POLISI WETU: Ukiwaona Ditopile Mzuzuri v. Lulu na ubaguzi wa madaraja...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Mheshimiwa Ukiwaona Ditopile Mzuzuri alipiga risasi na kuua mchana kweupe polisi walipoona aliyeuawa ni kijana kapurwa kwa maana ya kipato cha chini walimbadilishia Mheshimiwa Ukiwaona Ditopile Mzuzuri hati ya mashitaka kutoka mauaji na kuwa manslaughter....au mauaji bila ya kukusudia...

Lakini huyu binti Lulu wanaona hii sasa ni murder... Mtoto wa mlalahoi sasa anabebeshwa zigo zito na DDP bila ya hata ushahidi wa kufanya hivyo...

Jeshi letu ni Jeshi la kulinda viongozi na kulinda mabwanyenye na linapozungumzia polisi shirikishi ni kutushirikisha katika kukubali uonevu kama huu...

Hali hii yaweza kumtokea mtu yeyote kati yetu. Tuanze kupambana na ubaguzi tunaofanyiwa na hawa polisi ambao waweza kuwa chanzo cha machafuko........
 
Ndugu yangu,
Suala la Lulu inaumiza sana, na yule mtoto sijui kwanini wanamfungulia murder kesi wkt hana nguvu za kumpiga marehemu Kanumba? Inauma sana huyu mtoto kwa makubwa yanayomkuta. Lulu anahitaji msaada mkubwa sana hasa wa KISAIKOLOJIA.
 
hana maana kwani si mfano ktk jamii ya wastaarabu. Anafaa kutumikia adhabu ya kufungwa maisha!
 
Police wamefata upepo wa msiba wakajua kwa kufanya kwao hivyo wataonekana watendaji kazi.

sehemu ilipotokea tukio awakufanya uchunguzi wa kutosha kwakuwa ndipo palikuwepo msiba.
 
Ndugu yangu,
Suala la Lulu inaumiza sana, na yule mtoto sijui kwanini wanamfungulia murder kesi wkt hana nguvu za kumpiga marehemu Kanumba? Inauma sana huyu mtoto kwa makubwa yanayomkuta. Lulu anahitaji msaada mkubwa sana hasa wa KISAIKOLOJIA.

ni kweli. akini chanzo ni polisi wetu wana matatizo ya kutubagua kwa madaraja ya kiuchumi..........
 
Msiendeshwe na hisia lulu anausika sana na kifo cha sk

na Ukiwaona Ditopile mzuzuri ambaye alirudi kwenye gari yake akachukua bastola na kuvunja kioo cha daladala na kumpiga risasi dereva yeye alikuwa hahusiki na mauaji yale................................yaelekea yaliyofanyika chumbani mwa mwendazake wewe ulikuwemo ukishuhudia na kubaini unayotuelezea sasa
 
Police wamefata upepo wa msiba wakajua kwa kufanya kwao hivyo wataonekana watendaji kazi.

sehemu ilipotokea tukio awakufanya uchunguzi wa kutosha kwakuwa ndipo palikuwepo msiba.

ni kweli kabisa....wanafanyakazi kwa kufuata upepo badala ya maadili ya kazi yao.........
 
Hii nchi ilivyo sasa inaendeshwa kama mpira wa England unavyokwenda...kwa luninga. Lulu ana umri mdogo na kwa kweli she has to be very tought to come out strong and capable of progressing well with life. Her life, if not well thought, could as well be on the brink of collapsing for good.
 
tunaujua ushahidi waliokusanya polisi au tunaropoka tu!!

faili linasema uya kuwa mwendazake amekufa kwa mshutuko uliomeletea brain concussion na kufanya viungo vyote mwilini vishindwe kufanya kazi. Hana jeraha lolote mwilini la kujeruhiwa........................lakini Mzuzuri alimtoa roho kwa risasi dereva wa daladala................mchana kweupe na huhitaji ushahidi wowote ule........................lakini polisi wakasema ni mauaji ya kutokusudia huyu binti ambaye anasafishwa na kila mtu kuwa hakuwa na silaha na ndiye aliyeripoti kudhoofu kwa afya ya marehemu sasa aonekana ni muuaji................hii nchi inatisha kwa dhuluma........
 
umelisoma faili?Acha sheria ifanye kazi.SHERIA NA MSUMENO

sheria ya nchi inamlinda mwenye nacho kwa hiyoitafanya kazi ya kuendeleza dhuluma................hilo tuna uhakika nalo lakini siyo kutenda haki................mbona huongelei lolotte kuhusu ya mzuzuri kama sheria ilifuata mkondo wake?
 
faili linasema uya kuwa mwendazake amekufa kwa mshutuko uliomeletea brain concussion na kufanya viungo vyote mwilini vishindwe kufanya kazi. Hana jeraha lolote mwilini la kujeruhiwa........................lakini Mzuzuri alimtoa roho kwa risasi dereva wa daladala................mchana kweupe na huhitaji ushahidi wowote ule........................lakini polisi wakasema ni mauaji ya kutokusudia huyu binti ambaye anasafishwa na kila mtu kuwa hakuwa na silaha na ndiye aliyeripoti kudhoofu kwa afya ya marehemu sasa aonekana ni muuaji................hii nchi inatisha kwa dhuluma........

hayo umeyapata kwenye media.media na polisi sio ofisi moja.
 
Juzi kuna hukumu ya watoto wa miaka 13 wameua mtoto wa miaka 2 sababu ya kulipa kisasi kwa kuwa kaka yake marehemu alichukua gololi zao......wamefungwa miaka 6
 
Mimi sio mwanasheria ili ninachojua Polisi hawana uwezo wa kubadilisha kesi kutoka murder mpaka manslaughter, ni mahakama kuu peke yake yenye uwezo wa kufanya tena baada ya ushahidi mzito kutolewa na mashahidi. Inaweza ikachukua hata mwaka au zaidi ya mwaka kuthibitisha hili kwa mahakama zetu. Polisi wapo sahihi kabisa kupeleka mahakamani kesi hiyo kama hilo, kama ni murder case au manslaughter ni mahakama kuu ndio itatoa uamuzi, kama ana kesi ya kujibu au hana ni mahakama kuu ndio itajua.

Kesi ya Ditopile hukuifuatilia ndio maana maana umekuja kwa kushutumu tu bila kufanya uchunguzi wa ile kesi. Kama utakumbuka Ditoplie alisota zaidi ya mwaka mmoja segerea au ukonga lakini alikuja kutoka baada ya kesi kutoka kuwa murder na kuwa manslaugther lakini bado akawa ana kesi ya kujibu. Mpaka Ditopile anakufa alikuwa ana kesi ya kujibu tena ni manslaughter.Kesi ya aina hii mtu sio lazima asweke mahabusu kwa muda mrefu.

Lulu naye lazima apitie njia hii, hana njia ya kuepuka. Sasa kama ana kesi ya kujibu au hana, ni mahakama ndio itajua baada ya kujiridhisha na ushahidi ulioupata , kama ni murder au manslaughter ni mahakama kuu hiyo hiyo ndio itajua.

Kesi kama hiyo ilimkumba Zombe na wanzake, walisota sana lakini mwishowe kuna baadhi yao waliachiwa na mahakama kuu baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu ILA ZOMBE NA WALIOBAKI WALIAMBIWA WANA KESI YA KUJIBU TENA NA MURDER KESI, Mwishowe Zombe na wenzake walikuja kuachiwa baada ya kuonekana alioua hayupo. Polisi ikaambiwa imatfute Muuaji

Narudia tena mimi sio Mwanasheria ila nilichogundua Sheria haifuati mapenzi yetu sisi na vyombo vya habari. Sisi ni wapesi sana kuhukumu lakini Mahakama haina hayo .

MWSHO;Lulu ana ksei ya kujibu, in mahakama kuu tu ndio itaamua tofauti

USHAURI: Tujifunze kufuatilia mambo kwa undani ili kuepeusha Jamii Forums kuonekana sehemu ya kuzusha mambo
 
Back
Top Bottom