Prescion air mnatuaibisha!!!!!!!

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Tarehe 28/04/2012, ni siku ambayo sintoisahau kwa jinsi nilivyoteswa na kampuni ya usafiri wa anga ya Prescion air. Nilifika uwanja wa ndege wa Mombasa saa nne asubuhi, tayari kwa kuruka na ndege hiyo saa sita mchana kurudi Dar. Baada tu ya kucheck-inn, tukaambiwa kuwa ndege hiyo itachelewa kwa masaa mawili, hivyo itaondoka saa nane. Hatukua na jinsi zaidi ya kusubiri tu.

Ilipofika saa nane kasoro robo tukaambiwa kuwa muda umesogezwa tena hadi saa kumi, na ilipofika saa kumi jioni wakatuambia kuwa kutokana na sababu zisozozuilika hakutakuwa na ndege tena kwa siku hiyo toka Mombasa kwenda Dar, na kuwa itabidi tulale Mombasa ili tuondoke kesho yake alfajiri na KQ kupitia Nairobi.

Baada ya tangazo hilo ilibidi abiria tuwe wakali na baada ya muda wa karibu saa moja tukaambiwa kuwa tutapata usafiri wa KQ ifikapo saa mbili usiku hadi Nairobi na hapo tutapata usafiri wa Prescion air ya saa sita usiku.

Kwa kuwa tulishachoka na watu tulikuwa tunataka kufika Dar, ikabidi tuchukue uamuzi huo na tukaondoka na ndege ya KQ saa mbili na nusu usiku na kufika Nairobi saa tatu usiku na hapo tukakaa hadi hiyo saa sita dk 45 usiku ndio tukapata Prescion air kidege kidogo cha watu 60, na tukatua JKIA Dar saa tisa kasoro usiku.

Jamani hii ndio kampuni yetu, inasikitisha saana na hivi najiandaa niende kuonana na CEO wake.
 
Ona thread yangu hapo chini! shirika limeoza! ahsante victim ni wengi wa huu ujinga wao!
 
wakishapata mshindani watatia adabu
suluhisho ni kupigania air tanzania izaliwe upya,bodi mpya,uongozi mpya ndege mpya
 
Back
Top Bottom