Porokwa apasua jipu la CCJ

Wewe UNAYEJIITA Mlengo wa kati, shari ufahamu kuwa kuna tofauti kubwa ya tuhuma za ufisadi na uhaini wa kuasi chama.

Kwa chama cha siasa, kosa la uhaini wa kuasi chama ni kosa kubwa sana kuliko ufisadi. Ufisadi umefanyika ndani ya serikali na ndiyo maana kina Nape wanazungumzia kuwaondoa katika chama wanaowatuhumu. Hawazungumzii kuwafikisha mahakamani.

Sasa kama wanataka kuwaondoa katika chama wanaowatuhumu, basi lazima wawaondoe kwanza wasaliti wa kwenye chama…

Wewe unaejiita SPANNER usaliti wa Chama kwa Mwanachama una mgusa vipi Mtanzania ambae hana Chama? Halafu mwanzilishi wa Chama lazima jina liwe kwa msajili sasa hawa akina Sitta,Mwakyembe na Nape majina yao yako kwa Msajili wa vyama vya siasa Nchini? Mi naona ni hoja ya kijinga kabisa!
 
Katika mkutano wake na waandishi, Porokwa katika kuwashunghulikia kina Nape na wenzake amesema, "Nikiwa kada niliyefundishwa na kuaminishwa kwamba uongozi ni dhamana na ninayeamini katika msingi wa Nyerere, nimeamua kusema ukweli ili ukweli ubaki ukweli." Je, yuko wapi anayetaka kueleza ukweli zaidi ya huu?
 
Kama kweli Nape ni mmoja kati ya waanzilishi wa CCJ, mimi binafsi namkubali mpaka hapo alipo. Kwa muonekano wa kawaida tu CCJ, ndio imekamata usukani baada ya CCM magamba kuangukia pua, baada ya vikao vya Dodoma.CCJ imeonyesha kuwa ni Chama ambacho hakikuwa lelemama kama wengi tunavyodhani, kilijiwekea chanel nyingi za kukamata siasa za Tanzania. Chanel ya Ofisi ya Tendwa ilishindikana kwa kuzibwa na Rechels lakini bado CCJ haikukata tamaa na sasa, imetua kwenye kiini cha CCM kama kirusi kikiwamega wale walikuwa wanakibania. CCJ sasa iko na ina nafasi ndani ya CCM. Ndio maana wale waliopinga usajili wake sasa wanapata shida kubwa, shame on them and shame on Tendwa. CCJ sasa imepata usajili ndani ya CCM kwa kutumia njia za panya, sasa inawamega akina Rechel lazima waipate joto ya jiwe. Na kwa msingi huo hata Tendwa huu ndio msimu wako wa mwisho, kwani si CDM wala CCJ iliyondani ya CCM watakaobaki na wewe baada ya uchaguzi wa 2015 kama mmoja wapo atashinda, kwani Mafisadi wenzako uliokuwa unawapendelea mpaka sasa upepo unawavumia vibaya mno katika siasa za Tanzania. Mpaka sasa wanaona aibu kujitokeza hadharani badala yake wanatuma messanger wao kama Daniel Ole Porokwa kutueleza waanzilishi wa CCJ. Wanzilishi wa CCJ sisi kwetu si habari mpya kwani siasa za Tanzania baada ya kashfa ya Richmond kusomwa kule Dodoma zilionekana wazi kuambata na vitendo vya wazi vya watuhumiwa wa Richmond kulipa kisasi na zililenga zaidi kuwaengua walihusika kuwatema ndani CCM.Katika vita ile wapambanaji wengi wamepotezwa kwenye siasa, kama akina Chegeni, Sererii nk. Wengine bado walipita Mlango wa nyuma kama ndugu yetu Shibuda. Na wengine walijaribu kupita mlango wa nyuma, bado wakazuiwa (Mpendazole). Lakini wengine waliendelea kupigana ndani na sasa wameshika usukani. Tunajua walivyokuwa ndani ya misukosuko ya kutemwa CCM walipenda kukisajili CCJ ili kiwe shock absorver kama watadondoshwa. Na wangedondwa pia CCM kubwa ingeyumba, wazee wa CCM waliliona hilo walimweleza mkulu kuwa ukiwatema hao kamwe hatutakuwa salama. Hatimaye walibakizwa CCM na ndio mwisho wa harakati za Usajili wa CCJ. Kwa misingi mingine CCJ iliunganishwa ndani ya CCM. Si kuunganiswa tu, sasa inatoa amri na kuwasaga wazi akina Rechel.
CCJ pambana nao huko ndani ya CCM mpaka waone kuchungu watoke wenyewe. Na hii inanipa mwanga kuwa mwaka 2015 uchaguzi utakuwa kati ya CDM vs CCJ.
 
