Polisi wetu ni wana CCM?

Nimefedheheshwa na kitendo cha kiongozi wa juu wa jeshi la polisi kutangaza nia zao za ubunge kwa tiketi ya CCM.

Tibaigana, na jana nikachoka kusikia kamanda wa trafiki Kombe.

Hivi hawa walijiunga na chama lini au walikuwa na rangi ya kijani mfukoni? Muda waliostaafu awajapata uzoefu wa siasa hizo.


source: Kamanda Kombe kuwania ubunge Vunjo

Rule no 1 kama wewe ni mfanyakazi wa serikali na unaingia kwenye chama jiengue kwanza serikalini na ndio uje kwenye chama.

Sasa nataka kuuliza kombe still ni police na kama ndio aachane na upolice kwanza na ndio ajiunge CCM,

Na kama alisha staaafu upolice ni lini alijiunga CCM?
kwani inastahajabisha sana mapema tu anatangaza nia na ni majuzi tuu alikuwa kamanda wa Trafiki nadhani kama sijakosea iweje leo wananchi wa eneo husika ati wamekuomba ugombeee?

Kwa Tibaigana naweza kidooogo nae nika muhoji Uzoefu wake kwenye siasa ni wa muda gani? na ni lini nae alikuwa/kajiunga kwa chama "CCM"? maana nimekuwa na watoto wake na wameoa nao, nasija wahi mwona Tiba kwenye Siasa Tokea naanza mfaahamu huko msoma, Singinda, Tanga, Dodoma na hapa Dar?

 
Makamanda wote wa vyombo vya ulinzi ni wanachama,washabiki na wapenzi wakubwa wa CCM. Tukumbuke kuwa hawa ndiyo vitendea kazi vya CCM katika kuwadhibit wapinazani.Kule Pemba mwaka 2001 walioua wanachma wa CUF si polisi hawa hawa? Hivyo wanapostaafu lazima wapozwe kwa kuingizwa kwenye ulaji kwa kofia ya siasa.
 
Jambo la msingi hapa ni kuona jinsi wastaafu hao wasivyo waadilifu na pia kukosa haya katika jamii. wangesubiri kidogo kuthibitisha kwamba wameanza kujihusisha na siasa baada ya kustaafu kwa kuwa lazima wajipange.
Kulingana na maadili ya kazi zao, walitakiwa wasijihusishe na siasa, lakini leo tunawaona wakitangaza nia za kugombea muda mfupi tu baada ya kustaafu.
Huo ni uthibitisho kwamba walikuwa wakijihusisha na siasa wakiwa ofisini, hivyo siyo waadilifu na ni sababu tosha ya kutoa pingamizi ndani ya chama wanachotangazia nia na pia kama wakipitishwa pingamizi litolewe kwenye tume.
Naamini maamuzi yasyo ya kinafiki yatawaondoa, labda itashindikana tu kama walipokuwa ofisini viongozi watoa maamuzi walikuwa wanapata maslahi binafsi toka kwao na hivyo kuwalipa fadhila!
Nawashauri washindani wao wajiandae kwa mapingamizi kwa hoja ndani ya vyama na kwenye tume hata kama watafanyiwa mizengwe lakini watakuwa wametoa somo kwa wengine.
 
jamani hapa shida Yangu ni hii, Jeshi la wananchi wa Tanzania linasema, Kiongozi kuanzia meja na kuendelea, akistaafu ni lazima akaee not less than 2 good years without involvement in politics. Nadhani inaweza kuwa hivyo kwa polisi(sina hakika). Ila hapo lazima watakuwa makada na kutimiza malengo ya chama chao wakiwa kazini.
 
.
Balantanda, Wajeshi, Polisi, Wanausalama na Waserikali, hawaruhusiwi kujishughulisha na siasa wakiwa katika nyadhifa zao, ila haki zingine zote zakiraia wanazo kama raia wengine wowote ikiwemo haki ya kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila wasishabikie siasa, hivyo hizi taarifa za mjeshi fulani, polisi fulani au mserikali fulani kuwa kada wa chama akiwa kwenye utumishi wa umma, morally its wrong ila practically ndio watu wa kupongezwa na kupewa ulaji zaidi na zaidi kwa vile ni makada wa chama tawala.

The deviding line kwenye conflict of interest btn their political affiliation and duty of care is very thin, ndio maana Mahita, Ex-Darasa la 8 akiwa RPC Moshi, alimvurumishia mabomu Mrema bila huruma, akaonekana amefanya kazi mzuri, akapewa U IGP, hata kwa kumwangalia tuu machoni, utatambua wazi, thinking capacity yake ni sero flani kama kina Makamba type.

Sasa hawa wakuu baada ya kustaafu utumishi wa umma, wanahaki kushiriki shughuli za kisiasa kama raia wengine, ndio maana uliwaona kina Maj.Gen. Jesse Makundi, ulimsikia Mboma, Afande Tibaigana etc, ni haki yao.
Pasco asante sana kwa kutuweka sawa kuhusu hili. Nimekuelewa vizuri lakini si unaona umuhimu wa sheria hizi haupo? Imewekwa kama kiini macho. Nadhani unaelewa ninamaanisha nini maana ukiangalia kuna sababu nyingi za kuniaminisha hivyo.
 
.
Mzee Mwanakijiji, huku kutakuwa ni ukwiukwaji wa haki za binaadamu, ila kwa mtu mwenye akili timamu, kuna issue ya moral resiponsibility kwa jamii uliyoitumikia, binafsi naona ni kujiaibisha na kujidhalilisha, leo Mbona achukue fomu, Apson nae achukue, Mahita pia achukue, kwa kujiaminisha na utumishi wao uliotukuka ndani ya serikali, wanajifariji walifanya kazi nzuri, lakini chama kinaweza kuwagomea kuwapitisha kwa vile sio popula, hii si ni aibu ya mwaka!.

Nadhani hawa makamanda, tuwaache wajistaafie tuu kwa heshima.


...Tatizo ni wao wenyewe sio sisi. Sentensi yako ilipaswa kuwa...'wajistaafie wenyewe kwa heshima'! (Ondoa hiyo 'tuwaachie'! Sisi hatuhusiki na maamuzi yao!)
 
Back
Top Bottom