Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma

willium,
umewahi kufika kwa wananchi masikini wa dodoma?
Mfano mpwapwa miaka ya nyuma? Pale chuo cha ualimu?
Nilipofika pale nilitokwa machozi ( ilikuwa nyuma kidogo mwaka 2003 au 2004)
unajua kuwa walikuwa wanaomba ugali wa wanachuo?
Na hata ukitupwa walikuwz wakiuokota?
Unajua walikuwa wakijitolea kukaanga kitimoto bure ili wapate mafuta?
Hivi unajua maisha ya mtanzania aliyepo kijijini wewe?

Unajua kuna watu wanaishi kwa pusi moja ya pombe?(komoni) tena ya kununuliwa? Anainywa siku 1-2 kidogo asubuhi kidogo mchana kidogo jioni? Kwa sababu hana hela ya chakula?

Unajua kuna watu hawana shilingi 100 ya kununua panadol?

Ila haishangazi wewe kutokujua hayo........
 
Tunataka umtoe yule mpuuzi wa mtera aliyechanganyikiwa (lusinde) kupitia ccm au cdm
 
suluhisho ni dogo sana kwanza hizi posho wanazopewa zipunguzwe angalau kwa 10% hii itawafanya waonje makali ya maisha hii itasaidia sana kuwakumbusha vilio vya walimu, manesi na wafanyakazi wengine wanapolia ukali wa maisha; pili mfumo wa bunge letu lazima ubadilike inachekesha na kushangaza sana kuona congress nzima ya Marekani ina wabunge kama sikosei 400 wamerekani wapo milion 350, sisi tupo watanzania milion 40 wabunge zaidi ya 300 wa nini? kila kukicha ni mkoa na wilaya mpya zinaanzishwa hii ina maana kutakuwa na ongezeko la wabunge; bajeti yetu 50% ni mikopo na misaada, kwa nini tusiwe na wabunge wachache ambao tutaweza kuwalipa vizuri? Ukweli bunge letu limegeuka kama saigon hata ule msisimko wa kibunge halina. Pale wabunge watakapoanza kuwatetea wananchi ni wazi watanzania watawaunga mkono kwenye madai yao; kwasasa hakuna atakayewaunga mkono, kuhusu rushwa hicho ni kikwazo ndani ya bunge letu nadhani ipo haja ya kuwaelemisha watanzania maradhi tunafuga wenyewe. Pia ipo tabia ya hawa wabunge kuwalaghai wapiga kura si kazi ya mbunge kutoa pesa zake mfukoni kujenga zahanati au kununua madawati, wanatumia ufinyu wa mawazo walionao watanzania hasa wa vijijini, kazi ya mbunge ukiachia kutunga sheria ni kuibana serikali ipeleke maendeleo kwenye sehemu, mbunge anapaswa kutoa changamoto kwa wananchi wenyewe kuleta maendeleo kwenye maeneo yao, hili la kuwadanganya wananchi mfano mh. Selasini nimesoma article yake kwenye blog yako ndiyo kimekuwa kikwazo kikubwa kumbuka mbinu inatumiwa na wabunge wote, ikiwa wanatoa pesa mifukoni kununua madawati hii wazi pesa tunazowalipa ni nyingi hakuna sababu ya kuwaongezea posho.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Niliwahi kuandika humu, kwa Mbunge hata posho ya 300,000 kwa siku ni ndogo sana.
 
- Ni watunga sheria hawa, so ni tofauti sana na watu wengine kwenye serikali!

William.

Kwa nini mtu anahonga na yupo tayari kuweka rehani au kuuza nyumba yake na kuchukua mikopo kwa ajili aende kutunga sheria ? Hizo hela ndio wanatumia kuwaonga wananchi na ndio maana wananchi wanawafuata Dodoma kuwalilia shida maana wakati wa uchaguzi ndio kipindi wananchi kwa mbaaali wanaweza kuona unafuu wa maisha kwa upande wao kwani watahongwa chakula na fulana na kofia.