Hivi huyu Porokwa bado anadunda CCM? kutokana na haya yote aliyoyamwaha hadharani, CCM inachukua hatua gani? Mimi nina shauku kubwa kwanza kujuwa iwapo CCM itayakubali au itayapinga. Patamu hapa!
 
ni vizuri mkiendelea kuomba mungu aibariki tanzania labda kuna siku mtaomba kwa imani ya kweli na mungu akawasikia.
Tumekuwa na tabia ya muda mrefu ya kupenda kusikia yale tunayoyataka, na si vinginevyo.
Kuna kipindi anaweza akaingia mtu hapa na hoja fulani, utaona namna watu wanavyom-crash na kusema toa ushahidi. Katika hili sioni mtu akidai ushahidi, watu wanajikita moja kwa moja katika kujadili na kutoa laana na kashfa na lawama, hawataki ushahidi kwani wanajua ukitolewa ushaihidi huo utaonyesha taswira na ukweli halisi tofauti na kile wanachotaka na kupenda kukisikia.
Watu wa mahari hapa wanafikiri vizuri sana, lakini ushabiki na mapenzi huondoa mara moja nguvu na uwezo wao huo.
Kweli mungu ibariki tanzania.

Kuna ushahidi mkubwa zaidi ya ule wa eye-witness? Hakuna ushahidi written hapa. Porokwa alikuwapo, aliona! What else? Stori yake imekuwa corroborated na Six mwenyewe aliposema yeye alikuwa ni presidential material.
 
Intelijensia ya CCM ilishanasa harakati za kuanzishwa kwa CCJ mapema sana, na chama kikachukua hatua mapema ya kukaa na hao "wasliti wa CCM" na wakafikia "muafaka" ambao utekelezaji wake leo unaonekana vizuri, kwani vinara wote wa CCJ (Wasaliti) wameshinda viti vyao vya Ubunge na kupewa vyeo zaidi, Mpendazoe imemkera sana, maana yeye aliingia kichwakichwa CCJ wakati wenzake walikuwa wanatwanga kotekote. Parokwa hana news yoyote kwa CCM kuhusu mada ya CCJ, ni jinsi tu ya kuondoa hasira zake, maana na yeye ametoswa hana cha maana CCM. HIVO NDIVYO NIONAVYO MIMI!
 
Kwa muonekano wa kawaida tu CCJ sasa ndio imekamata usukani baada ya CCM magamba kuangukia pua baada ya vikao vya Dodoma.CCJ imeonyesha kuwa ni Chama ambacho hakikuwa lelemama kama wengi tunavyodhani, kilijiwekea chanel nyingi za kukamata siasa za Tanzania.

Chanel ya Ofisi ya Tendwa ilishindikana kwa kuzibwa na Rechels lakini bado CCJ haikukata tamaa na sasa, imetua kwenye kiini cha CCM kama kirusi kikiwamega wale walikuwa wanakibania. CCJ sasa iko na ina nafasi ndani ya CCM. Ndio maana wale waliopinga usajili wake sasa wanapata shida kubwa, shame on them and shame on Tendwa.

CCJ sasa imepata usajili ndani ya CCM kwa kutumia njia za panya, sasa inawamega akina Rechel lazima waipate joto ya jiwe. Kwa misingi mingine CCJ iliunganishwa ndani ya CCM. Si kuunganiswa tu, sasa inatoa amri na kuwasaga wazi akina Rechel.

CCJ pambana nao huko ndani ya CCM mpaka waone kuchungu watoke wenyewe. Na hii inanipa mwanga kuwa mwaka 2015 uchaguzi utakuwa kati ya CDM vs CCJ.

Haa ha ha ha, you made my day..
 
Intelijensia ya CCM ilishanasa harakati za kuanzishwa kwa CCJ mapema sana, na chama kikachukua hatua mapema ya kukaa na hao "wasliti wa CCM" na wakafikia "muafaka" ambao utekelezaji wake leo unaonekana vizuri, kwani vinara wote wa CCJ (Wasaliti) wameshinda viti vyao vya Ubunge na kupewa vyeo zaidi, Mpendazoe imemkera sana, maana yeye aliingia kichwakichwa CCJ wakati wenzake walikuwa wanatwanga kotekote. Parokwa hana news yoyote kwa CCM kuhusu mada ya CCJ, ni jinsi tu ya kuondoa hasira zake, maana na yeye ametoswa hana cha maana CCM. HIVO NDIVYO NIONAVYO MIMI!

