Polisi mkoani DODOMA leo wamebatilisha kibali cha kufanya mkutano wa hadhara wa chama cha democrasia na maendeleo-CHADEMA.Mkutano huo ulikuwa ufanyike katika kata ya Chang'ombe eneo la standi kwa madhumuni ya kujenga na kukiimarisha chama katika kata hiyo.Mkutano huu ulikuwa ufanyike wiki iliyopita lakini ikashindikana kutokana na CCM kuwa na mkutano siku hiyo katika kiwanja hicho ndipo polisi waliwataka CHADEMA kuchagua siku nyingine ambapo CHADEMA walikubaliana na polisi kufanya mkutano huo siku ya leo.Kisheria polisi wanatakiwa kubatilisha kibali cha mkutano saa arobaini na nane kabla ya mkutano.Hakukuwa na sababu za msingi kutoka polisi.Licha ya mkutano kuvunjwa wakazi wa kata hii ya chang'ombe walikuwa na shauku kubwa ya kuwasikiliza viongozi wa CHADEMA kwani walimiminika kwa wingi kitu ambacho sio cha kawaida kwa mkoa wa DODOMA kwani ni ngome kubwa ya CCM.Kimsingi hii ni njia ya kukadhamiza democrasia kwa vyama vya upinzani kwa kukilinda chama Tawala CCM.Naomba kuwasilisha.source nipo DODOMA.