Prof. Kitila Mkumbo: Watanzania hawapingi uwekezaji wa Bandari, wanataka Mikataba iwe Mizuri

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Chama cha Mapinduzi (CCM) kilibadili mwelekeo wa kisera za kiuchumi na kisiasa miaka ya 90's, mojawapo ya mabadiliko ya kisera za kiuchumi na kibiashara ni kuachana na Serikali kuhodhi nyenzo za uchumi kama ilivyokuwa hapo kabla"- Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Miaka ya 90's Chama cha Mapinduzi (CCM) ilitoa maana ya ubinafsishaji hauna maana ya serikali kukabidhi mali za umma kwa watu binafsi au watu.
Ubinafsishaji maana yake ni :-
1. Kuuza baadhi ya hisa za kampuni ya umma kwa wawekezaji binafsi
2. Kuingia ubia na makampuni au watu binafsi wa ndani au nje ya nchi
3. Kukodisha kampuni ya umma kwa watu binafsi au watu binafsi" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kamwe asingeweza kuruhusu kuingiza azimio humu bungeni ili kuuza bandari lakini wabunge wote hawa wasingeweza kupokea azimio la namna hiyo" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Baada ya taarifa za uwepo wa mkataba wa uendelezaji wa bandari wananchi wengi waliingia hofu, na sisi kama wabunge ni lazima tuzipokee hofu hizo, kuzielewa na kuzishughulikia hisia na hofu za wananchi wetu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Azimio lililopo bungeni halihusu kuuza bandari, azimio linahusu uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari. Chama cha Mapinduzi (CCM) kisingeruhusu serikali yake kuingiza bungeni azimio la kuuza bandari" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Katika uwekezaji wowote kunakuwa na hofu, hata wakati wa kubinafsisha NBC kulikuwa na hofu na wapo walisema NBC imeuzwa. Mwaka 2005/2006 wakati nikiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tulimega eneo kwa ajili ya kujenga Mlima City, tuliambiwa chuo kikuu kimeuzwa lakini tulisimama imara sidhani kama kuna Mtanzania leo analalamika kuhusu Mlimani City" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Azimio lililopo bungeni linahusu kuanzisha mahusiano ya kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai, tukisharidhia ndio serikali inakwenda kufanya kazi yake ya kawaida ya kuingia mikataba. Hadi hapa tulipo hatuna mkataba kati ya TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania) na Kampuni ya DP World" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Kifungu cha kwanza cha mkataba kinaelezea maeneo ya uwekezaji, uwekezaji utafanyika kwa bandari ya Dar es Salaam lakini akifanya vizuri serikali inaweza kumualika aende kwenye maeneo mengine" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Wapo wanaosema mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) hauna namna ya kurekebisha, mkataba unarekebishika kwa kupitia ibara ya 22 ya mkataba huu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Eneo la mifumo ya TEHAMA ni eneo nyeti na linahusu usalama wa nchi, nashauri na kuwaomba sana watu wa TCRA na serikali mtandao lazima wawepo na wasiachiwe wawekezaji peke yao." - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Nchi yetu ni miongoni mwa nchi ambazo zimebahatika kuwa na waasisi, msingi mkubwa ambao Marekani waliachiwa na wanaulinda ni uhuru wa watu wao. Sisi tuna waasisi wawili Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume na msingi waliotuachia ni umoja na ni lazima tuulinde msingi huu. Nchi yetu ni ya kidemokrasia hivyo tukitofautiana tutofautiane kisera lakini tusivunje misingi yetu ya umoja" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Mimi natoka wilaya ya Iramba person mkoani Singida lakini ni mbunge wa jimbo la Ubungo, hilo limewezekana kutokana na umoja wa nchi hii, kuna nchi wabunge wao ni wabunge wa makabila. Na natamani watoto na wajukuu wangu mimi wawe wabunge Pemba miaka ijayo na wa kutoka Pemba waende kugombea ubunge Bukoba" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

Niwaombe wanasiasa na sisi viongozi tuepuke kauli ambazo zinagusa misingi mama (ya umoja), tutofautiane kisera" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Watanzania hawapingi uwekezaji wa bandari wanataka mikataba iwe mizuri, wataalamu mzingatie hilo ili uwekezaji katika bandari uwe na tija" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo.

FyQl8eiWcAIzqf2.jpg
 
Ni kati ya wabunge walio ingia bungeni kwa nguvu ya John.
Nauona mwisho wake ukiwa mbaya sana kisiasa, na nina uhakika haito kaa arudi tena bungeni baada ya 2025.
 
Mimi ni mtanzania na sijampa uwezo wa kuwa ni msemaji wangu, utafiti gani ameufanya kuthibitisha kuwa watanzania wengi wanaunga mkono uchafu huu?,ujinga, uoga na uzuzu ndio mtaji pekee uliobaki kwa chama dola
 
View attachment 2653008
PRESIDENTIAL MATERIAL .CCM,2030 TULETEENI MTU HUYU KWENYE UCHAGUZI
 
Back
Top Bottom