Prof. Kindiki anatoa onyo kwa Odinga dhidi ya dhidi ya maandamano yenye vurugu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,149
Kiukweli Jeshi la polisi limetumia hekima kuzuia Maandamano ya UVCCM kwani wanaokufaga huwa hawahusiani kabisa na Maandamano mfano Akwilina pale Kinondoni Magomeni

Hata Maandamano ya Kenya polisi waliishia kuwaua Wanafunzi wasio na Hatia

Mlale Unono!
---

1689635304009.png

Prof. Kindiki
Waziri wa Usalama Kithure Kindiki anasema vyombo vya usalama havitaruhusu maandamano yenye vurugu sehemu yoyote nchini.

Ameonya kuwa polisi watashughulikia waandamanaji wenye vurugu jinsi wanavyoshughulika na wahalifu wenye silaha.

Waziri huyo mwenye sauti laini alisema kila Mkenya ana uhuru wa kufanya maandamano lakini asitishie wengine usalama.

Kindiki anatoa onyo dhidi ya maandamano yenye vurugu

Kindiki aliwaonya viongozi wa upinzani kwamba uhuru wa kuungana na haki ya kudai haki haiondoi haki ya kufanya uharibifu na kuiba mali.

Waziri wa Masuala ya Ndani alisema vyombo vya usalama viko tayari kushughulikia mtu yeyote atakayekutwa akiuka sheria kwa jina la maandamano.

"Uhuru wa kuungana na haki ya kufanya maandamano/harambee haiondoi haki ya kusababisha uharibifu na kuiba mali. Jumatano, yeyote anayetishia kufanya nchi kuwa isiyoweza kusimamiwa kupitia vurugu, wizi, fujo, na umwagaji wa damu atashughulikiwa kwa nguvu na kwa uamuzi, kulingana na sheria. Tunawasiliana nawe," Kindiki alionya.

Kulingana na Kindiki, mtu yeyote anayejihusisha na vurugu atashughulikiwa kwa njia ile ile kama magaidi na majambazi.

"Watu hao wanaotishia raia wanaofuata sheria kwa vurugu, kuvuruga amani na kufunga barabara, tutakushughulikia kama tunavyoshughulikia wahalifu wengine kama majambazi, magaidi, wafanyabiashara wa dawa za kulevya na wahalifu wengine wote, wewe ni katika kundi moja. Hakuna mtu aliye juu ya sheria," alisema.
 
Unadhani Kindiki na kasauti kake ana mkwara, vitisho au ukatiri kuliko mzee Moi?

Raila amefanya Hadi uhaini enzi za utawala wa kikatili wa Moi. Kindiki anatakiwa kumwambia boss wake akae na

Raila waweke sawa mambo yao sio kwa mikwara mbuzi wanayoleta.
 
Maandamano ni Thanks ni hukumu la bavicha hapa Tanzania

USSR
 
Kiukweli Jeshi la polisi limetumia hekima kuzuia Maandamano ya UVCCM kwani wanaokufaga huwa hawahusiani kabisa na Maandamano mfano Akwilina pale Kinondoni Magomeni

Hata Maandamano ya Kenya polisi waliishia kuwaua Wanafunzi wasio na Hatia

Mlale Unono!
Ukifuta futa kote...sio huyu hapana yule ndio.
 
Unadhani Kindiki na kasauti kake ana mkwara, vitisho au ukatiri kuliko mzee Moi?
Raila amefanya Hadi uhaini enzi za utawala wa kikatili wa Moi. Kindiki anatakiwa kumwambia boss wake akae na Raila waweke sawa mambo yao sio kwa mikwara mbuzi wanayoleta.
Tusubiri Wednesday!
 
Kwa mambo ya hovyo yanayofanywa na watawala wa tanzania,inatakiwa tuondoe uoga il kupambania nchi yetu kuiokoa.maana watawala wao wanazidi kuimega tu kwa kuwauzia waarabu
 
Maandamano yanaogopwa na tawala nyingi duniani maana within a minute utawala unadondoka. Kw kenya kinachowaponza ni kwamba ruto kashindwa kula na kipofu odinga kama kenyata alivyofanya. Na ruto akicheza anaenda kuwa one term president
 
Unadhani Kindiki na kasauti kake ana mkwara, vitisho au ukatiri kuliko mzee Moi?

