President Paul Kagame responds to Jakaya Kikwete on FDRL comments 'utter nonsense'

Huu ni wakati wa watanzania kuungana na kuwa wamoja kwa sababu majirani zetu wanatumia tofauti zetu kutuvuruga.Vita mbaya sana.wenzetu walipotofautiana walikimbilia Tanzania na kwa sababu ya ukalimu wetu tuliwakaribisha. Lakini ninyi sijui mtakimbilia wapi kwa sababu majirani zenu hawawapendi sana. Mtapata shida sana. Dumisheni umoja uliopo.Jenga nchi.
 
..teh teh najua hammaanishi mlichoandika au hamkushirikisha ubongo vizuri, usizungumzie uganda na mamluki,hawa jamaa wako vizuri tutake tusitake,muulize mfaransa nae alitunishiwa msuli na huyu dogo akasalimu amri sembuse magobore yetu yanayolipuka ovyo huko mbagala...chezeya bahutu na batutsi weye..?

Gefu,
Labda wewe uhakika hata JKT hukwenda. JWTZ ni jeshi imara sana na uimara wake unatokana na utiifu wa askari wake na kufuata amri wanazopewa. Hivi sasa Rwanda wanafikiri wana uwezo mkubwa kivita kwa vile walifanikiwa kuwatesa Wakongo lakini ni kwa vile Wakongo hawana Jeshi lenye mpangilio na kufuata orders
. Sababu kubwa za ubavu wetu ni hizi zifuatazo:

  1. Rwanda inatawaliwa kidikteta kwa hiyo raia walio wengi hawaipendi serikali ya Kagame na labda baadhi ya raia na wanajeshi wapo kwa sababu ya hofu tu.
  2. Sio ajabu sehemu kubwa ya Jeshi la Kagame likasambaratika kama wakiona wanalipuliwa kama ilivyokuwa kwa jeshi la Amini, maana tayari makamanda wake wakuu wameshaanza kumkimbia k.m. Gen. Kayumba Nyamwasa aliyekimbilia SA.
  3. Majemadari wakuu wa Jeshi la Rwanda wengi walijifunzia kwetu wakati wa vita ya Uganda. Kwa hiyo nyingi ya mbinu zao ni zile tulizowafundisha.
  4. Tanzania inapigana kwa niaba ya jumuiya ya kimataifa, kwa hiyo upuuzi wowote wa Kagame utamfanya abanwe zaidi.
  5. Lakini kubwa zaidi ni ubora wa jeshi letu, kinidhamu na kiutaalamu. Ingawa hatujapigana kwa muda mrefu, uzoefu na mafanikio tulioupata Uganda, Mozambique, Seychelles na Comoro utatusaidia sana.
Watanzania tunatakiwa kuondoa tofauti zetu kisiasa na kumuunga mkono Kikwete, kwani jeshi letu halipigani kwa niaba ya chama chochote bali kwa niaba na usalama wa taifa letu lote.

VIDEO: Kagame arushiwa mayai, mawe, chupa na mavi huko London

Last edited by a moderator:
Kama una wasiwasi na uimara wa JWTZ pata fursa unuse pale Monduli au Ngerengere na kwavile wengi mmekariri hizi kambi mbili maarufu sasa hivi Command ya JWTZ ipo level nyingine na ndio tulichobaki kujivunia Kusini mwa jangwa la sahara!
JWTZ ina uwezo wa kupigana na nchi zote zilizotuzunguka kwa mpigo na tukashinda!
Hutaki unaacha!!!
 
ee kwa kuwa ustaarabu huanzia nyumbani MWANADIPLOMASIA HUYU WA TZ ANGEANZIA MTWARA,ARUSHA MJINI,IRINGA MJINI,MOROGORO na kwenye kesi ya madakktari na hata waalimu wa shule za serikali ,ambapo kupingwa tu kumemwaga damu na wamwagaji wamepandishwa vyeo wamepelekwa hqtrs wangojelee pesa ya kustaafu.Anaayeua mamilioni KONGO ILI AIBE MADINI NAna anayeua watu 10 TZ eti kuudhaifisha upinzani wote ni wauaji.Hivi mzee RAISI tukiandamana JIJI LOOTE LA ARUSHA FANYA FUJO UONE WATATUCHINJA KWA RISASI AMA UTAKUJA TUZUNGUMZE KIDIPLOMASIA?
 
