Polisi watoa elimu na kuchangia damu katika Siku 16 za Kupinga Vitendo vya Ukatili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
0efe4ea6-889d-4ab6-86d1-8687f1d8a550.jpg

Jeshi la Polisi Wilaya ya Longido limeendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia makundi mbalimbali ya jamii za kifugaji huku wakitumia siku 16 za kupinga vitendo hivyo kuchangia damu katika kituo cha Afya Longido.

Akiongea mara baada ya zoezi hilo Mkuu wa Polisi wilaya ya Longido Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Leah Ncheyeki amesema kuwa wilaya hiyo kiasili ni jamii ya kifugaji ambayo imekuwa ikiendelea kuziishi tamaduni ambazo baadhi zimekuwa zikiwanyima fursa hususani watoto wakike wa jamii za kifugaji.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi wilaya hiyo kupitia siku kumi na sita za kupinga ukatili waliona vyema waendelee kutoa elimu kwa jamii hizo za kifugaji ili kuachana na tamaduni ambazo hazina tija kipindi hiki cha mabadiliko ya dunia.
b7c2f1e7-cd8c-47de-b99e-ad1bf6362d4d.jpg

c0b11102-a218-49ee-bafe-e308dd159292.jpg

Aidha amebainisha kuwa wataendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii hizo za kifugaji ili waondokane na vitendo hivyo vinavyowanyima fursa ya kufanya maamuzi.

Kwa upande wake kaimu afisa Tarafa Longido Enna Mtera licha ya kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha mpango wa Polisi kata ambao umesaidia sana kutoa elimu na kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii hiyo amesema jamii hiyo imekuwa ikiendekeza mila ambazo zinamnyima haki mwanamke na watoto kwa kufanya maamuzi huku akiwaomba Jeshi hilo waendele kutoa elimu zaidi ili kuikomboa jamii hiyo na mila Potofu.
2604f7aa-7b67-4c6a-8eb1-3464b2e2fa4e.jpg

dbbe5a48-b83b-4462-be65-240888fdbf01.jpg
 
Back
Top Bottom