Na Nape kwa nini amekuwa mbogo -- iwapo ni kweli unayoyasema? Angekaa kimya na kuchekelea tu -- tongue in cheek.
 
Hili swala ukiliangalia juu unaweza usione Mantiki yake ila kwa kweli hawa waliotajwa kwenye hii Issue kwanza ni Wasaliti,Wanafiki,Watu wasiokuwa na Misimamo na kikubwa zaidi ni Waoga na ninaamini kabisa wanachama wa ccm hata mimi ningekuwa mmoja wao kamwe tusinge waamini tena daima.

Mfano pa1 na kashifa zote ambazo Lowasa anatuhumiwa nazo kwa sasa hii skendo Ya Sitta na uanzishwaji wa ccj let say Mwaka kesho hawa wawili wapambanishwe kwenye kuwania Uenyekiti wa Chama amini usiamini Sitta atagaragazwa vibaya mno sababu pa1 na yote yanayosemwa juu ya Lowassa bado amekuwa mwanachama Madhubuti na Mtiifu kwa ccm.

Dhambi kubwa aliyoifanya Sitta ni ya Usaliti na Unafiki labda aombe Radhi lasivyo amekwisha Kisiasa coz Siasa ni Credibility ya Watu juu yako so hilo likiondoka kwa Watu basi we hufai kuwa kiongozi wao.
 
Wewe unaejiita SPANNER usaliti wa Chama kwa Mwanachama una mgusa vipi Mtanzania ambae hana Chama? Halafu mwanzilishi wa Chama lazima jina liwe kwa msajili sasa hawa akina Sitta,Mwakyembe na Nape majina yao yako kwa Msajili wa vyama vya siasa Nchini? Mi naona ni hoja ya kijinga kabisa!
Nafikiri wewe ndiye mjinga kwa kufikiri kila mwanzilishi lazima jina lake liwe kwa msajili wale ni wawakilishi tu.
 
Hakuna jipya hizo zote ni harakati za kupiganga ufisadi, labda tumuulize mh. Porokwa anayesema hayo kwa maslahi ya CCM au kwa maslahi ya kundi fulani? Kutetea rasilimali za watanzania si usaliti wasaliti ni mafisadi,

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Kuanzishwa kwa CCJ ilkuwa hatua ya baadhi ya viongozi wa CCM kutoridhika na mwelekeo wa chama chao CCM.. Kwa mtazamo wangu CCJ haikuwa tofauti kubwa na CCM isipokuwa ni waumini wa chama hicho kuuunda dhehebu jingine nje kwa kutokubaliana na mafundisho ya mhubiri JK..

Hakuna dhambi wala kosa kubwa kwa muumini wa kiitikadi kuondoka ktk chama ambacho kinakiuka mafundisho ya kimaadili ya chama kama isivyokuwa haramu kuhama dhehebu la dini kuingia dhehebu jingine ama kuunda dhehebu jipya linalofuata maadili halisi ya mafundisho..

Kama kuna wakati CCM imejivua gamba basi ilikuwa wakati wa muafaka baina ya makundi ndani ya chama..Na naweza kusema kina Sitta, Mwakyembe, Nape na wengineo walifanya jambo la maana sana kuweza kumweka sawa JK ambaye hakutaka kabisa kusikia upande wa pili na imemgharimu sana ktk uchaguzi uliopita.

Hivyo katika kutafuta suluhu ndani ya chama ndio tunawaona kina Nape wakipewa madaraka. Ikumbukwe tu jinsi Nape alivyokuwa akipigwa vita toka CCM vijana, leo tunamsikia kuwa katibu wa itikadi, hivyo ni somo kwetu kutambua kwamba Nape hakupewa nafasi hiyo hivi hivi tu.. Nadhani n katika muafaka uliopitishwa na chama kurudisha imani ya wanachama wake na kuondoa makundi baina yao.

Kama tunavyomjua JK, ukijipendekeza sana msitari wa mbele basi yeye hukupachika nafasi ambayo wewe hupigia kelele akuone ukiifanya kazi...Na wengi wameshindwa, wenmgi wamejikuta wakiiingia wao ktk Ufisadi hali mwanzo walikuwa wapiga kelele wakubwa...Hii ndio Tanzania yetu wakubwa zangu.