Hakuna cha ushauri, wakati tumeshindwa kukaa na wanaMtwara meza moja kutatua tatizo la Gass. Viva Kagame
wewe ni lazima uwe MTUTSI NDIO MAANA KUMUUA MHUTU SIYO ISSUE KWAKO. TUNAKUAMBIENI NYIE WATU 15 KAENI NA WALE 85 ILI MKUBALIANE MTAISHIJE, NYIE MNAZUNGUMZA HABARI YA MAKABURI.UJINGA WENU NDIO ULIOWAFIKISHA KWENYE MAKABURI HASA KIBURI NA DHARAU ZA WAHIMA NDO CHANZO CHA YOTE HAYA. NAKUMBUKA NILIWAHI KUKAA NA BWANA MMOJA AMBAYE ALIFANYA KAZI KAMA AFISA MIFUGO (W) -TABORA SIKU 1 AKAWA ANATAKA KUNISAMILIA KWA MKONO WA KUSHOTO IKABIDI NIMPE MKONO WA KUSHOTO. HII NI DHARAU WALIYOZOEA KUWAFANYIA WAHUTU. ACHENI HAYO MAMBO YA UHIMA HAYAPELEKI MBINGUNI MORE OR LESS YATAWAPELEKA JEHANAMU
 
TANZANIA IN ITS ENTIRETY DONOT DEPEND ON RWANDESE ECONOMIC SUPPORT AND IS NOT inter-dependent economically WITH IT, MORELESS THE LATER CANNOT SURVIVE WITHOUT SUCKINGBOOD FROM THE DONOR(TZ). THIS IS SUPPORTED BY BY MANY ILLEGAL ENTRY INTO TANZANIA SOIL AS REBELS , GANSTERS, REFUGEES AND LOOTERS OF TANZANIA NATURAL RESOURCES . I DONT THINK THE RWANDESE HAS THE AUDACITY TO PLAY DOWN THE ADVICE ADVOCATED BY OUR PRESIDENT. LET THEM TAKE THIS AS A PIECE OF WISDOM. YOU PEOPLE IN RWANDA NONE OF YOU IS FREE FROM BLOODLETTING DURING THE GENOCIDE AND KAGAME WAS THE FORERUNNERS AND QUICK SEIZE POWER WHEN THE LAND BECAME RAMPAGED BY 3 MONTH CIVIL STRIFE
 
wewe ni lazima uwe MTUTSI NDIO MAANA KUMUUA MHUTU SIYO ISSUE KWAKO. TUNAKUAMBIENI NYIE WATU 15 KAENI NA WALE 85 ILI MKUBALIANE MTAISHIJE, NYIE MNAZUNGUMZA HABARI YA MAKABURI.UJINGA WENU NDIO ULIOWAFIKISHA KWENYE MAKABURI HASA KIBURI NA DHARAU ZA WAHIMA NDO CHANZO CHA YOTE HAYA. NAKUMBUKA NILIWAHI KUKAA NA BWANA MMOJA AMBAYE ALIFANYA KAZI KAMA AFISA MIFUGO (W) -TABORA SIKU 1 AKAWA ANATAKA KUNISAMILIA KWA MKONO WA KUSHOTO IKABIDI NIMPE MKONO WA KUSHOTO. HII NI DHARAU WALIYOZOEA KUWAFANYIA WAHUTU. ACHENI HAYO MAMBO YA UHIMA HAYAPELEKI MBINGUNI MORE OR LESS YATAWAPELEKA JEHANAMU
Why are you shouting?
 