Raila amefanya Hadi uhaini enzi za utawala wa kikatili wa Moi. Kindiki anatakiwa kumwambia boss wake akae na

Raila waweke sawa mambo yao sio kwa mikwara mbuzi wanayoleta.
Upo sahihi hao kina kindiki, sabina chege.Rigathi pamoja na wengine wa mrengo wa kenya kwanza naona wanambwekea sana odinga .Lakini chuma kipo still . Na kinachomponza ruto hadi baba anapata political popularity ni kujibishana nae kwenye majukwaa. Hapo odinga anapata credit sana
 
Unadhani Kindiki na kasauti kake ana mkwara, vitisho au ukatiri kuliko mzee Moi?

Raila amefanya Hadi uhaini enzi za utawala wa kikatili wa Moi. Kindiki anatakiwa kumwambia boss wake akae na

Raila waweke sawa mambo yao sio kwa mikwara mbuzi wanayoleta.
Ilimsaidia nini? Umesahau Moi alichomfanyia? Amekua rais sasa?
 
Wakenya hawajaendekeza ujinga kama watanzania, wako active kwenye mambo yao wanapoamua.

Mnyukano uliotokea 2007 ndio ulileta heshima hadi wakapata katiba mpya 2010 hii pia naona ndio njia pekee ya watanzania nao kuja kuheshimiana.

Huu upumbavu wa kuona kama maandamo na makusanyiko hayaruhusiwi ndio mlikuwa mkiufurahia ile miaka 5 unusu nchi ikiwa inakabiliwa na lile jinamizi kutoka chato wakati haki ya kuandamana na kufanya makusanyiko iko kisheria kikatiba sio tu kwa katiba hii hii chakavu ya miaka 46 iliyopita jukumu la polisi ni kulinda waandamanaji ila ajabu polisi wanageuka na kuanza kukamata watu.

Katiba ya Kenya inasema hivi:

Article 37 of the Constitution 2010 gives the right to assemble, demonstrate and picket, but the participants must be peaceful and unarmed.

Ukiangalia hapo wananchi wanaruhusiwa kukusanyika na kuandamana maandamano ya amani kabisa yasiyo na fujo kwanini wazuiwe?
 
Kiukweli Jeshi la polisi limetumia hekima kuzuia Maandamano ya UVCCM kwani wanaokufaga huwa hawahusiani kabisa na Maandamano mfano Akwilina pale Kinondoni Magomeni

Hata Maandamano ya Kenya polisi waliishia kuwaua Wanafunzi wasio na Hatia

Mlale Unono!
Hautaki Demokrasia? 😂😂
 
Wakenya hawajaendekeza ujinga kama watanzania, wako active kwenye mambo yao wanapoamua.

Mnyukano uliotokea 2007 ndio ulileta heshima hadi wakapata katiba mpya 2010 hii pia naona ndio njia pekee ya watanzania nao kuja kuheshimiana.

Huu upumbavu wa kuona kama maandamo na makusanyiko hayaruhusiwi ndio mlikuwa mkiufurahia ile miaka 5 unusu nchi ikiwa inakabiliwa na lile jinamizi kutoka chato wakati haki ya kuandamana na kufanya makusanyiko iko kisheria kikatiba sio tu kwa katiba hii hii chakavu ya miaka 46 iliyopita jukumu la polisi ni kulinda waandamanaji ila ajabu polisi wanageuka na kuanza kukamata watu.

Katiba ya Kenya inasema hivi:

Article 37 of the Constitution 2010 gives the right to assemble, demonstrate and picket, but the participants must be peaceful and unarmed.

Ukiangalia hapo wananchi wanaruhusiwa kukusanyika na kuandamana maandamano ya amani kabisa yasiyo na fujo kwanini wazuiwe?
Kaandamane na mumeo kama wapenda kuandamana!!
 
Kiukweli Jeshi la polisi limetumia hekima kuzuia Maandamano ya UVCCM kwani wanaokufaga huwa hawahusiani kabisa na Maandamano mfano Akwilina pale Kinondoni Magomeni
Tunatengeneza mchongo ili tuje tuwaambie;
"...si mliona hata vijana wetu (uvccm) tuliwazuia?"
 
Back
Top Bottom