CCM wanawajua wote walijiunga na CCJ, iwe waasisi au wananchama kwa sababu majina yao yalipelekwa kwa msajili kama tishio kwa chama CCM. Hakuna jipya na wala hakuna mtu anayepasua ukweli hapa kwani CCM wanawajua wote waliokuwa wametaka kujiengua na kuunda CCJ kwanii hili sii jambo la siri na haiwezi kuwa siri kama chama kilitaka kujiandikisha na kikakataliwa, na hata kama kulikuwa na siri sio Tanzania yetu - hakuna siri..

Kwa hiyo, tunapoteza muda mwingi sana kuwazungumzia WATU, tukisaghau sisi wenyewe kuwa ni mazuzu kuliko hata hao viongozi tunaowazungumza. Hivi kweli mtu unaweza kumchagua rais wako kwa ahadi ya kuleta flyover mji mzima wa Dar wakati rais huyo anashindwa hata kufanyia ukarabati reli ya kati?.. Unaweza kweli kumchagua rais anayeahidi kuibadilisha Kigoma na kuwa Dubai in five yrs? hii sii akili ya wendawazimu kweli? kisha wepesi wa kuwazungumza kina Nape kwa usaliti wa chama hali nyie wenyewe mnaisaliti nafsi yenu..
 
Haya ndo maelezo ya bwaba Porokwa nimeyatoa kwa Michuzi blog. Watasema yote mwaka huu mpaka kieleweke...

KADA WA CCM AIBUKA NA KUWATAJA WAANZILISHI HALALI WA CHAMA CHA JAMII (CCJ)