Waswahili wanasema mtt akililia wembe mpe unashabikia vita wakati hata yale ya Gongolamboto hukuwawi kuyaona hv vita unaijua au unaisikia ww?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Pamoja na tofauti zangu juu ya CCM na Rais Kikwete kwa ujumla; kwa hili, napingana na kile Kagame alichokisema. Lugha iliyotumiwa na Kagame sio ya kidplomasia na inaonyesha dhahiri dharau zake zidi ya Rais Kikwete.

Lakini kama kweli anataka amani ya kudumu basi ana budi kufuata huo ushauri. Tumeona leo kule Afghanistan, Marekani wanatafuta njia ya kuwashirikisha Taliban katika serikali. Kagame inabidi afike sehemu, akubali kwenda mbele na kutafuta muafaka wa kudumu.
Je ungeweza kuwaambia wayahudi wafanye mazungumuzo na Hitler leo kama angekuwa hai?
 
kazi kweli kweli,duuh hadi naogopa sasa aiseeee people like Kagame au Museveni waje kututawala ni heri nikae nyikani na hayawani au kufa tu.
 
SASA ni dhahiri kuwa kuna mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda kwa mujibu wa maoni aliyotoa Rais wa Rwanda, Paul Kagame juu ya mapendekezo ya jinsi ya kumaliza mapigano ya vikundi vya waasi wa Rwanda ya Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza katika mahafali ya Chuo cha Kijeshi cha Rwanda hivi karibuni, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya nchi hiyo akisema kwamba “ni upuuzi kutaka serikali yake izungumze na waasi wa kundi la Democratic Forces for The Liberation of Rwanda (FDLR).”

Ingawa hakutaja jina la serikali au mtu aliyemtaka kufanya hivyo, inajulikana kwamba wazo la kutaka Kagame azungumzee na waasi hao lilitoka kwa Rais Kikwete wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika Addid Ababa, Ethiopia mwezi uliopita.

“Kwa kweli kututaka sisi tuzungumze na waasi ni upuuzi mtupu. Wote wanaotaka tuzungumze na waasi hawafahamu historia ya Rwanda. Watuache tumalize matatizo yetu ya sasa kama walivyotuacha wakati mauaji ya kimbari yakiendelea,” alisema Kagame ambaye ameelezwa na gazeti la Times of Rwanda kuwa alionyesha kuwa na hasira.

Kagame alisema tangu maoni hayo yaanze kutangazwa (ya upatanishi na waasi), amekuwa kimya kwa muda mrefu bila ya kueleza kitu lakini sasa ameamua kuweka hisia zake hadharani.

Magazeti ya Rwanda yamedai kwamba Kagame alikuwa na maana iliyojificha kwa kusema aliyoyasema wakati akizungumza na wanajeshi wake na si kwenye mikutano ya kawaida ya kiraia.

Inafahamika kwamba Kikwete alitoa maoni hayo kwenye mkutano huo kwa Kagame, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambao nao pia wana waasi kwenye nchi zao.

Tayari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ametoa kauli bungeni wiki mbili zilizopita, akisema serikali haitaomba radhi kwa Rwanda au yeyote iliyompa ushauri wenye lengo la kutafuta amani.

“Serikali ilikwishatoa kauli bungeni (Kagame akutane na FDLR kuondoa tofauti zao), hilo ndilo jibu la kudumu kwa yaliyojitokeza, yanayojitokeza na yatakayojitokeza,” alijibu Membe alipoulizwa kuhusu maelezo hayo ya hivi karibuni ya Kagame.

Kwa takribani wiki tatu sasa, suala la mazungumzo hayo na waasi limetawala katika duru za kidiplomasia, huku serikali ya Rwanda ikionyesha kuchukizwa na hatua hiyo ya Kikwete.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushwakiwabo, ameandika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo twitter wiki mbili zilizopita, na akasisitiza kwamba Tanzania imekosea kwa kutaka nchi yake izungumze na waasi.

