Pongezi kwa Zakazakazi kuufafanua mgogoro wa Israel na Palestina kwa facts na kuweka udini pembeni

Watu wengi huzihusisha dini kwenye mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu.

Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.

Photo by thabith chumwi zakaria on October 10, 2023. May be an image of map and text that says...jpg


Kuna sehemu mbili za waarabu.

1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.

2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.

Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah.

Sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza.

Hili ni eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9.

Lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.

Asilimia kubwa ya watu hawa ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu.

Watu hawa hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).

Hamas ni kikundi ambacho kimechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel.

Hii ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.

ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.

Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni.

Wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani.

Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru.

Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena.

Baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.

Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina.

Hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao'.

Wayahudi wakasambaa Ulaya yote ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.

Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita.

Kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea.

Akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi.

Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu.

Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.

Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu.

Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.

Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu.

Hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.

Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, zilioitwa Zionism.

Harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina.

Hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi.

Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.

Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.


Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka.

Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.

Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.

Ramani inahusika.

View attachment 2778309

Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.

Itaendelea...
Hii nondo haina pdf yake?
 

Palestine​

Also known as: Eretz Yisraʾel, Philistia, Syria Palaestina
 
Porojo nyingi kuliko uhalisia.

Unakubaliana vipi na historia ya wakristo waliyiwauwa wayahudi kwa imani yao na kuikataa historia ya waliowapokea walipokuwa wakimbizi na kuwahifadhi?


Mfano Tanzania imepokea wakimbizi wa Burundi na Rwanda ikawapa eneo, baada ya miaka kadhaa wanadai hapo ni kwao kwa kuwa wamezaliwa hapo.

Inakuja hiyo?

Iwe miaka 3000 au 1000 nyuma hakujawahi kuwa na nchI ya wayahudi wala inayoitwa Usrael.

Vipi imani ya kiroho iwe na nchi?
 
Potojo nygi kuliko uhalisia.

Unakubaliana vipi ma historia ya wakristo wliyiwauwa wayahudi kwa imani yao na kyikataa historia ya waluowapokea walipokuwa wakimbizi na kuwahifadhi?


Mfano Tanzania imepokea wakimbizi wa Burundi na Rwanda ikawapa eneo, baada ya miaka kadhaa wanadai hapo ni kwao kwa kuwa wamezaliwa hapo.

Inakuja hiyo?

Iwe miaka 3000 au 1000 nyuma hakujawahi kuwa na nchI ya wayahudi wala inayoitwa Usrael.

Vipi imani ya kiroho iwe na nchi?
Umeandika kwa hasira sana.
Kumbuka, hata taifa la wapalestina halikuwahi kuwepo. Pia Wayahudi hawakuwa wakimbizi pale. Hawakupelekwa na mtu, ni kwao, wapalestina pia ni kwao.
 
Hivi wakatoliki wa peramiho leo hii wakisema wanaanzisha nchi yao hapo peramiho kwa kuwa wapo 100% wakatoliki na eneo hilo walipewa na Wajerumani walipokuwa wanatawala kimabavu basi ndiyo imeshakuwa sawa hivyo?
 
Hivi wakatoliki wa peramiho leo hii wakisema wanaanzisha nchi yao hapo peramiho kwa kuwa wapo 100% wakatoliki na eneo hilo walipewa na Wajerumani walipokuwa wanatawala kimabavu basi ndiyo imeshakuwa sawa hivyo?
Mfano wako ni irrelevant, nakupa nafasi ujaribu mfano mwingine.
Labda jaribisha mfano wa Wamasai na waarabu kule Ngorongoro.
Au jaribu mfano wa Watusi na Wahutu.
 
Watu wanapotosha sana.
Wafilisti walikuwepo enzi na enzi zaidi ya miaka 500 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Enzi za Ibrahimu,
MImi ni Mkristo.
Ukweli ni kwamba Wafilisti ndio
Wakaazi wa kwanza pale Kanaan/Israel.

Ona
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.

Mwanzo 10:14
Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.

Mwanzo 21:32
Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Mwanzo 21:34
Hiyo nchi walikaa wacaanani wewe na wanefili na agizo la Mungu waangamizwe wote Na ndicho kilichotokea chief. Caanani alikuwa na laana ya baba yake Nuhu kwa kumchungulia akiwa amelewa. Na wanefili walikuwa na mijitu makubwa sana breed ya Malaika na binadamu. Kuna malaika waliwaingilia binadamu ikatokea breed moja hatari sana. Na hao malaika wapo vifungoni wakisubir hukumu. Haya Mambo yapo kiroho sana kuyaelewa.
 
Hiyo nchi walikaa wacaanani wewe na wanefili na agizo la Mungu waangamizwe wote Na ndicho kilichotokea chief. Caanani alikuwa na laana ya baba yake Nuhu kwa kumchungulia akiwa amelewa. Na wanefili walikuwa na mijitu makubwa sana breed ya Malaika na binadamu. Kuna malaika waliwaingilia binadamu ikatokea breed moja hatari sana. Na hao malaika wapo vifungoni wakisubir hukumu. Haya Mambo yapo kiroho sana kuyaelewa.
Ninaweza kukupa maandiko yote.
Kanaani walikaa mataifa/makabila zaidi ya 5.
Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi.

Mwanzo 13:7
Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu.

Mwanzo 34:30
MATAIFA/MAKABILA YALIYOKAA KAANANI
Itakuwa hapo Bwana atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu.

Kutoka 13:5
 
Back
Top Bottom