William umeleta pointi ya msingi suala la kujiuliza kinachofanya Dodoma hoteli ziwe ni nini? Ukweli wabunge wenyewe wanapaswa kulaumiwa wameweka ubinafsi mbele hawajali maslahi ya Taifa, hata leo serikali ikeleta muswaada wa kujenga Hosteli utapingwa; wao wanachotaka ni pesa; nina uhakika kama wabunge wangeweka maslahi ya Taifa mbele hosteli ingekuwapo, au bunge liwepo wakati vyuo vimefungwa Dodoma pana vyuo vingi tu tatizo wabunge wetu wanataka kuwa kama wafalme, hata posho zikiongezwa hiyo halitakuwa suluhisho kumbuka ongezeko la posho litasababisha wafanyibiashara kuongeza bei ya bidhaa zao. Unamkumbuka congressman wa Texas aliyeamua kuwa atalala ofisini kwake wakati wa vikao vya congress hawa wetu wataweza?
Chama
Gongo la Mboto DSM
Chama
Gongo la Mboto DSM