Serikali ya Rwanda inalichukulia kundi hilo la FDLR kama wakosaji wakuu kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994; hasa kutokana na ukweli kwamba kiongozi wa kundi hilo kwa sasa, Sylvester Mudacumura, ni miongoni mwa watu wanaotafutwa kwa ugaidi huku kiasi cha dola milioni tano za Marekani kikiahidiwa kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwake.

Mahusiano haya mabaya kati ya Tanzania na Rwanda yanatajwa kuanza kutia shaka kazi ya Jeshi la Kimataifa la Kulinda Amani la Umoja wa Afrika (UNAMID) lililopelekwa nchini DRC na Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zilizochangia askari.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, alisema suala la mgogoro baina ya Tanzania na Rwanda linakuzwa tu pasipo sababu.

“Mimi nimesoma hotuba ya Rais Kagame kwenye vyombo mbalimbali na kwa kweli sijaona sehemu yoyote ambayo ameitaja Tanzania au Rais Kikwete kwa namna yoyote ile. Ni vyombo vya habari ndivyo ambavyo vimeweka hayo majina lakini hayapo kwenye hotuba mnayosema,” alisema.

Wachambuzi wanaona kwamba kazi kubwa ya UNAMID itakuwa ni kupambana na waasi wa kundi la M23 ambalo linadaiwa kuungwa mkono na serikali ya Rwanda.

Kuna dalili kwamba badala ya UNAMID kulinda amani, inaweza kutumika kuwa uwanja wa vita baina ya Tanzania na Rwanda nchini DRC.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa, aliliambia Raia Mwema jana kwamba kamati yake haiwezi kutoa ushauri wowote kwa serikali kwenye suala la Rwanda kwa vile inaamini inaweza kulimaliza.

“Kwa sasa kamati haiwezi kutoa maoni yoyote kuhusu uhusiano wa Tanzania na Rwanda.

“Serikali tayari imetoa maelezo yake na kama inataka maoni yetu inakaribishwa. Ila hatuwezi kuzungumza kuhusu hili suala kwa vile ni la serikali,” alisema.

Tanzania na Rwanda hazijawahi kuwa na mgogoro wowote wa kijeshi au kidiplomasia tangu nchi hizo zipate Uhuru kwenye miaka ya 1960 na mgogoro ni jaribio kuu la kwanza kwenye mahusiano baina ya nchi hizi.

Na maelfu kwa maelfu ya raia wa Rwanda wa sasa na waliopita wamepata kuishi Tanzania, wengine wakiaamua kuifanya Tanzania nchi yao ya kuishi.

- See more at: Raia Mwema - Kagame akoleza hasira
 
Pamoja na tofauti zangu juu ya CCM na Rais Kikwete kwa ujumla; kwa hili, napingana na kile Kagame alichokisema. Lugha iliyotumiwa na Kagame sio ya kidplomasia na inaonyesha dhahiri dharau zake zidi ya Rais Kikwete.

Lakini kama kweli anataka amani ya kudumu basi ana budi kufuata huo ushauri. Tumeona leo kule Afghanistan, Marekani wanatafuta njia ya kuwashirikisha Taliban katika serikali. Kagame inabidi afike sehemu, akubali kwenda mbele na kutafuta muafaka wa kudumu.

Wewe unaongea tu manake siku utakapokutwa na genocide kama Kagame ndio utaelewa mziki wake
 
Ndugu yangu mimi niko huru simtetei JK wala Kagame..! Hawa ni watu wazima tena viongozi wakuu!
Kikwete kakosea mambo makubwa kama haya alitakiwa ayaongee pembeni na Kagame kwanza badala ya kukurupuka! Mbona mwalimu alikuwa anawaita kina Buyoya kwanza!? Hivi yeye Kagame angesema amrudishie ushindi wake Dr Slaa inaosemeka JK alimhujumu JK angesemaje?

