Ponda: Serikali haiwezi kunifunga mdomo

chuki binafsi hazisaidiiiiiii

Hakuna chuki bali ni kutaka ufafanuzi tu...........simjui Ponda wala Lipumba....hapa tunajadili hoja na sio watu

Kwa VIDEO, tembelea

VIDEO: Prof. Lipumba akiri kumsaidia Rais Kikwete katika Uchaguzi 2010





LIPUMBA AIBUA JAMBO ZITO - AKIRI KUMNUSURU KIKWETE UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na "kumnusuru" Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita.

Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa.

Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa kiimani, Profesa Lipumba alianza kwa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, na ushindani mkali wa kisiasa uliokuwapo.

Alisema hawaoni matunda ya jitihada walizofanya kumnusuru Rais Kikwete asishindwe, kwani hata chini ya uongozi wake, Waislamu wameendelea kutothaminiwa.

"Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi. Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo katika mtihani mgumu zaidi," alisema.

Katika hali ambayo inasemekana ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana kwa mbinu, huku wengine wakiituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ilimnusuru mgombea wa CCM, kauli hii ya Profesa Lipumba inadokeza kwamba anajua mkakati zaidi wa kazi ya Tume ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema "wenzetu wameanza kujipanga" kuelekea 2015.

"Kwahiyo kama Waislamu tunataka kupata haki zetu, kama tunataka kuishi kama raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu, lazima tujipange kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga kwa sababu wenzetu wameanza kujipanga, vinginevyo tutaendelea kubaki maskini na raia wa daraja la nne katika nchi yetu wenyewe.

"Mwaka 2010 wakati mshindi wa uchaguzi wa rais alipotangazwa, mimi nilikwenda kwenye hafla ya kutangazwa matokeo, na nilikwenda makusudi tu, siyo kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila nilikwenda makusudi kwa kujua hali ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo.

"Huku nilikutana na Sheikh Basaleh. Nilipokutana naye, alinipongeza; sijui kama yeye anakumbuka, akaniambia ‘umeweka mbele imani yako na umekuwa mwelewa wa mambo.'"

Hata hivyo, licha ya Profesa Lipumba kuwaambia Waislamu wajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu, hakusema wajipange kupitia chama kipi.

Lakini alisisitiza kwamba uchaguzi ujao ni zaidi ya siasa au rais yupi anafaa, bali maslahi, hasa ya rasilimali nyeti zinazopatikana katika ukanda wa Pwani ya Mashariki, eneo ambalo alisema linakaliwa zaidi na watu wenye imani ya Kiislamu.

Katika moja ya kauli zake, Profesa Lipumba alisema kwamba kuna chama kimoja kinataka kuchukua madaraka ya nchi, lakini kinasaidiwa na mataifa ya magharibi, yasiyoenzi wala kuthamini imani ya Kiislamu.

Kwa muda sasa, zimekuwapo tetesi kwamba CCM imekuwa inafanya siasa za udini dhidi ya vyama vya upinzani, hasa inapoona maslahi yake yapo hatarini.

Mwaka 2010 makada kadhaa wa CCM walitumia mitandao ya simu kuchonga (spoofing) ujumbe wa simu ulioshambulia mgombea mmoja wa upinzani, ukimhusisha na imani yake.

Kauli ya Lipumba imethibitisha pia minong'ono iliyokuwapo muda mrefu kuwa baadhi ya kura za Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais Kikwete.

Katika uchaguzi huo, Lipumba alitangazwa kushika namba ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.

Alipoulizwa kuhusu ziara yake msikitini na kauli aliyotoa, Profesa Lipumba alikiri kwamba alikwenda kuzungumzia hali ya kisiasa nchini.



CHANZO: Tanzania Daima - Mei 26, 2013
 
Hata makaburu walimwambia mandela ni mchochezi sishangai kwa ponda
 
Dah!..

Nilikuwa sijui lakini kwa hayo maelezo ni wazi Allah ni mungu wa waislamu na sasa ninaamini Waislam wanamungu wao siye

Mungu ninayemjua mimi Muumbaji wa Mbingu na nchi!...

Allah is not equal to God(Mungu).

Sh Ponda usitetereke.....simama imara hakuna mwenye uwezo wa kukuziba mdomo......sana sana watakueka Jela na hiyo kwa Waislam ni University llah Yusuf.....kingine labda wakuhamishe mji na hiyo kwa Waislam ni Hijra Fii Sabilillah...jambo la mwisho ambalo wataeza kukufanyia ni kuuua na kukupa tiket ya Jannat,,....raha gan ilioje Muislam kuuawa na Kafir....,,ivyo bac Muislam hana hasara yoyote ile..,,wafanye watakayofanya ila wajue kua ndo wanakupandisha darja mbele ya Allah SW..,,Jazaka llah kheir Sh Ponda our Muslim Fighter
 
amiiiiin,,nawe pia Allah SW akulinde Dunian na Akhera..unajua Qur an kamwe haikosei..,,Allah SW ashasema chuki zao juu ya Waislam ni kubwa sana kuliko wanayoyadhihirisha kwenye vinywa vyao..,,ivo bac tuzid kumuomba Allah SW atulinde na hila zao.......(Hamtopata Pepo mpaka muyapate waliyoyapata waliokua kabla yenu),,...!!

Kweli kabisa mwenyezi amesema hawatowaacha hao mayahudi na manaswara mpake mfuate mila zao na wanawahofia waislam kuliko wanavyomuogopa mwenyezi mungu.
 
Huyu ni Ponda si ni MFUNGWA WA NJE na yuko chini ya UANGALIZI?Haya ndiyo madhara ya kupindisha sheria ili kumfurahisha mtu fulani. Huyu Ponda alitakiwa awe BEHIND BARS sio kifungo cha nje!

Sheria uijuayo wewe kwa muislaam ni kufungwa jela tu? au anyamaze, pole.
 
Ponda kazi yako ni nzuri sana cha msingi simamia katika sheria za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu.
Serikali inapaswa kuwa fair na kuacha wanaharakati wafanye kazi za kutetea maslahi yao na wala msilete habari za kuwabambia kesi ili kuwafumba midomo mtakuwa mnaharibu zaidi.
Ukweli una nguvu daima na kamwe hauwezi kushindwa,sema tu haki inachelewaga kupatikana ni vyema kusikiliza madai ya waislamu kuliko kujitia pamba masikio na kuwashughulikia wale wapigania haki kwani kwa mrengo mnazidi ongeza imani kwa vijana wengine kuamua kumtumikia mungu wao kwa kupigania maslahi ya watu wao.
 
Mods kuna watu wanaleta thread za uchonganishi,mtu kaleta thread ya Ponda alafu anachomekea Chadema,watu kama hawa wapigwe ban na sio wanaotukana tu..
 
Sh Ponda usitetereke.....simama imara hakuna mwenye uwezo wa kukuziba mdomo......sana sana watakueka Jela na hiyo kwa Waislam ni University llah Yusuf.....kingine labda wakuhamishe mji na hiyo kwa Waislam ni Hijra Fii Sabilillah...jambo la mwisho ambalo wataeza kukufanyia ni kuuua na kukupa tiket ya Jannat,,....raha gan ilioje Muislam kuuawa na Kafir....,,ivyo bac Muislam hana hasara yoyote ile..,,wafanye watakayofanya ila wajue kua ndo wanakupandisha darja mbele ya Allah SW..,,Jazaka llah kheir Sh Ponda our Muslim Fighter
Ndugu kama kufanya hivyo ni suna mbona wewe hujitokezi ukafanya hivyo? unamsukumizia mwenzio afanye wakati wewe uko nyumbani kwako unakula bata na wanao, nenda kajitokeze na wewe, nyinyi ndo wale mnawapa wenzenu wavae mabomu alafu mko kwambali mnasikilizia, acha hizo wewe kwani nani hapendi ubwabwa.
 
Nadhani siku moja atakipata anachokitaka huwezi kushindana na serikali.

Acha kutisha watu, serikali haina haki yoyote ya kikatiba kukandamiza mawazo yatu. Namna Pekee ya Kukabiliana nae ni kuja na hoja mbadala kama ni serikali kweli inawajibika kumjibu.
 
Bandiko lako la kwanza lilifutwa, umekuja tena na bandiko lile lile....unataka ban?
Mkuu uyu jamaa hajakaa kichama bali kidin,kaleta thread ya Zitto hana jipya zaidi ya udini wake,watu kama hawa hatari sana.
 
Ponda si mfia dini kama anavyotaka ajulikane, ukweli ni kwamba Ponda ni mganga njaa kupitia mgongo wa dini, lakini yupo anayempa kibri naye si mwingine ni jk kwa kuwa ameingia ikulu kwa mgongo wa uislam kama Lipumba alivyotoboa siri, anachotafuta Ponda ni kuitwa na kupelewa fungu kwa kelele zake.
 
Akizungumza kwenye kongamano lililofanyika diomond jubilee shehe ponda ameitahadharisha serikali kutaka kumfunga mdomo asizumze juu ya masuala ya dini ambapo hiyo ni haki kikatiba na yeye kama raia wa tanzania anapaswa kuheshimiwa.source majira na mtanzania

mwambie... masikio hayapiti kichwa, yakipita kichwa basi ngiri huyo!!!

he will get what he deserves
 
Back
Top Bottom