Kwa kweli Kaka William naanza kupata taabu jinsi unavyoangalia maisha ya Watanzania wengi na wabunge wachache mno. Hakuna aliyelazimishwa kuwaongoza wananchi zaidi ya wao kulazimisha kuwepo madarakani hata kama hawana uwezo na hata pale wanapokuwa hawatakiwi. Badili mtazamo kidogo maana mabadiliko yapo inevitable..
 
A fact, a fact indeed!!!!!

William is isolated from reality, to him, so it seems, life is Dodoma hotel and the parliament building, Muungano, Kuu street etc where the big boys play.

Life is at ving'hwawe, farkwa, kalinzi etc. Go there, see them, hear them, eat with them, work with them, sweat with them, cry with them, bleed with them. Thereafter come and post something about sitting allowance for MPs

BADILI[B said:
[/B] TABIA;3924715]willium,
umewahi kufika kwa wananchi masikini wa dodoma?
Mfano mpwapwa miaka ya nyuma? Pale chuo cha ualimu?
Nilipofika pale nilitokwa machozi ( ilikuwa nyuma kidogo mwaka 2003 au 2004)
unajua kuwa walikuwa wanaomba ugali wa wanachuo?
Na hata ukitupwa walikuwz wakiuokota?
Unajua walikuwa wakijitolea kukaanga kitimoto bure ili wapate mafuta?
Hivi unajua maisha ya mtanzania aliyepo kijijini wewe?

Unajua kuna watu wanaishi kwa pusi moja ya pombe?(komoni) tena ya kununuliwa? Anainywa siku 1-2 kidogo asubuhi kidogo mchana kidogo jioni? Kwa sababu hana hela ya chakula?

Unajua kuna watu hawana shilingi 100 ya kununua panadol?

Ila haishangazi wewe kutokujua hayo........
 
ni kweli tofauti.....maana hawa wanapiga makofi kila siku ilhali....

Mwalimu huko tandahimba kijijini anaishi kwa hofu ya simba mshahara 430,000 gross
mtumishi wa serikali anayehakikisha shughuli zinaenda ipasavyo sh 410,000
polisi anayehatarisha maisha mshahara wake aibu hata kuutaja...
Mahakimu
madaktari


halafu unasema hawahitaji posho? Mazingira magumu wanayofanya kazi unayajua wewe? Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaaa

ila ni kweli kazi yao ni tofauti .......maana hata wanavyohatarisha maisha wacha wahatarishe.....hawana 'umuhimu' kwa taifa


Kwa style hii haistaajabishi ccm inapoteza mvuto kila siku... Mmejaa matabaka vichwani mwenu.... Kuna watu muhimu na wasio muhimu...kuna ambao pamoja na kufanya kazi hatarishi au kuishi mazingira hatarishi hamuwazi kuwapz posho ya mazingira magumu, mnawaza kujiongezea posho....ubinafsi ndio utawaangamiza......

Na sitashangaa hali hii kwenda mpaka majimboni....... Hawawawazii wananchi na shida zao, bali waona matumbo yao..........

Wabunge wa ccm wasipobadlili tabia 2015 wataingia 100 tu bungeni...

Hawaoni hali halisi.....
Hawaoni wananchi walivyowachoka.....

- Kwamba hawahitaji posho hapana ila mimi nimeongelea Wabunge na wewe unaweza kufungua thread ya waalimu na wengine, mimi nimesema niliyoyaona Dodoma!

- Ninasema hivi hoja ya posho za wabunge ijadilike sasa kuliko later, maana itaendelea kulitafuna taifa, tunawaweka wabunge wetu open for Rushwa, hasara yake ni kubwa sana kuliko kuwapa posho zaidi au kuwatengenezea mazingara bora ya kuishi kule Dodoma wakiwa bungeni, nashangaa sana kwamba hata wao miaka yote iliyopita kutokudai hili la mazingara bora ya kuishi Dodoma toka taifa!