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel ole Porokwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi juu ya ukweli kuhusu waanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).hapo chini ni taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimeripoti maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Mh. Anthony Komu, kwamba Nape Nnauye alikuwa mwasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ). Madai haya yakathibitishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe ambaye alitaja watu kadhaa nikiwamo mimi, kuwa walishiriki au waanzilishi wa chama hicho ambacho hakikuwahi kufanikiwa kupata usajili wa kudumu.Hivyo basi, nimewaita hapa leo hii, ili pamoja na mambo mengine, kueleza ukweli wa hiki ambacho kimeelezwa vizuri na Mheshimiwa Mpendazoe na kimenukuliwa vema na vyombo vya habari, hasa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI.Nimeamua kufanya hivyo kwa misingi miwili mikuu. Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaonyeshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita na tuamini katika hiyo njia tunayoelekea.Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu, ni kusema ukweli, na kwamba uwongo na fitina ni mwiko kwa viongozi na wachama wa CCM.Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mh. Nape Nnauye, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe na Mh. Fred Mpendazoe.Aidha, nilikutana mara moja na Mh. Samwel Sitta baada ya Mh. Nape na Dk. Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza. Naye Mh. Sitta alinieleza kuwa nilichoelezwa na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe hakina chembe ya mashaka.Katika mikutano zaidi ya mitano niliyofanya na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wenzangu walinieleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM kwa hoja kuwa kilipofikia chama hicho hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka ya kuongoza dola.Walisema CCM hakiaminiki tena machoni mwa wananchi na kimepoteza mvuto mbele ya umma; yote haya ni kwa kuwa chama hiki kimekuwa kinaacha ile misingi kama ilivyoasisiwa na waasisi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Walinieleza, kihistoria Chama Cha Mapinduzi ni chama cha ukombozi na kilijipa kazi ya kupigania wanyonge, lakini kikafika mahali historia hiyo ikaporomoka kwa kuingia katika mikono ya watu wasiojali, wasiokuwa na maadili ya uongozi na labda wasiowaaminifu.Wakati wote wa mazungumzo yetu, Mh. Nape na Dk. Mwakyembe walikuwa wakisisitiza umuhimu wa mimi kukubali kujiunga haraka na CCJ, ili kurahisisha upatikanaji wa usajili wa kudumu wa chama hiki, lengo likiwa CCJ kiweze kishiriki katika uchaguzi mkuu wa 2010.Hata hivyo, kila muda ulivyozidi kusogea, ndivyo nilivyopata kujua undani Mh. Mwakyembe na Mh. Nape wa kutaka kuanzisha chama chao cha siasa, kwamba kinachowasukuma katika mpango huo, ni matakwa binafsi ya kisiasa na hivyo nikaanza taratibu kuwa mbali na mkakati wao.Nimeamua kuyasema haya baada ya kuwasikia Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wakimkana Mh. Mpendazoe na kimsingi wakikana chama chao – CCJ. Napenda kuwaambia Watanzania, kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa na kuasisiwa na viongozi hao wawili, pamoja na Mh. Sitta kama ambavyo Mpendazoe alivyoeleza.Katika mpango huu, mimi niliahidiwa kusaidiwa kugombea ubunge katika jimbo la Monduli kupitia CCJ, huku Mh. Nape akiahidi kusimama katika jimbo la Ubungo.Nimeyasema haya ili kuondoa unafiki unaojengeka ndani ya chama chetu na taifa kwa jumla, kwamba kuna kikundi cha watu wanaotaka kupotosha umma juu ya uanzishwaji wa CCJ na ujio wake ili umma uwapime na uamue juu ya watu hao.Mimi kama kada wa CCM niliyefundishwa na kuaminishwa kwamba uongozi ni dhamana na ninayeamini katika misingi ile aliyotuachia Mwalimu Nyerere, nimeamua kuyasema haya ili ukweli ubaki ukweli katika historia ya nchi yetu.Kuyumba kwa chama chetu na hata kufikia hatua ya kuanza kuporomoka kwa kupoteza nafasi mbalimbali kwa vyama vingine kwa wingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi katika nchi hii, ni kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye malengo na agenda zao binafsi, tofauti na zile za chama chetu.Hii bila mashaka inanipa sababu ya kuamini kwamba Bunge la Tisa kama mmoja wa mihimili muhimu wa dola, chini ya Mh. Samwel Sitta lilitumika vibaya kufanikisha agenda nyingine ya kuanzisha chama kingine badala ya CCM.Ni vema Rais Jakaya Kikwete akajua kuwa ndani ya timu yake, kuna wachezaji ambao wako tayari kujifunga na kuinyima timu yao ushindi. Ni vema akaamua kuachana nao kwa maslahi yake na chama chake.Ni maoni yangu kwa dhati kabisa na rai yangu kwa viongozi wa chama, kwamba ni wakati mwafaka watu kama hawa wawajibike au wawajibishwe kwa matendo yao. Baada ya mimi kushutukia na kutokuwa na imani na minendo ya waasisi wa CCJ na hivyo kujiondoa, nilipata taarifa kuwa baada ya kujiridhisha kuwa chama chao hakitasajiliwa na kuwahi uchaguzi wa 2010, waliamua kufanya mazungumzo na viongozi wa Chadema na kukubaliana kuwa wote kwa pamoja watajiondoa CCM na kujiunga na Chadema ili kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe. Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe.Na hili la Mpendazoe ambaye alikuwa mbunge, akaacha mishahara kadhaa na mafao yake kwa makubaliano ya kazi ya pamoja ambayo nilishirikishwa katika hatua za awali na mwisho wake wakamtosa na sasa wanamkana hadharani, ni moja ya sababu iliyonisukuma sana kutoa ushuhuda huu. Daniel ole Porokwa,Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Mzee MKJJ naona bado yupo kimya kwenye topic za waasisi wa CCJ ! Yeye alikipigia sana debe humu wakati ule!
 
Great thinker use your thinking!!!

1. Kwa kipindi Sita, Mwakyembe na Nape walipoa asisi CCJ walikuwan sahihi kabisa na ilihitaji ujasikri mkuu ...Lazima waheshimiwe kwa hilo. Hali ya nchi ilikuwa Tete mapacha watatu walikuwa wanayumbisha nchi na CCM yao!!
2. Wakati CCJ ilipokuwa ina asisiwa ilikuwa ni jambo muhimu na huwezi kuwaita wahaini watu waliokuwa wanafanya hivyo wakati huo.Ilikuwa muhimu na CCM ilikuwa inawajua na wengi walipenda CCJ ikomae na ifanye kazi lakini Mapacha 3 waliimaliza CCJ kwa manufaa yao..
3. Sababu za kuasisi CCJ ndio hizi zilizoleta Gamba Leo. Na mleta gamba wa kweli lazima alione hilo na aone umuhimu wa waanzishi wa CCJ
4. Bila CCJ hapangekuwa na Gamba leo...JK ataniunga mkono na watumie hawa jamaa kama unaniunga mkono.
5. Kikwete atawatumia hao mnaowaona hawafai sasa ..SITA, NAPE na MWAKYEMBE ni MTAJI kwa KIKWETE kwa kuendesha Gamba kampeni kwani Gamba ndio CCJ. nani haoni hilo?
6. Mapacha watatu kwa kuwa ndio waliolengwa CCJ na ndio wanolengwa na Gamba ...watafanya kila upuuzi wanoujua kuwamaliza Mapacha watatu wa CCJ aka Nape, Mwakeyembe Na Sita.
7. Nape, Sita na Mwakyembe waheshimiwe ... kwa kuanzisha CCJ NA GAMBA!!!
8. Kikwete watumie ....Kikwete watumie ...kikwete watumie...!!
9. Kiwete wachana na viporojo vya mafisadi wa CCM wanaowatisha na kuwasumbua mapacha wa CCJ
10. Nani anaujasiri wa kuanzisha CCJ pale CCM ..wote waoga... wale waliokuwa na uajsiri wa kujitena sio wahaini ni wajasiri ...watumike Gamba!! Kikwete analijua hilo na watanzania wanalijua hilo!!