Kama kujuana nadhani wanajuana sana na ninaamini Kagame anamjua JK zaidi...kwasababu viongozi wetu wengi tu wabunge na madiwani na maafisa wengine wameisha enda Rwanda mara nyingi kwa kile wanachodai eti kwenda kujifunza namna Rwanda ilivyofanya hadi ikapata maendeleo!! SUMATRA walinda kule wakaa sana tena kifisadi eti wanajifunza jinsi ya kuiga utaratibu mzuri wa kuendesha bodaboda!!! Kagame tena kwa kuwatia aibu baadhi ya wabunge alikataa kuonana nao akasema yeye kila kitu amechukua Tannzania sisi tunahangaika nini?

Kama ni damu, jiulize JK alishasema pole yeyote kwa familia ya Mwangosi? kwanini kampandisha cheo alie muua mwangosi! Waliomtesa Dr Ulimboka JK hawajui? walio mfanya vibaya Kibanda JK kweli hawafahamu?? mbona mtoto wake amehisishwa na watekaji hao nahajakanusha??
Yaani maovu ya kagame yatuume kuliko ya huyu wa kwetu?

Sawa JK ni raisi wetu, ila kachemka!!

Ndugu yangu Mzizi wa Mbuyu, naona hamasa yako ni kubwa sana, ila ninachoshangaa kwako, ni kutooanisha hotuba ya JK na mazingira aliyosemea, ukiisoma hotuba hiyo unaona kuna kipengele cha kuleta hamasa uliyonayo kumkosoa JK? Labda unajua mengi. Slaa na Mwangosi sijaona sehemu anayopata kwenye huo mkutano wa Mazungumzo ya Amani katika Maziwa Makuu, ulioitishwa kwa nia ya kupata ufumbuzi wa kudumu DRC. Jamani kama unampenda sana Slaa, si jambo baya subiri umpigie kampeni (zenye busara na ustaarabu) achukue nchi, lakini kama unadhani unawezaa kuchangia amani ya maziwa makuu, naona ndugu yangu hapo mmhhh!!!.

Historia ya Rwanda na Kagame inapenda sana kujirudia, wale wanaotakiwa kukaa meza moja na kuzungumza amani na Serikali ya Kagame, ni Wahutu na yeye ni Mtusi (very Royal), nadhani kuna mambo huyasomi vema. Matusi makali ya Kagame yasingetokana na Hotuba ya JK kama inavyoonekana pale. Je kuna ujinga wa Historia pale kuomba wanaogombana kuelewana. Tena kama kuna waliosemwa vibaya ni wale waasi maana akasema "the FDLR and the ADF who should also be engaged and find a peaceful way of making them stop their negative activities against their countries of origin" pale nilipopigilia msitari umepaelewa vema? Nadhani tukubali hamasa ya hasira ya Kagame haitokani na JK alisema nini bali """NIKAE NA WAHUTU????""""

ALAMSIKI
 
Kama una wasiwasi na uimara wa JWTZ pata fursa unuse pale Monduli au Ngerengere na kwavile wengi mmekariri hizi kambi mbili maarufu sasa hivi Command ya JWTZ ipo level nyingine na ndio tulichobaki kujivunia Kusini mwa jangwa la sahara!
JWTZ ina uwezo wa kupigana na nchi zote zilizotuzunguka kwa mpigo na tukashinda!
Hutaki unaacha!!!
Hivi toka jwtz waende Congo bado m23 wanawaua wacongo?naomba unijuze ndugu yangu
 
Ndugu yangu Mzizi wa Mbuyu, naona hamasa yako ni kubwa sana, ila ninachoshangaa kwako, ni kutooanisha hotuba ya JK na mazingira aliyosemea, ukiisoma hotuba hiyo unaona kuna kipengele cha kuleta hamasa uliyonayo kumkosoa JK? Labda unajua mengi. Slaa na Mwangosi sijaona sehemu anayopata kwenye huo mkutano wa Mazungumzo ya Amani katika Maziwa Makuu, ulioitishwa kwa nia ya kupata ufumbuzi wa kudumu DRC. Jamani kama unampenda sana Slaa, si jambo baya subiri umpigie kampeni (zenye busara na ustaarabu) achukue nchi, lakini kama unadhani unawezaa kuchangia amani ya maziwa makuu, naona ndugu yangu hapo mmhhh!!!.