William.
 
kaka kwa wabunge wa kibongo kuwaweka kwenye hostel watakubali?
wataimport sangap?
HAWATAKUBALI.

afu maisha magumu ni kwa kila mtu ata uk0o uchochoron tunapokaaga sie ni hatar pia kwa maisha yetu si wabunge peke yao so km wabunge wakiongezewa posho bas ata wafanyakazi wanaoenda uko kwa bunge waongezewe posho as well...

km ni kufuatwa dodoma na wananchi wao ni kwa sababu awaendi majimbon mwao....afu io sio factor kwa wao kuongezewa pesa...
 
mimi naona suluhisho sio kuongeza posho, kama ambavyo watu wengi ambao ni wa kundi lamafisadi wamekuwa wakijaribu kutushawishi kuwa tatizo ni uchache wa pesa. Na hii inatokana na wawakilishi wetu wengi kuwa ni wawakilishi maslahi au wamewekwa na chama kwa ajili ya kulinda masilahi ya chama na wao wenyewe, kwa hiyo kwao wananchi ni ngazi tu ya kufanikisha mambo yao. Suluhisho la matatizo mengi yanayohusisha pesa ni TUME YA BEI. Kwa kuwa na hiyo bei za vitu vingi vitakuwa standardized na pesa itakuwa na thamani, na hata hiyo posho siyo tu kuwa itatosha bali pia kutakuwa na haja ya kuipunguza.
 
Unahitaji kuwa na ngozi ngumu kama kiboko kutetea posho ya 200,00 kwa wabunge kwenye nchi ya kipato cha chini ya dola!!

Ndio na mimi nilichokiona hapa. Hivi katika nchi ambayo karibu 33% ni maskini wa kutupwa unapataje ujasiri wa kupandisha posho za wabunge kwa karibu asilimia 150? huku uki'ignore' makundi mengine. Ukiangalia hoja anazoziweka bwana Malecela kwamba 'hawa ni watunga sheria' utaona hazina mashiko kabisa. Kinachotakiwa ku'determine' nani alipwe nini na nani alipwe kipi kwanza kabisa ni UCHUMI wa nchi nzima!. Sasa kama tunalia uchumi ni mbovu tunapata wapi Ujasiri wa kusema wabunge waongezewe posho?. Hapa ni ubinafsi tu!
Hoja kwamba mbona Wachina wanawalipa vizuri wabunge wao nayo inatia shaka. Kwanza, Malecela angetuambia 'rates' na 'differences' za mishahara na posho za wafanyakazi wa huko Uchina ili tuone hilo 'gap'. Na kama analinganisha 'posho' za wabunge na Tz na wale Wachina asingepaswa kwenda umbali huo angeenda tu hapo jirani Kenya ambako wabunge wanalipwa vizuri kuliko Tz. Lakini pia angepaswa kuangalia Chumi za hizi nchi mbili.Huwezi kuwa na uchumi usiojisimamia kama wetu afu ukawa unalipa wabunge posho kwa kuangalia nchi za wenzio!
Mwisho, what goes around comes around!. Kama wabunge waliwapa wananchi pesa, tshirts, chumvi, sabuni n.k, wakati ule wa kampeni na wakaahidi kwamba wakichaguliwa wao wenyewe watazigeuza sehemu zao kuwa 'paradiso', kwa nini walalamike sasa wananchi kuwafuata huko Dodoma kufuatilia mahitaji yao kama walivyokuwa wanapewa wakt wa kampeni? Ni haki yao kwa sababu walizoeshwa!.
Bado sijaona hoja ya kuhalalisha hizi posho, wabunge hawa wajipange upya!
 
- Watunga sheria ni muhimu sana kuliko wengine wote kwenye taifa, ndio maana China inasonga mbele kwa sababu wanalijua hilo na wanlijali sana kuliko yote, wanahakikisha wabunge wao hawapo kwenye mazingara ya kwua wazi kwa rushwa ndio maan wakiwashika kunakuwa hakuna excuse, maana walishawatengenezea mazingara bora dawa ni Risasi tu!

- Na sisi tujifunze, hii hoja ijadilike sasa, sio lazima posho iwe laki mbili, lakini something must be done now!

William.

Hiyo haitajalisha kwa sisi Watanzania. Kwanza kwa sisi inabidi tubadili mitazamo yetu na jinsi tunavyochukulia mambo (Thinking behaviour and mentality). Kwani mawazili, makatibu wakuu na wakurugenzi wanapungukiwa nini kwenye maisha yao ? Mishahara, posho na safari lukuki zinazowapatia zinazowapatia fedha nyingi. Wengine wengi mpaka umeme wa nyumbani wanalipiwa na ofisi achilia mbali kupewa usafiri na mafuta na gharama nyingine kama mawasiliano lakini bado wataamua kuiba. Kwani hawa watunga sheria wametutungia sheria ngapi za ovyo na kijinga ?

Wake up man, the bullet train has gone while ago..
 
- Wabunge ni tofauti sana na hao wengine, WAO NI WATUNGA SHERIA! sasa mwenye kutaka sheria mbovu kwa wananchi akiwapa rushwa na kutupitishia sheria mbovu kwa taifa utasema ni sawa na wengine serikalini?


William.


Bwana William, kwanini usishauri itungwe sheria ya kudhibiti bei za hizo hotel! au kuwe na chombo cha kudhibiti bei za wenye mahotel kuliko kutaka kutuambia wambunge waongezewe posho. Alternatively, wajengewe hizo hostel. Sisi mtaani tunapandishiwa kila kitu kuanzia umeme, maji na vyakula lakini hakuna kinachofanyika kwa sie walala hoi.
 
If at all malipo ya WABUNGE ni peanuts basi huu mchuano tunaohushuhudia wa watu wa kada mbalimbali kukimbilia Bungeni usingekuwepo!
 
A fact, a fact indeed!!!!!

William is isolated from reality, to him, so it seems, life is Dodoma hotel and the parliament building, Muungano, Kuu street etc where the big boys play.

Life is at ving'hwawe, farkwa, kalinzi etc. Go there, see them, hear them, eat with them, work with them, sweat with them, cry with them, bleed with them. Thereafter come and post something about sitting allowance for MPs



more than real
william thk abt t
dnt b selfish ma broo.....et maisha magumu na ao wanaopewa elfu 45 pa day wakiwa dom?gest elfu 25-3o
aya apo aujala..sjui usafiri....EBU WAZA FRESH KAKA WILE.
 
Hiyo haitajalisha kwa sisi Watanzania. Kwanza kwa sisi inabidi tubadili mitazamo yetu na jinsi tunavyochukulia mambo (Thinking behaviour and mentality). Kwani mawazili, makatibu wakuu na wakurugenzi wanapungukiwa nini kwenye maisha yao ? Mishahara, posho na safari lukuki zinazowapatia zinazowapatia fedha nyingi. Wengine wengi mpaka umeme wa nyumbani wanalipiwa na ofisi achilia mbali kupewa usafiri na mafuta na gharama nyingine kama mawasiliano lakini bado wataamua kuiba. Kwani hawa watunga sheria wametutungia sheria ngapi za ovyo na kijinga ?

Wake up man, the bullet train has gone while ago..

- Kama hatuwezi kuwaongeza posho, then lets talk the alternative lakini Taifa we should be responsible na maisha yao wakiwa bungeni, badala ya kuwaacha ovyo ovyo tunawajengea mazingara ya rushwa na kutuletea sheria mbovu!

- People ninawasoma sana, lakini kubalini kwamba Watunga sheria ni muhimu sana kwa taifa kuliko wengine wote, hawa wana msiha yetu mikononi mwao, I undestand kwamba tumezoea maneno maneno sana, lakini hii hoja haikwepeki, kivuli cha posho na maisha ya wabunge kitaendelea kututafuna hili taiofa mpaka tutakapokubali kujadili na a compromise!

