Pongezi kwa Zakazakazi kuufafanua mgogoro wa Israel na Palestina kwa facts na kuweka udini pembeni

Hiyo ardhi awali ilikaliwa (kwanza) na Wafilisti kaka, kabla Joshua hajaamuriwa awasngamize wenyeji wote ili Israel akae.

Tukiongea uongo hata haisaidii ukristo wetu
Mkuu kwenye History haupo Sawa... Miaka ya Joshua ilikuwa ni time za kurejea kwenye Nchi ya Ahadi ambayo Ibrahim alishapewa na kina Isaac pia waliishi kabla hawajaenda Israel so stuka. Ibrahim ndio alielekezwa hiyo nchi na haikuwa na kitu wala kukaliwa na watu
 
Mawazo yako ni kama yangu niliochangia sehemu flan kuhusu chanzo cha mgogoro. Watu wengi hawaanzii mwanzo wa mgogoro. Wao wanaanzia Israeli kashaingia Kanaani na kuvamiwa na warumi kisha wapalestina wakachukua ardhi yao. Sijui ni maksudi au wanasahau.

Kingine ambacho sijui, hawa wapalestina ndo wale wafilisti wa mwanzo au hawa ni wengine? Na kama sio, wafilisti wa kale masalia yao ni akina nani wa sasa?

Unajua vitu hivi vinachanganya

Nuhu alizaa watoto wa 3, Hamu, Shamu na Yafeti

Yafet ndio baba aliendeleza ukoo wa akatokea Abrahamu

Shamu ndio baba wa Wakanaani (palestina ya leo)

Ila wanavopigana kama hawajuani kabisa

Mfano mwingine

Lebanon na Jordani ni watoto wa Luthu aliozaa na mabinti zake 2 (Amoni na Moabu) na wakati wana Wa Israel wanatoka Misri walionya na Mungu wasiwapige kwasababu hizo nchi amewapa

Ila sasa hivi ni maadui wakubwa
 
Hiyo ardhi awali ilikaliwa (kwanza) na Wafilisti kaka, kabla Joshua hajaamuriwa awasngamize wenyeji wote ili Israel akae.

Tukiongea uongo hata haisaidii ukristo wetu

Iko hivi

Ibrahimu alinunua Ardhi ambayo alimzikia mkewe sara alipofariki maana aliomba apewe ardhi aweke na sehemu ya makaburi, hapo ndipo ikawa sehemu yao ya kuishi

Kumbuka wakati ule Yusufu yupo Misri, Walikuja watu 70+ ukoo wake kuja misri wakati ule wa njaa it means walikua wanaishi kwenye ardhi waliyonunua.

Wanaporudi Kanaani sasa ilikua kama kwenda kuteka
 
Miaka 1800+ hawakuingiliana na jamii zingine huko walikokua?.

Je Judea ile ndiyo hii nchi yote inayozozaniwa!?

Kama yesu alikua na rangi ya shaba kwanini netanyahu ni mweupe pee!?
Acha kukaza hicho kichwa mzee wangu, Yesu aliishi karne ipi na netanyau yupo karne ipi.?

Ww n msukuma kwa sababu baba ako n msukuma lkn mbona ww sio Mmasai kwa sababu mama ako n Mmasai.?

Zamani watoto wakike wanavunja ungo wakiwa na miaka 12 ila sasa hv ht 9 tayari, hy inatokana na life style pamoja na sababu za kimazingira.

Pia kuna kuchangamana na watu tofauti tofauti zinapelekea watu kubadilika.
Mambo hayo n simple sana kuelewa ukiamua kufungua akili ili uelewe
 
Wakristo wanatumia nguvu kubwa mno mno kuongea uongo, why? Ila naamini kabisa mnaujua ukweli ila chuki zimewajaa vifuani mwenu dhidi ya waarabu na waislamu kwa ujumla

Katika hii page ni mkristo mmoja tu ameongea ukweli na kuweka kando unafiki, ubarikiwe sana mkuu Dannion
 
Acha kukaza hicho kichwa mzee wangu, Yesu aliishi karne ipi na netanyau yupo karne ipi.?