Kwa hiyo kwa ufupi ni kuwa vita vya magamba bado vinaendelea.... ngoja tuendelee kukaa mkao wa tahadhari maana wagombanapo fahari wawili....
 
Ni muhimu watu wakaangalia pande zote za shilingi. Ole Porokwa alishawahi kutangaza kumpinga Lowasa, ghafla akabadilika na kwenda kwenye vyombo vya habari kumuomba radhi kwa kutaka kutumia haki yake ya kikatiba na kidemokrasia!!! Porokwa amekuwa ni mtu asiyeeleweka kwa vipimo vyote vya uelewa na kauli zake ni za kuziangalia kwa umakini.

Kama aliitwa ajiunge CCJ hayo angeyasema mapema tena wakati kuna mvurugano ndani ya CCM, lakini angalia ni wakati gani ameamua kuyasema na jiulize ni kwanini.
Siku chache zilizopita mifasadi(hasa pacha 3) walisemekana kutumia mbinu za hali ya juu kujinasua.
Tunakumbuka mapacha walisema tuhuma za kutajwa si ushahidi wa wao kufanya maovu na kuwapa muda wa kujitoa au kuachia nyadhifa ni kuwaonea. Walisema mbona watu wengine wanatajwa katika mambo kadha wa kadha na hawapewei muda iweje wao?

Kitendo cha Nape kutajwa kuwa mwanzilishi wa CCJ kimetumiwa na mapacha ili kujenga hoja ya kuwa kama tuhuma tu zinatosha mtu kuachia ngazi basi Mwakyembe na Sitta nao wapewe muda wa kujitahmini. Ni kwa mantiki hiyo Porokwa amewezeshwa ili awe 'whistle blower' na hapa ndipo mapacha watatu watakapoponea. Utashangaa ishu itavaliwa njuga sana kwasababu mapacha watatu watagawa pesa(wanayo) kununua wasema hovyo ili kujenga hoja ambayo sasa inashika kasi.

Hapa kuna wafa maji (mapacha 3) na wanashika kila kilicho karibu nao hata kama ni ubua. Tuliangalie suala hili kiundani na mtazamo mpana, ushabiki unaweza kuwa ni sehemu ya kuokoa mapacha watatu bila kudhamiria. Kama kuanzisha chama ni usaliti porokwa alitakiwa aseme hili mapema ndani ya vikao vyao au vyombo vya habari, kujitokeza leo ni kununuliwa ili awaokoe mapacha watatu, hasa ikizingatiwa kuwa baada ya 'kutubu' EL alimweka karibu sana.
Sasa mapacha watakuwa na hoja, endapo wao wanatajwa bila ushahidi(kama wanavyodai) basi kila anayetajwa naye afuate mkondo. Kama walivyoanza kuwanunua wenyeviti wa mikoa wa CCM hili watalitumbukiza tu kushadidia hoja yao. Kama hoja ililenga kumweka Nape mahali pagumu, itasaidia kuwaweka wengine mahali rahisi, lakini itakuwa ni jiwe moja kwa ndege wawili kwababu Nape sasa ni mwiba kwao, na akina Sitta na Mwakyembe ni mwiba wa zamani, kama kuna 'kisu' chenye makali pande zote hicho kinafaa mapacha 3.

ni wakati wana CDM popote walipo wajiulize kuna umuhimu wa kulikuza au kulipigia baragumu jambo hili?
Time will tell.
 
Jamani njaa ni mbaya sana huyu Parokwa alikua anampinga sana Lowassa leo amegeuka Mtetezi wa Lowassa! Njaa inaleta aibu na fedheha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom