POLISI WETU: Ukiwaona Ditopile Mzuzuri v. Lulu na ubaguzi wa madaraja...

Aliyenitangulia ameandika mengi ambayo yalikuwa ya mtazamo wangu.Ninachotaka kuwakumbusha wadau ni kwamba sheria inataka mtuhumiwa kupelekwa mahakamani baada au ndani ya masaa 48 baada ya mtuhumiwa kukamatwa.
Pale mtuhumiwa anaposomewa mashitaka, kama sio ya mauaji ,basi mtuhumiwa ataulizwa kama anakubali au kukataa mashitaka yanayomkabili.Haitajalisha kama upelelezi umekamilika au haujakamalika.
Kwa kesi za mauaji ,mahakama ya hakimu mkazi haina uwezo wa kisheria wa kutoa dhamana au kumtaka mtuhumiwa ajibu mashitaka.Mahakama yenye ewezo huo ni mahakama kuu.
Ndivyo ilivyo kwa Lulu .UKISOMA VIZURI MASHITAKA ya Lulu hashitakiwi kwa kuumua Kanumb ANACHITAKIWA KUHUSIANA NA KIFO CHA kANUMBA.
 
Back
Top Bottom