Posho ya Vikao vya Bunge na Ziara za Kamati zifutwe

Hata kama bunge ni mhimili haimanishi watumie fedha au kujilipa posho kwa nguvu kwanza huko bungeni hakuna kazi kubwa zaidi ya kupiga domo tu.....na kusema ndiyooooo
 
Kuna kipindi Nilikuwa natamani sana Rais wa Kenya UHURU KENYATA kutokana na tabia yake ya kupeleka maslahi ya Kenya Mbele! ILA KWA SPEED HII. TANZANIA tunae Rais! Najitokeza Kuwaambia I LOVE MY PRESIDENT. This is our president of all time!

Kama unamkubali THE PRESIDENT karibu.

ipo siku hizi kauli zako zitakuponza

yani wiki moja tu umeona huyu ni rais au unatafuta sifa lamda atakuona akupe kitengo maana ccm ndiyo zao ukisifia utumbo wanakupa kajinafasi haya
 
1. Allowances lazima wapewe kwa sababu wapo nje ya majimbo/vituo vya kazi, hii inafanyika kisheria zaidi. Swali ni je, hizo allowance wanazopewa zinaendana na uchumi wa nchi yetu?

2. Mishahara ni haki yao vile ni wafanyakazi kama wengine, lakini swali ni je, hiyo mishahara ya milioni 12( kama ni kweli), inaendana na uchumi wetu?? Kwa nini kuwe na gape kubwa kati ya mbunge na wakili/daktari/mwalimu..nk? Lazima serikali iangalie na kuingilia.

3. Mikopo ya magari(shangingi), kwa maoni yangu serikali iangalie upya ni aina gani ya magari ya kuwapa waheshimiwa wabunge. Japo ni mikopo, sidhani kama wanahitaji kukopeshwa shangingis.

4. Mafao, kama mbunge anafanya kazi miaka mitano na kupewa marupurupu ya zaidi ya 100m, kwa nini mwalimu/daktari au mtumishi mwingine wa umma anayefanya kazi miaka 25+ asipewe marupurupu ya 500m?

Kuna sababu na haja ya kuangalia haya mambo kwa kina ziaidi. Nchi ni ya wa Tanzania sio ya watu wachache.

Sitting allowance wanayopewa wabunge haina uhusiano na kufanya kazi nje ya kituo cha kazi. Kama hufahamu, huwa wanapewa siting allowance na per diem (ambayo ndo ipo kisheria kwa kuwa wapo nje ya kituo cha kazi). Per diem wanapewa ya kipindi chote cha bunge (including weekends and holidays). Sittting allowance wanapewa kwa siku wazokaa vikao vya bunge.
 
Sitting allowance wanayopewa wabunge haina uhusiano na kufanya kazi nje ya kituo cha kazi. Kama hufahamu, huwa wanapewa siting allowance na per diem (ambayo ndo ipo kisheria kwa kuwa wapo nje ya kituo cha kazi). Per diem wanapewa ya kipindi chote cha bunge (including weekends and holidays). Sittting allowance wanapewa kwa siku wazokaa vikao vya bunge.

So kimsingi wanatakiwa walipwe perdiem tu na ile mishahara yao ya kifisadi baasi. Hizo posho nyingine zifungiwe kufuli
 
Pendekezo langu: Allowances zote ziingizwe kwenye mshahara wa mbunge. Then mshahara wa mbunge uanze kupigwa kodi ya PAYE. Hii itaingizia serikali mapato bila kuathiri maslahi ya wabunge wetu wapendwa. Mbunge atakae kataa hili huyo sio mzalendo.
 
Agizo la Raisi linasema 'Safari zote nje ya Tanzania zimepigwa marukufu' bila kusema za wabunge zinaruhusiwa. Neno zote kwangu mimi inajumuisha pia zawabunge. Sijui ni kwa nini Lizaboni anaona katika katazo hili halihusu wabunge
Sitting allowance ya wabunge zifutwe na kubakia na mshahara tu! Hela ya dereva sijui msaidizi zote ziondolewe! Malipo ya vikao vya kamati zifutwe. Mfuko wa Jimbo ufutwe, Safari za Ulaya za kamati vibali kwa Rais. Wabunge walipwe mishahara tu na magari wakopeshwe. Ni maoni yangu tu ila kwakuwa Rais alikuwa Mbunge najua gharama halisi anazijua.

La mwisho ni I LOVE MY PRESIDENT! Najisikia raha kusema huyu ni Rais wangu.
 
Hili wazo linataka tafakari ya kizalendo zaidi na hasa kutoka kwa waheshimiwa wabunge wenyewe wajipime wajitadhmini waangalie mapato hayo wanastahili? maana kuna fikra tafauti kutoka kwao.
Kwa kweli bunge ni sehemu moja wapo kuna matumizi makubwa sana ya pato la taifa udhibiti unahitajika.
 
ni kweli waungwana ni ufujaji mkubwa fedha za umma. ila naomba msaada wa ilani ya ACT wazalendo
 
Sitting allowance ya wabunge zifutwe na kubakia na mshahara tu! Hela ya dereva sijui msaidizi zote ziondolewe! Malipo ya vikao vya kamati zifutwe. Mfuko wa Jimbo ufutwe, Safari za Ulaya za kamati vibali kwa Rais. Wabunge walipwe mishahara tu na magari wakopeshwe. Ni maoni yangu tu ila kwakuwa Rais alikuwa Mbunge najua gharama halisi anazijua.

La mwisho ni I LOVE MY PRESIDENT! Najisikia raha kusema huyu ni Rais wangu.
NCHI HII ni yetu sote upo sahihi JPM ondoa posho zisizo na tija ,warsha ,kongamano ,workshop zinazotafuna .kataa mikopo ya wafadhili inayokumbatia haya matumizi.kuanzia bungeni ,wizarani hadi halmashauri.piga marufuku wakuu wa idara na vitengo kusafiri bila ruksa ya mkurungezi wa halmashauri.
 
Sitting allowance wanayopewa wabunge haina uhusiano na kufanya kazi nje ya kituo cha kazi. Kama hufahamu, huwa wanapewa siting allowance na per diem (ambayo ndo ipo kisheria kwa kuwa wapo nje ya kituo cha kazi). Per diem wanapewa ya kipindi chote cha bunge (including weekends and holidays). Sittting allowance wanapewa kwa siku wazokaa vikao vya bunge.
Asante kwa kurekebisha hilo. Kwa hiyo wanacho deserve ni per diem tu, hiyo sitting allowance ni utapeli tu.
Na Vipi kuhusu mishahara ? Huoni kuwa 12M ni nyingi mno? Na kwa nini wasikatwe kodi??

Ndio maana watu wanaukimbilia ubunge kwa kuwa ni dili sana.
 
Mh,magufuli kwa kasi ya mabadiliko uliyoanza nayo kila mtanzania anayeishi maisha ya kitanzania anakuunga mkono isipokuwa wapiga dilli najua hawakupendi lakini mungu amekuleta kwa makusudi yake zidi ya taifa lake,

tunakuomba haya juu ya wabunge,

1, kufuta posho za mamilioni wanazolipwa kwenye vikao vya bunge na vya kamati za bunge,

2,mishahara yao walipwe sawa na watumishi wengine wa serikali maana hawana umuhimu zaidi ya madakitari,walimu au watanzania wengine,

kwanini napendekeza hivyo,

1,wabunge wengi hizo pesa hakuna kazi zinafanya ya moja kwa moja kugusa maisha ya watanzania badala yake wanaishi kama wafalme wakati waliowachagua wanatabika na pengine serikali ndo inaangaika tu,

2,kuna wabunge pamoja na kulipwa pesa zote hizo lakini hakuna hata kikao kimoja wanafanya majimboni kwao cha kusikiliza shida za watanzania badala yake wanaishi dar na kwenye miradi yao,

3,kupunguza ubwe kubwa la wasomi na watalamu mbalimbali kuacha kazi na kwenda kwenye siasa wakidai ndo kunalipa sasa pesa zote zitolewe kwenye siasa na zirudi kwa wafanya kazi ,

4,tunakosa watu ambao wako tayari na niwazarendo kwa taifa kisa pesa nyingi zinazotumika wakijua watavuna nyingine bungeni huku wananchi hawana maitajio yao muhimu,

mh,ili kuondoa kero hii tunakuomba posho za mamilioni zifutwa na vikao viwe ni chakula maji tu maana tumeona watumishi wengine wanafanya kazi hata nje ya muda wa kazi lakini hakuna posho,

baada ya kufanya hivyo pesa zote zitakazotokana na kupunguza posho na mishahara ziende kwenye huduma za jamii,
hakuna cha sijui sheria ya posho na mishahara ya wabunge ya nchi gani wala nini na kama sheria zipo zifutwe ili tushirikiane wote kujenga nchi na kupunguza matabaka,tunawajua wataanza kunukuu vifungu lakini haku ambaye hataki aindoke tu,

mwisho maoni yenu,
 
Wanaotizamia fursa bungeni wamevimba kwa hasira na hofu na uchangiaji kwenye thread hii,
 
Mh,magufuli kwa kasi ya mabadiliko uliyoanza nayo kila mtanzania anayeishi maisha ya kitanzania anakuunga mkono isipokuwa wapiga dilli najua hawakupendi lakini mungu amekuleta kwa makusudi yake zidi ya taifa lake..,

JK ndiye Mungu wako?
 
Hzo ni ndoto kwa siasa zetu mbofu mbofu hzi. Watawala wa CCM wanalitumia bunge letu kufunika na kufanikisha maovu na madili yao kwa hiyo kuwaminya wabunge hasa wa ccm ambao ndio wengi ni sawa na kuiweka serikali hatarini kukwama mambo yake hasa bajeti na mengineyo kupita bungeni. Na hii ndio simple logic ya wabunge kupewa mishahara mikubwa na marupurupu kibao wakati walimu na madaktari na watumishi wengine wa umma wakiendelea kuuumia kwa kisingizio cha serikali haina fedha!

Wenzako wanaongelea Tanzania kwanza wewe unaongelea vyama, wewe ni mkimbizi NINI?
 
Wangejenga Hostel kadhaa za serikali ambazo kipindi cha Bunge kila mbunge atalala huko kwa gharama za serikali,Mbunge apewe hela kidogo tu ya kujikimu.Wakisingisingizia gharama za hotel tayari Hostel za serikali zipo na Chakula kiwepo kwa bei Rahisi
 
Back
Top Bottom