Ww n msukuma kwa sababu baba ako n msukuma lkn mbona ww sio Mmasai kwa sababu mama ako n Mmasai.?

Zamani watoto wakike wanavunja ungo wakiwa na miaka 12 ila sasa hv ht 9 tayari, hy inatokana na life style pamoja na sababu za kimazingira.

Pia kuna kuchangamana na watu tofauti tofauti zinapelekea watu kubadilika.
Mambo hayo n simple sana kuelewa ukiamua kufungua akili ili uelewe
Unamjua kila aliyevunja ungo zamani!?..Nina mabinti wa miaka 14 na 9,na hawajavunja ungo
 
Naomba kujua asili halisi ya wapalestina?@sky soldire ili tuwaombee tu wakakatiwe kaeneo hata size ya dar waunde taifa lao?wasipoangalia miaka 100 ijayo wapalestina watakua wamebaki 50%duniani kote

wapalestina ni waarabu kutoka mataifa ya jirani
jordan,syria,lebanone,saudia na Egypt

kifupi kulikua hamna Nchi inayoitwa palestina kabla ya israel ! Palestine ulikua ni ukanda
 
Watu wanapotosha sana.
Wafilisti walikuwepo enzi na enzi zaidi ya miaka 500 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Enzi za Ibrahimu,
MImi ni Mkristo.
Ukweli ni kwamba Wafilisti ndio
Wakaazi wa kwanza pale Kanaan/Israel.

Ona
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.

Mwanzo 10:14
Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.

Mwanzo 21:32
Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Mwanzo 21:34

sasa alokwambia wafilisti n waarabu ni nani??
 
Watu wengi huzihusisha dini kwenye mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu.

Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.

View attachment 2779426

Kuna sehemu mbili za waarabu.

1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.

2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.

Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah.

Sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza.

Hili ni eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9.

Lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.

Asilimia kubwa ya watu hawa ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu.

Watu hawa hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).

Hamas ni kikundi ambacho kimechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel.

Hii ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.

ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.

Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni.

Wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani.

Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru.

Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena.

Baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.

Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina.

Hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao'.

Wayahudi wakasambaa Ulaya yote ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.

Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita.

Kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea.

Akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi.

Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu.

Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.

Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu.

Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.

Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu.

Hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.

Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, zilioitwa Zionism.

Harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina.

Hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi.

Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.

Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.


Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka.

Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.

Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.

Ramani inahusika.

View attachment 2778309

Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.

Itaendelea...
Ki ufasaha unatakiwa uandike wakristo. Siyo wakristu. Pia ni Yesu Kristo na siyo Yesu Ktistu.
 
Mkuu taifa la Israel rasmi lilianzishwa mwaka 1948 kwa msaada wa Serikali ya Uingereza na Marekani ndio walichukua jukumu la kuwasafirisha Jews kutoka nchi mbalimbali za Ulaya kwenda Israel na hata Raman ya Nchi ya Israel rasmi imeingia ktk uso wa Dunia mnamo mwaka huo kabla ya hapo hakukuwa na taifa la Israeli duniani
Kwanza tujiulize ramani ya dunia ilichorwa mwaka gani.? Kwa vyovyote vile ramani ya Israel hauwezi kuwepo kwenye ramani ya dunia kwa sababu kwa muda huo ramani inachorwa hapakuwa na nchi ya Israel mana walisambaa duniani kote.

Ila kabla ya mchoro wa ramani ya dunia nchi ya Israel ilikuwepo.

Hvy baada ya vita vya pili vya dunia na Israel kupewa eneo bc ni lazima nchi yao ionekane kwenye ramani ya dunia.

Ni sawa na sasa hv Morogoro ikijitawala yenyew bc lazima ramani ya dunia ichorwe upya kuonyesha nchi ya Morogoro.
 
Back
Top Bottom