumtaka Lipumba awaombe radhi kwa kuwahusisha na wahuni,vibaka na magaidi!
 
hata waislam, mkuu wa mkoa na viongoz wengine wanasema waliochoma makanisa na uharibifu mwingine ni WAHUNI
so Lipumba anataka kutuaminisha kuwa WAHUNI= WAISLAM kitu ambacho si kweli hata kidogo.
waislam wa kweli ni wema na hawana mambo ya k-i-p-u-m-b-a-vu kama yale.

nategema waislam wakweli watampinga Lipumba.

Halafu waziri wa mambo ya ndani aliposema ni wahuni walio choma makanisa mkambishia sasa mnarudia kauli yake na kukubali ama kweli nyinyi ni vigeugeu kama kilivyo kitambulisho chenu
 
Lipumba kacheza karata zake vibaya katika siasa. Alitaka ku wa win waislamu lakini kakosea. Wale waliofanya yale sii waislamu kwa maana ya uislamu. Aliyemshauri kampoteza. Profesa umecheza garasha.....

Mkuu, usimshangae Lipumba, hapo anajaribu kurudisha umaarufu wake ulioporomoka.
 
Greenwhich Hapo kwenye nyekundu kafiri=asiye muislamu mf: mkristo
- kwahiyo mwandishi anataka kutuambia vitendo hivyo hufanywa na wakristo, wapagani na dini nyingine ndogondogo na si waislamu; kama tulivyo zoea dunia nzima.. Ktk hili mwandishi kaonyesha udhaifu mkubwa.

Mkuu huelewi maana ya neno Kafiri.Kafiri haina maana ni mkristo tu.Muislam gaidi na muovu naye ni Kafiri.Muislam anayeiba mikate kanisani huyo ni Kafiri tu.Muislam anayeiba pombe na kwenda kunywa huyo ni Kafiri tu.

Mwandishi kakosea nini kusema wapuuzi waliofanya ushenzi huu ni makafiri?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom