Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Msalala: Nitasimamia maendeleo ya kiuchumi nchini

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
IMG_20200928_151755_123.jpg
IMG_20200928_151831_231.jpg

PROF. LIPUMBA AKISALIMIA WANANCHI WA MSALALA KATIKA STENDI YA KAKOLA AKIELEKEA KAHAMA

NITASIMAMIA MAENDELEO YA KIUCHUMI NCHINI "PROF.LIPUMBA"

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itajenga uchumi wa kisasa wenye ushindani wa kitaifa na kimataifa na utakaohimili misukosuko ya utandawazi, unaokuwa kwa kasi bila kuharibu mazingira, na ambao utakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Kukua kwa uchumi kunahitaji uongozi imara na utawala makini, mikakati na mipango mizuri ya maendeleo na utekelezaji mzuri wa mikakati na mpango hiyo. Kujenga mazingira mazuri ya kuwekeza, kufanya biashara na ushirikiano wa kimataifa bila kuathiri uhuru wa nchi yetu.

Kuweka misingi ya utawala bora na utekelezaji wa sera utakaohakikisha kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 8 – 10 kila mwaka kwa miaka kumi ijayo na kufanikisha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu mwaka 2030.
 
Aisee sasa kama hata Lipumba anapata nyomi hivi, kale kawakala ka beberu Amsterdam mbona kana jifariji kushinda?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom