Polisi yapiga marufuku kuuza visu, sime, mapanga barabarani ili kupunguza matukio ya watu kujiua

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141

Polisi yapiga marufuku kuuza visu, sime, mapanga barabarani ili kupunguza matukio ya watu kujiua kwa wivu wa mapenzi

1.gif

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imepiga marufuku biashara ya kutembeza visu, sime na mapanga barabarani na kusema yeyote atakayekiuka agizo hilo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema jeshi hilo lipo katika mchakato wa kupendekeza sheria mpya ya matumizi ya silaha na umiliki ili kudhibiti matumizi mabaya yakiwamo uuzaji wa visu, mapanga na sime kiholela.

Kamishna Kova alisema tatizo kubwa si mtu kumiliki silaha, bali jinsi watu wanavyozitumia vibaya na kusababisha madhara katika jamii na kuongeza kuwa sheria hiyo itajumuisha uuzaji holela wa visu, mapanga na sime barabarani na umiliki wa silaha za moto.

“Kwa mfano visu, kwa kawaida vinatumiwa nyumbani kukatia nyanya na vitunguu, lakini mtu anaweza kukitumia vibaya kwa kumchoma nacho mtu tumboni au kifuani...hivyo atakayeonekana anauza vitu hivyo, atachukuliwa hatua.

Hatua hiyo imekuja baada ya mfululizo wa mauaji ya kutumia silaha za moto yanayohusishwa na wivu wa mapenzi kukithiri nchini.

Novemba 19, mwaka huu, Gabriel Munisi aliwaua watu wawili kwa risasi na kumjeruhi mpenzi wake, Christina Newa, mama mzazi wa mpenzi wake, Ellen Eliezer na kisha kujiua, kwa kile kinachoaminika kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mapema Oktoba mwaka huu, Mwandishi wa Habari wa Kituo cha ITV, Ufoo Saro alijeruhiwa pia kwa risasi na mpenzi wake, Anthery Mushi. Pia alimuua mama mzazi wa Ufoo na kisha kujiua kwa kujipiga risasi.

Kamishna Kova alisema pia kuwa katika mchakato huo wa kuunda sheria mpya za umiliki wa silaha, hatua kali ikiwamo kunyang’anywa silaha hizo kwa watu wanaozitumia vibaya itachukuliwa.

Hata hivyo, alisema wakati sheria hizo zikisubiriwa, polisi watawachukulia hatua kali wote watakaobainika kuzitumia vibaya. Aliwataka Watanzania kuwa makini na matukio ya uhalifu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka na sikukuu.

Mzee
Kamishna Suleiman Kova Umfanya jambo la maana sana maana watu wamekuwa wajinga sana wanauana kama kuku kwa sababu za ujinga wa wivu. Ahhh sijapata kuona upumbavu kama

huu tangu nizaliwe mpaka umri wangu nilionao vijana wa siku hizi wanauwana eti kwa sababu ya wivu wa kimapenzi? Kama mpenzi wako hakutaki tafuta mpenzi mwengine wako wengi mbona.

wanawake wazuri wapo wengi na wanaum wazuri wapo wengi yanini kupigan Risasi na visu kulikoni? Ni ulimbukeni wa mapenzi huo jamani tuache ujinga huu jamani.

Kova hujitambui.. Kwa matukio hayo ulioanisha.. Ni lipi limetumia Judy au panga,, jipange" acha kukurupuka na kuwa msemaji wa kila kitu.. Kwani wewe ndo msemaji wa kila kitu ? Au unapenda media? Mrekebisheni huyu jamaa..
 
Polisi yapiga marufuku kuuza visu, sime, mapanga barabarani ili kupunguza matukio ya watu kujiua kwa wivu wa mapenzi

1.gif

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imepiga marufuku biashara ya kutembeza visu, sime na mapanga barabarani na kusema yeyote atakayekiuka agizo hilo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema jeshi hilo lipo katika mchakato wa kupendekeza sheria mpya ya matumizi ya silaha na umiliki ili kudhibiti matumizi mabaya yakiwamo uuzaji wa visu, mapanga na sime kiholela.

Kamishna Kova alisema tatizo kubwa si mtu kumiliki silaha, bali jinsi watu wanavyozitumia vibaya na kusababisha madhara katika jamii na kuongeza kuwa sheria hiyo itajumuisha uuzaji holela wa visu, mapanga na sime barabarani na umiliki wa silaha za moto.

"Kwa mfano visu, kwa kawaida vinatumiwa nyumbani kukatia nyanya na vitunguu, lakini mtu anaweza kukitumia vibaya kwa kumchoma nacho mtu tumboni au kifuani...hivyo atakayeonekana anauza vitu hivyo, atachukuliwa hatua.

Hatua hiyo imekuja baada ya mfululizo wa mauaji ya kutumia silaha za moto yanayohusishwa na wivu wa mapenzi kukithiri nchini.

Novemba 19, mwaka huu, Gabriel Munisi aliwaua watu wawili kwa risasi na kumjeruhi mpenzi wake, Christina Newa, mama mzazi wa mpenzi wake, Ellen Eliezer na kisha kujiua, kwa kile kinachoaminika kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mapema Oktoba mwaka huu, Mwandishi wa Habari wa Kituo cha ITV, Ufoo Saro alijeruhiwa pia kwa risasi na mpenzi wake, Anthery Mushi. Pia alimuua mama mzazi wa Ufoo na kisha kujiua kwa kujipiga risasi.

Kamishna Kova alisema pia kuwa katika mchakato huo wa kuunda sheria mpya za umiliki wa silaha, hatua kali ikiwamo kunyang'anywa silaha hizo kwa watu wanaozitumia vibaya itachukuliwa.

Hata hivyo, alisema wakati sheria hizo zikisubiriwa, polisi watawachukulia hatua kali wote watakaobainika kuzitumia vibaya. Aliwataka Watanzania kuwa makini na matukio ya uhalifu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka na sikukuu.

Mzee
Kamishna Suleiman Kova Umfanya jambo la maana sana maana watu wamekuwa wajinga sana wanauana kama kuku kwa sababu za ujinga wa wivu. Ahhh sijapata kuona upumbavu kama

huu tangu nizaliwe mpaka umri wangu nilionao vijana wa siku hizi wanauwana eti kwa sababu ya wivu wa kimapenzi? Kama mpenzi wako hakutaki tafuta mpenzi mwengine wako wengi mbona.

wanawake wazuri wapo wengi na wanaum wazuri wapo wengi yanini kupigan Risasi na visu kulikoni? Ni ulimbukeni wa mapenzi huo jamani tuache ujinga huu jamani.

jamani kuna mtu anaweza kunitupia cv ya kova hapa?kwani vikiuzwa madukani ndio havita tumika kwenye matukio?mbona tindikali haiuzwi madukani lakini ina matukio kibao?hata kova asemeje kuhusu silaha za moto,ukiwa na hela lazima utaimiliki tu,hakuna wa kukuzuia
 
Kova hamnazo kabisa badala ya kupiga marufuku bastola,yeye anapiga marufuku mapanga kwa kuua Dr.mvungi au?na kwenye maduka,sokoni jee kama mtu anataka si atanunua huko?
 
Mbona kila mwaka kukitokea Yukio wanarudia yaleyAle?
 
Vichekesho kweli mbona hakupiga marufuku wakati ujambazi unashamiri anapiga marufuku nw? Kweli hii nchi cjui inaenda wap
 
Nahisi amesahau kujumuisha na jembe pia ni silaha.

akikukamata...!
hata mawe yatapigwa marufuku kuonekana hovyo mitaani.
yeyote atakayeonwa amekaa kando ya jiwe atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Atatakiwa atueleze,kwanin yupo karibu na jiwe hilo,au ana mpango gani na hilo jiwe.
Haaa haaa haaaaaaaa!
 
Sijui itakuwaje mkuu tyta! Watu wanauana kwa kupigana risasi wao wanakataza mapanga!
 
Hongera Kova.maana mpo bar mtu ana sime zaidi ya 20 anapita anauza.ni hatari sana
 
Siwezi kumlaumu uwezo wake umeishia hapa, hivi mtu akitaka kujiua atakosa kisu kweli na hao wanaojiua visu wamevipata kwa njia hizo?
 
akikukamata...!
hata mawe yatapigwa marufuku kuonekana hovyo mitaani.
yeyote atakayeonwa amekaa kando ya jiwe atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Atatakiwa atueleze,kwanin yupo karibu na jiwe hilo,au ana mpango gani na hilo jiwe.
Haaa haaa haaaaaaaa!

hapo ndio vijiti vya meno vitatawala kulia chips kuanzia mtaani mpaka mahotelini :smile-big: maana uma nao ni silaha
 
Kwani hata dukani mbona zitanunuliwa au kutahitajika kibali cha RPC kama silaha za moto?
 
pamoja na kuwa wahalifu wanatumia silaha za moto,

Heri wapige marufuku kuuza mapanga na visu

Imagine upo kwenye foleni mtu anakugongea dirishani na panga limenolewa pande zote mbili
 
Back
Top Bottom