Historia ya Rwanda na Kagame inapenda sana kujirudia, wale wanaotakiwa kukaa meza moja na kuzungumza amani na Serikali ya Kagame, ni Wahutu na yeye ni Mtusi (very Royal), nadhani kuna mambo huyasomi vema. Matusi makali ya Kagame yasingetokana na Hotuba ya JK kama inavyoonekana pale. Je kuna ujinga wa Historia pale kuomba wanaogombana kuelewana. Tena kama kuna waliosemwa vibaya ni wale waasi maana akasema "the FDLR and the ADF who should also be engaged and find a peaceful way of making them stop their negative activities against their countries of origin" pale nilipopigilia msitari umepaelewa vema? Nadhani tukubali hamasa ya hasira ya Kagame haitokani na JK alisema nini bali """NIKAE NA WAHUTU????""""

ALAMSIKI

Bado huja gusa kitu baba!!
Kama Kagame anasema nikae na WAHUTU!!
JK kipenzi chako ni mara ngapi anaambiwa aunde chombo huru cha kuchunguza matukio ya kishetani yanayitokea nchini...HATAKI!!
JK hana sifa za kuwaweka watu meza moja eti waelewane, kwakuwa nayeye anayalea mambo ya ovyo yanayoashiria tatizo kubwa tu mbele lisipodhibitiwa kama la Rwanda tu..( Kiongozi wako akiendelea kuchekea mambo muhimu)
 
Kagame's grief over FDLR, is more on the fear of the revenge. He understand very well that, after the Tutsi under Kagame, had killed Habyarimana, the Hutu's revenge was to kill the Tutsi (cockroaches) wherever they were.
In fact, hata wasipolipa kisasi, bado FDLR ni threat kubwa kwa Kagame na ndio maana hataki kufanya nao mazungumzo!! Kwamba hawezi kufanya nao mazungumzo kwa kigezo kwamba FDLR wamekuwa named as Terrorist Group ni bla blah zake tu kwani hata hao anaowafuata (U.S) tayari wameshagundua kwamba GUN can never bring peace na sasa wameamua kukaa meza moja na TALBAN, wale wale magaidi wakubwa ambao US ilisema isingeweza kukaa nao meza meja ku-negotiate na terrorists!!

Hofu kubwa ya Kagame ni kwamba ingawaje Ukabila wa wazi wazi umepungua sana ndani ya Rwanda lakini ukabila wa siri siri bado upo!! Kufanya mazungumzo na FDLR ni sawa na kuikaribisha FDLR kwenye ulingo wa kisisasa za Rwanda! Hili kamwe Kagame hawezi kulikubali kutokana na ukweli kwamba Watutsi (kabila la Kagame) ndani ya Rwanda ni abut 20% wakati Wahutu (ambao ndio FDLR) ni 80%!! So, ingawaje ukabila wa wazi umepungua kwa kiasi kikubwa lakini ukabila wa chini chini bado upo! So, kwa kuwa kufanya mazungumzo na FDLR ni kuikaribisha kwenye ulingo wa kisiasa manake ni kwamba RPF iwe tayari kukabiliana na FDLR kwenye sanduku la kura! Na kama nilivyosema, ukabila wa siri siri bado upo na kwa kuwa sanduku la kura nalo ni siri, it's obvious endapo kutakuwa na uchaguzi, Wahutu wengi wanaweza kuwachagua Wahutu wenzao wa FDLR! Hili ndilo linalomtisha zaidi Kagame! Ikiwa Tanzania tu wapo wapumbavu wanaopiga kura kwa kuangalia kabila, seuze Rwanda!!
 
Back
Top Bottom