- Sawa wengine wote kwenye jamii wanahitaji kuongezwa posho, lakini priority iwe kwa wabunge kwanza watunga sheria za jamhuri!, sio lazima iwe 200,000 lakini something needs to be done!


William.
 
- Kwamba hawahitaji posho hapana ila mimi nimeongelea Wabunge na wewe unaweza kufungua thread ya waalimu na wengine, mimi nimesema niliyoyaona Dodoma!

- Ninasema hivi hoja ya posho za wabunge ijadilike sasa kuliko later, maana itaendelea kulitafuna taifa, tunawaweka wabunge wetu open for Rushwa, hasara yake ni kubwa sana kuliko kuwapa posho zaidi au kuwatengenezea mazingara bora ya kuishi kule Dodoma wakiwa bungeni, nashangaa sana kwamba hata wao miaka yote iliyopita kutokudai hili la mazingara bora ya kuishi Dodoma toka taifa!

William.

ndo maana hamjui chanzo cha umasikini ni nini......

Hebu niambie unataka posho ibadilike iwe shilingi ngapi
 
more than real
william thk abt t
dnt b selfish ma broo.....et maisha magumu na ao wanaopewa elfu 45 pa day wakiwa dom?gest elfu 25-3o
aya apo aujala..sjui usafiri....EBU WAZA FRESH KAKA WILE.

- Sawa baby, ila siwezi kuwaza tofauti na nilivyooona Dodoma kwa macho yangu, hoja ya posho inajadilika tena sana!, halafu love yah too! ha! ha! ha!

William.
 
ndo maana hamjui chanzo cha umasikini ni nini......

Hebu niambie unataka posho ibadilike iwe shilingi ngapi

- It does not matter, ninasema something needs to be done, hasara kwa taifa ya kutojadili hii hoja ni kubwa sana kuliko hizi blah! blah! blha!

William.
 
KAZI KWELI KWELI

Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi? Fikiri, matumizi nyumbani: chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni.

Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu. Matibabu hospitalini, pesa ya walinzi kwa mwezi, sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya; Zaka ya kanisani na misikitini, Kupanda Mbegu/ Sadaka, Shukurani ya Neno, Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzitupa hapo hapo), Madalali wa nyumba/viwanja, Pango la nyumba, Fremu ya biashara/ofisi, Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers];

Mafuta ya gari Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa); Tozo za kuegesha magari, Makato ya Mikopo, Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf. Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu, Harusi ya ndugu yako waa ukoo na zawadi, Sendoff ya mtoto wa mdogo wake rafiki yako na zawadi,
Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi,

Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara; Michango ya besdei party na zawadi; Ndugu wa kule kijijini, Mshahara wa Hausigeli na hausiboi;
Bodaboda, teksi na bajaj; Duka la dawa, Tuisheni ya mtoto, Kuchangia
wahanga wa mabomu na mafuriko. Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa, Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu.

Chakula cha mbwa, Mchango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa, Kuchangia
Uinjilisti Masasi, outing ya kitimoto, Ujenzi wa Nyumba Mabwepande, Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa).

Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi. Maji ya Traffik, Chai ya Nesi na Daktari, Kahawa ya Hakimu, Karani na PP. Vishoka waunganisha maji na umeme; Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa. Hivi hali inakuwaje? Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba, kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni.

umeme uliopanda bei, gesi iliyopanda bei, maji yaliyoadimika, bado contingency mana huu usafiri unaotembelea ball joint, bush, feni belt havijaf a - hapo bado service.

Bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie
wanakaribiana bei za restaurants, bado mchango wa kitchen pati na sare, baby shower.

Na hapo bado hujatoa watoto outing jumapili , upatu, mchango wa wawata, saluni, ukiangalia hapo hujanunua nguo wala kiatu kipya, kina sie mara dada aseme pampers zimeisha.n.k

Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above
19%. Ndipo unapoimba "Mwokozi nitoe roho niepuke na hili balaaa"

Ukifikiria kwa makini unajiuliza watanzania wana-survive vipi kwa style hii???
TAFAKARI………….CHUKUA HATUA…….!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom