Polisi wanne mbaroni kwa mauaji ya raia Songea:IGP MWEMA APELEKA KIKOSI CHA UCHUNGUZI

Sidhani kama tume ya chagonja itakuja na jipya, sana sana inaenda kujipatia per diem na posho za vikao.
Ukiisoma statement hiyo, ni kama tume imeshamaliza kazi yake, inaenda tu kupunga hali ya hewa.

Mkuu Chagonja, fikiria since November mnaokota maiti, taarifa zinatolewa hakuna hatua mnayochukua,
mtu anauawa tena hamchukui hatua na RPC wenu anatoa majibu rahisi rahisi tu, ulitaka ndugu yako
apigwe shoka na hao wauwaji ndo uamke na kutuma kikosi kazi.
Rai kwenu nyie viongozi wa polisi, mfanyie kazi hizi tetesi, siyo kupanga kulipua mikutano ya chadema as if chadema ndo jambazi sugu Tanzania.
 
Hakuna haja kupoteza pesa za walipa kodi kupeleka maafisa uchynguzi wakati wameshatoa taarifa rasmi ya uchunguzi hata kabla kufika eneo la tukio...hawafai kwenda maana wameshatoa maamuzi wanaenda kufanya nini sasa kama maamuzi yametoka pindi wakita dar bado???wanakula pesa zetu bure
Hawa wakuu wetu wa polisi vichwani watupu kabisa. Baada ya tamko la Mwakyembe kuhusu kauli ya Manumba tungetegemea kauli tofauti na hizi za kiwendawazimu. Siku moja lazima wasimame mbele ya haki.
 
wanapoteza muda tu ..yaani chagonja hajaanza kuchunguza anasema maandamano yalikuwa ya kihuni..nchi hii bwana...mi ndo maana natamani tupigane vita tusokomezane vijiti maeneo ya tukio ndo tutakuwa tunaheshimiana
 
kama anajua maandamano yalikuwa ya kihuni...sasa anaenda kuchunguza nini...maana anajua chanzo cha maandamano ni uhuni
 



Chagonja akizungumza na Mwananchi jana
alisema maandamano hayo hayakuwa ya amani bali ya kihuni kwani yalilenga kuvamia ofisi za serikali ikiwemo Ikulu ndogo na Ofisi ya Mkuu wa mkoa. Chagonja alikuwa akijibu swali lililotaka aeleze endapo haoni kama polisi imetumia nguvu kubwa kutawanya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani.

"Maandamano ya amani watu wanavamia Ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi ya mkuu wa mkoa?"

"Sijafika huko ndo naelekea lakini, yale si maandamano ya amani. Yaani
wahuni wanataka kuivuruga nchi waachiwe? Kuweni wazalendo, msiwe kama labda ninyi ni waandishi wa BBC kutoka Uingereza, hii ni nchi yenu."

Alifafanua kwamba, maandamano ya amani yanafahamika kwani watu hulazimika kuomba kibali na kuweka wazi ajenda ya maandamano "
Lakini siyo maandamano yale, watu hayakuwa na kibali chochote, wahuni wamejiingiza wanataka kuvuruga nchi tu."

Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema,"Usifikirie polisi hawana akili.
Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue hovyo risasi za moto kwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia..., lakini watu wanavamia Ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa, magari ya polisi hapo kuna amani kweli?"

Ukisoma hii taarifa ya mwananchi ni wazi kabisa hii team ya polisi toka makao makuu wameshafikia 'conclusion' ya uchunguzi wao. Angalia seheme nilizohighlight kwa red, utaona mkuu wa hii team ya uchunguzi - Chagonja, ameshaamua kuwa waliokuwa wanaandamana ni wahuni tena waliokuwa wamekusudia kuvamia Ikulu na ofisi ya mkuu wa mkoa!

Swali ambalo IGP Mwema angeweza kujibu ni kwanini apoteze hela za walipa kodi kwa kupeleka timu ya uchunguzi wakati team hiyo tayari ina majibu? Chagonja na wenzake wanaenda kufanya nini Songea? Kuongea na wahuni? Watu wa Songea ni wahuni?

Pili, ni kweli wananchi wa Songea hawakuwa na sababu nyingine ya kuandamana zaidi ya kuvamia Ikulu na ofisi ya mkuu wa mkoa? Nafikiri kitu cha kwanza anachotakiwa kufanya huyu Chagonja mara tu anapofika Songea na kuwaomba radhi wananchi wa Songea kwa kuwaita wahuni. Hili halikubaliki kabisa.
 
Hivi ni mahakama gani iliyopitisha hii hukumu kwa hao waandamanaji. kazi ya polisi ni nini. Hawa waliopigwa risasi walikuwa na silaha gani. Nazidi kuwa na chuki na serikali yangu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Maandamanoya amani watu wanavamia Ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi yamkuu wa mkoa?"
"Sijafika huko ndo naelekea lakini, yale si maandamano ya amani. Yaaniwahuni wanataka kuivuruga nchi waachiwe? Kuweni wazalendo, msiwe kama labdaninyi ni waandishi wa BBC kutoka Uingereza, hii ni nchi yenu."

Baada ya kusema haya , hakupaswa kwenda tena huko Songea,au labda anakwenda kutalii na kuharalisha posho ya safari, si kwenda kutafuta chanzo cha tatizo, majibu tayari anayo. WanaSongea msikubali tamko la huyo Chagonja tayari amewadharau, chukueni hatua nyingine.

Waandishi walitakiwa kumuuliza anaenda Songea kufanya nini wakati ameshachunguza na kubaini kuwa waandamanaji walikuwa wahuni?

Yaani huyu askari hata kazi yake haijui kabisa, haelewi hata scope of work aliyopewa. Unaendaje kuchunguza ukiwa tayari na upande unaoutetea na unaoukandamiza. Hawa watu wamelogwa na nani jamani.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hata ukiwa na moyo mgumu na kusema leo sichangii saa nyingine utajikuta tu unaandika

1. Hivi kweli hawa na kauli zao ndo viongozi wa majeshi na kutoka kwao tutegemee justice????
2. Biased.....unethical investgation ndo intelijensia ya jeshi hili??? Concluded before investgated????
3. Huwa hakuna mtu wa kuchunguza mambo kama haya zaidi ya huyo huyo tu tangu Arusha???

Sitamani kuamini.....hata kidogo....lakini ushahidi wa mtiririko wa matukio ya kuuana hovyo baina ya jeshi la polisi na wananchi inashawishi kukubali kwamba ama jeshi letu halina ujuzi wa kutosha kukabiliana na matukio ya vurugu ama wananchi wamechoshwa sana na hali ya Taifa letu kiasi cha kutojali tena kuishi ama laaa.

OPINION; Hata jipu huanza kama kipele.....amani tunayojidai tunayo inatoweka kwa kasi ilhali wenye jukumu la kuilinda mmelala fofofo....chonde chonde enyi wazee mloishi na kuridhika sisi bado vijana tuna nguvu na ujuzi wa kutumikia taifa letu ili tuishi kwa raha na amani kama ambavyo nyinyi mliishi na kulelewa na wazee wenu.....mnatuhuzunisha sana kwa uchoyo huu mnaotufanyia kwa makusudi.....mnatukatisha tamaa....mnatusononesha....mnatutia hasira sana.....inafikia hata kutujutisha kuzaliwa Watanzania.....mnatujengea hisia za visasi na kizazi chenu no wonder hata watoto hawawapishi tena watu wazima kuketi kwenye mabasi au kwenye foleni.

Imagine Rais huongea mara kadhaa na wazee n thus wana nafasi ya kusemea unyama kama huu....but wako kimya kabisa ndo maana nawaita wachoyo watu wazima hawa.......

Aaaaagh it is already a bad morning
 
chagonja anisamehe tu ila ameonesha uwezo mdogo sana wa matumizi ya akili anaenda kuchunguza wkt tayari ana NEGATIVE MENTAL ATTITUDE. jaman ivi nyie kina chagonja mnadhan hii ni nchi yenu pekeenu. just wait our time wil come
 
Kama hao waliouwawa ni wahuni na yeye pia anasound kama chizi! kwani aliambiwa wahuni ndio halali yao kuuwawa. Hivi hii nchi inawapa uongozi wavuta bangi ambao wana jump to conclusion bila kuwa logical!? what a shame!!
 
Yaani unajua unasoma statement ya mtu unajikuta unachukia source iliyokupa habari badala ya kumchukia mtoa habari.
Hii habari inaudhi, inakasirisha, inabore na inaonekana kutolewa na mtu ambaye ashatoa hukumu ya anachoenda kuchunguza
Hakukuwa na haja huyu Chagonja aende Songea kuchunguza kitu ambacho ameshakitolea hukumu.
Aache tuu wala asitumie kodi za watu kula raha huko wakati kashawasema waliondamana ni wahuni. Hata hao polisi walioua waachiliwe maana walikuwa wanapambana na genge la wahuni na wakorofi wa songea. Wanawashikilia kwa kipi maana wale walikuwa wahuni waliokuwa wanavunja sheria.
Yaani inaudhi kusoma matamko kama haya kutoka kwa mtu anayeenda kuwa kiongozi wa tume ya uchunguzi. And by the way hata majibu ya tume yake yakitoka hayatakuwa na faida maana yataozea kwenye makabati yao. Kwani ya arusha mpaka leo yanajulikana
Mwache akale raha songea kwa siku kadhaa.
 

"
Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema,"Usifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue hovyo risasi za moto kwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia..., lakini watu wanavamia Ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa, magari ya polisi hapo kuna amani kweli?"

Hivi huyu Chagonja akili yake imekaa kushoto au vipi. Hapa juu kwenye nyekundu inaonekana Changoja tayari ameamini kilichosemwa na Kamuhanda, anaamini polisi walikuwa sahihi. Sasa anakwenda kufanya uchunguzi gani tena na wa nini? Kwa nini uchunguzi ufanywe na polisi hao hao ambao ndio watuhumiwa wakuu kwenye ili suala? Kwa nini isiundwe tume huru isiyohusisha polisi kabisa kama kweli wanataka kufika to the bottom of the matter? We are not that much fools!!!!!

Tiba
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Chagonja aseme ukweli nani muhuni kati ya jeshi lake na wananchi. Wamepewa taarifa ya mauaji yanayoendelea hapo Songea na hakuna hatua yeyote ilichukuliwa. Alitaka wananchi wafanye nini waende kwao Polisi na kuwaambia kuwa tunaomba kibali cha maandamano kupinga Jeshi la Polisi kutowajibika na watu wasio na hatia kupoteza maisha? Anasema Usifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue hovyo risasi za moto kwa raia. Hayo mafunzo anayojisifia wanayo askari wake, mbona wameshindwa kuyatumia mpaka kuwafanya wakazi wa Songea kutafuta namna ambayo itawafanya Polisi kuwajibika. Na sioni mantiki ya kuundwa kwa tume ikiwa kiongozi wa tume anajua kila kitu kama alivyojieleza, naona ni matumizi mabaya ya pesa za Serikali.
 
Sasa huyu Chagonja ameshatoa verdict kwamba waliouawa walikuwa "wahuni", anaenda kufanya nini huko Songea? Ameshatoa kauli ambazo zinahalalisha vitendo vya askari kuwaua wale raia, kuna haja gani ya kupoteza rasilimali zetu? Atulie mjini aendelee kuwatetea.

namchukia sana huyu lodi lofa(chagonja) watu wanakufa kwa uzembe uzembe wa hao polisi wake, yakiwakuta kama yale ya zombe watalalamika kuwa haki haijatendeka, yaani natamani siku moja mungu atujaze nguvu kuu! waje waione nguvu ya wanyonge, pia waje wayaone machozi ya wanyonge na mayatima wa wahanga wa polisi, watakuja kujuta kama sio wao basi vizazi vyao
 
Hivi ni mahakama gani iliyopitisha hii hukumu kwa hao waandamanaji. kazi ya polisi ni nini. Hawa waliopigwa risasi walikuwa na silaha gani. Nazidi kuwa na chuki na serikali yangu.

Mkuu mimi binafsi nashindwa kuelewa tofauti ya polisi ya wakwetu na nchi nyingine katika kuzibiti maandamano wao wana bunduki lakini hawazitumii sijui mfunzo ya kipolisi kwa Tanzania ni tofauti na wenzetu.
 
Kazi kweli kweli kama polisi analojibu kwanini wanaenda kuchunguza?vilevile kauli za chagonja na RPC zinapishana,hii ndo bongo ofisi moja kauli mbili tofauti kufafanua jambo moja.
 

Mwenzenu nina mashaka makubwa juu uwezo wa kufikili wa Chagonja. Nadhani inabidi akapimwe akili kwanza kabla ya kuanza safari yake ya kuja songea.
 
Namuuliza Mjomba, hivi nchi yetu imekuwa ngumu kutawala kiasi hiki? Wanakosekana watu wenye busara na uvumilivu, wenye utashi wa kibinadamu katika safu ya viongozi wa jeshi letu kiasi cha kumwaga damu ya wenzetu kwa kisingizio cha kulinda amani? Kamwe, kwa mtindo huu, mwananchi atakuwa na imani na jeshi hilo. Mifano ni mingi na inajirudia. Panahitajika tafakuri pana na nzito kutenganisha kufanya kazi na utu wa mtu. Matamshi ya kwamba hao ni wahuni tuu inadhirisha ufinyu wa mawazo au kutosheka kwa mtoa kauli. Inasikitisha.
 
Back
Top Bottom