Press Tv

TEGEMEA

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
369
56
Habari wana JF.kuna tv nimeipenda sana kwa matangazo yake,ni press tv.inapatikana kweye dish satellite panam 7/10 ku-band frequencie 12562 H 26657.au tumia link hii ([www.presstv.ir]).
 
Yah ndoyo TV inayorusha habari zake bila propagandana na kuueleza ubovu na uasi wa US,UK na nchi nyingine zinazokandamiza hii dunia kwa kuimpose sera zao za ushoga,unyonyaji na sheria za kimataifa jinsi zinavyovunjwa na hao jamaa..kwa mfano siku moja nilikua naangalia documentary moja iliyokua inalushwa kuhusu kampuni ya BARRICK jinsi inavyo haribu mazingira na inavyojipatia faida kubwa uku kirejesha faida kidogo kwa nchi husika...na hiyo documentaru ilikua ni nchi za America kusini au Asai na sasa Barrick wamevamia AFRICA na nchini kwetu pia...pia hizi kampuni zinamafungamano na serikali zao ambazo huwezi kudai kodi zaidi bila nchi zao kukutishia....
 
Nani kakuambia press tv hawafanyi propaganda?kifupi ni moja ya channnel zinazojitahid kusambaza propaganda zake kwa hali na mali-na mbaya zaid inaponda kila ki2 westerners wanachofanya-hata kama wanakosea-
Itwatilie utakuja jua wakati mwingine press tv hawajui wanachozungumza
 
Ni ya Iran na si Iraq.Ukweli i kuwa inatoa habari ambazo hutazipata katika media za magharibi.Kwa mfano Bahrain kuna uprising kubwa lakini hutaona CNN wala BBC. wana waandishi dunia kote na mara nyingi alfajiri wanaendesha midahalo ya kisiasa. Lazima watakuwa na upendeleo kidogo,wewe mwenyewe akili ya kuambiwa changanya na yako.
 
hii wala sio nzuri,inaponda kila kitu cha nchi za magharibi!kuna mtangazaji ambaye ni mbunge wa uingereza(George Galloway)ndio amepelekea press tv kufungwa katika anga la uingereza,inapatikana kwenye intanet tu!
 
Mi naipenda but ningeiadmire zaid km ingekuwa na correspondent bongo kwn KJ na washkaj zke labda tungewaskia the Hague.
 
Haiwezi kuja bongo, ina correspondets nchi za kiarabu tuu, hasa zile zenye uprising.

Mi naipenda but ningeiadmire zaid km ingekuwa na correspondent bongo kwn KJ na washkaj zke labda tungewaskia the Hague.
 
Hawa hawa Wairan ndio waliowaponza wengi duniani, eti mpaka Zanzibar wanafadhili Mwamsho wa waislamu dhidi ya Tanganyika kibaraka wa Magharibi.
 
Kwanza sio kweli kwamba imefungwa ktk anga la Uingereza. Kilichofanyika ni kwamba, imeondolewa tu ktk packages za ving'amuzi vya makapuni yanayotoa service kule. Lakini bado watu wenye mapenzi nayo wanaweza kuipata free thru analogy decorders kama tunavyoipata sisi huku.

Pili, si kweli kwamba mtangazaji huyo ndiye kapelekea kuifungia. Hebu soma hapa, ili tusiendelee kupotosha umma.
 
Tatizo haitadumu

Sina hakika sana na hilo, ila ninachafahamu mimi ni kuwa imekuwepo hewani kipindi kirefu sasa. Mimi nimekuwa nayo kama FTA tangu 2007, baada ya hapo channels nyingi zimekuwa zikipotea(scrambled) kila mara lakini hii ipo tu.

Unajua hii tv haitegemei matangazo kujiendesha. Kwa kiasi kikubwa inaendeshwa na pesa inayotokana na mafuta ya Iran, so si rahisi kukwama.

Lkn jambo la pili, makampuni mengi yenye uwezo wa kuinunua yanatoka nchi za magharibi, ambazo hazifurahishwi na tv hii. Kwa mfano, kwa UK ilikuwa kwenye package ya Sky lkn baada ya kutoa habari ambayo haikuifurahisha familia ya kifalme, mara moja Sky waliambiwa kuvunja mkataba na Press tv. Kwa sasa UK ukitaka kutazama Press tv, ni lazima kununua dish na kuitazama thru fta kama tunavyofanya huku.

Lkn pia tv hizi zenye msimama na habari zake, hasa zisizobeba maslahi ya nchi za magharibi kwa mfano Aljazeera ni lazima zinakuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato. Havitegemei hisani ya pesa kutoka magharibi, na ndio maana hurusha matangazo yake bure kwa watu wote.
 
Haiwezi kuja bongo, ina correspondets nchi za kiarabu tuu, hasa zile zenye uprising.

Mimi sina hakika na hilo, ila ninachofahamu ni kuwa ina correspondets sehemu nyingi sana duniani. Nakumbuka hata ktk lile tutio la kuzama meli ya Zanzibar iliripoti. Ila siwezi kudhibitisha kama correspondent wake yupo bongo au la.

Inawezeka wewe ukaona kama ni televisheni ya middle east tu, lakini pengine labda wewe si mpenzi wa tv hii, kwa maana kwamba pengine mara moja moja unapoitazama unakuta kipindi cha Middle East Toaday au unakuta documentary inayohusu Gaza.

Kiujumla watu wengi wanaopenda kutazama tv za habari za kimataifa, mara nyingi wataitaja Press TV kama miongoni wa channels nzuri.
 
Back
Top Bottom