Polisi wanne mbaroni kwa mauaji ya raia Songea:IGP MWEMA APELEKA KIKOSI CHA UCHUNGUZI

Waandishi walitakiwa kumuuliza anaenda Songea kufanya nini wakati ameshachunguza na kubaini kuwa waandamanaji walikuwa wahuni?

Yaani huyu askari hata kazi yake haijui kabisa, haelewi hata scope of work aliyopewa. Unaendaje kuchunguza ukiwa tayari na upande unaoutetea na unaoukandamiza. Hawa watu wamelogwa na nani jamani.

Mkuu waandishi wetu wa habari wa leo kuna kitu? they can not go beyond, huwa nashangaa sana wanapewa kitu na kuchukua/copy mbio wanakimbia ofcn kwao kuandika. Walio makini walipaswa kuhoji hilo maana ndo msingi wa safari nzima to Songea. Anyway lets hpe itakuwa fair maana yupo RSO,OC Ngome wa kule, Boss kubwa ya Immigration na mkuu wa wazuia rushwa wa mkoa
 
Chagonja anaenda kufanya nini Songea wakati keshahukumu? Anakwenda kuchunguza au anakwenda kukamilisha ratiba na kutumia pesa ovyo? Anawaitaje wananchi wote wale kuwa ni wahuni? Hivi wote wale wangekuwa wahuni huko Songea kungekalika? Bado naona ni mwendelezo wa dharau kwa wananchi unaofanywa na viongozi wa polisi. Kwanza Rpc alitangaza kuwa yale mauaji yaliyojumuisha kunyofoa sehemu za siri si lolote si chochote bali ni mambo ya mapenzi! Na sasa kiongozi mwingine Chagonja anawaita wananchi "wahuni"! Na kwamba ili waandamane walitakiwa waende polisi wakaombe kibali, hivi ni sheria ipi inayoelekeza hivyo? Hata katiba iliyopo sasa pamoja na mapungufu yake haitoi mamlaka kwa polisi kuwa ni ofisi ya kuratibu maandamano. Acheni dharau.
 
Tungekuwa na BUNGE lenye kutekeleza wajibu wake haya yote yangekoma mara moja! bahati mbaya sana bunge letu ni sawa na chama cha siasa!!!
 

IGP Mwema achunguza
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema ametuma kikosi cha maofisa waandamizi kutoka makao makuu ya jeshi hilo, kikiongozwa na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo, Kamishna Paul Chagonja kwenda mjini Songea kufanya uchunguzi wa ghasia hizo. Chagonja akizungumza na Mwananchi jana alisema maandamano hayo hayakuwa ya amani bali ya kihuni kwani yalilenga kuvamia ofisi za serikali ikiwemo Ikulu ndogo na Ofisi ya Mkuu wa mkoa. Chagonja alikuwa akijibu swali lililotaka aeleze endapo haoni kama polisi imetumia nguvu kubwa kutawanya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani.

"Maandamano ya amani watu wanavamia Ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi ya mkuu wa mkoa?"
"Sijafika huko ndo naelekea lakini, yale si maandamano ya amani. Yaani wahuni wanataka kuivuruga nchi waachiwe? Kuweni wazalendo, msiwe kama labda ninyi ni waandishi wa BBC kutoka Uingereza, hii ni nchi yenu."
Alifafanua kwamba, maandamano ya amani yanafahamika kwani watu hulazimika kuomba kibali na kuweka wazi ajenda ya maandamano "Lakini siyo maandamano yale, watu hayakuwa na kibali chochote, wahuni wamejiingiza wanataka kuvuruga nchi tu."

Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema,"Usifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue hovyo risasi za moto kwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia..., lakini watu wanavamia Ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa, magari ya polisi hapo kuna amani kweli?"

Alitoa angalizo kwamba ni lazima hata vyombo vya habari, viache ushabiki badala yake viangalie maslahi ya taifa kwani nchi ikivurugika wao pia hawatasalimika na kusisitiza, "Kuweni wazalendo bwana, msifikirie kulishutumu jeshi la polisi tu



Kwa mtazamo wangu:

IGP Mwema: Yambidi aelewe kuwa:-

- Kumpeleka Chagonja huko Songea kuwa kiongozi wa hiyo safari ya kuchunguza hatoweza kupata jibu lililo sahihi, kwani tayari ameanza kuhukumu kabla ya kufika eneo la tukio. Ina maana hatokuwa na jibu jipya. Ni heri abaki DSM kwa majukumu mengine kuliko kupoteza peas kwenda Songea na ikiwa tayari report ndio hii aliyowapa Waandishi wa Habari.

- Afande Chagonja ni mkuu wa Mafunzo, lakini huenda naye ana walakini kwani askari wake aliofundisha ndio hao wanatumia risasi ovyo, wanaua raia badala ya kulinda raia na mali zao kama inavyosema kauli mbiu ya Jeshi la polisi.

- Afande Chagonja ana walakini kwani anatetea askari, ina maana hata akimuona askari anaiba yeye atakwambia kuwa ameokota siyo kuiba. Yaani anatetea uhalifu.

-Kutokana na matukio ya mauaji ya Raia yanayofanywa na Askari Polisi mfano kaika maandamano au hata mitaani mfano yale ya Mwanafunzi wa chuo kuleMbeya, yanafanya Wananchi wakose Imani na Askari Polisi, kiasi kwamba hata mtu akipita njiani na Polisi amebeba Bunduki anakuja mbele yake, yule raia itambidi atafute njia nyingine asije kutana na Polisi kwa hofu ya kupigwa risasi. KWani tumeshuhudia mauaji yasiyo na sababu, kwa kisingizio ni jambazi!!!!! Hii inajenga uhusiano mbaya kati ya Polisi na Raia.


Afande Chagonja yambidi aelewe kuwa:-

-Kiongozi mzuri na mtendaji huwa hatoi kauli kabla ya kufuatilia, asipokee report mezani na kuitangaza kuwa ndiyo report kamili. Askari wake akiwemo Kamanda wa Mkoa wanamdanganya naye anakubali. Ataharibu CV yake na kupoteza uaminifu kwa raia.

-Ungelikuwa na busara kama usingeliwajibu hao Waandishi wa Habari. Ungewaambia wasubiri urudi Songea ndio uongee nao. Sasa unapotoa majibu ina maana hakuna sababu ya wewe kwenda Songea kumbe unaweza kutoa report hapo hapo DSM. Sasa Songea unafuata nini au kuwatunuku vyeo askari wauaji??? BADO SIPATI :photo::photo::photo: JUU YA SAFARI YAKO.

-Kama wewe ulivyowatetea askari wako kuwa ni watu wenye akili; lakini elewa kuwa hata wale wananchi waliondamana si kwamba ni wahuni kama ulivyowaita (Kwanza hili ni TUSI KUBWA SANA KUTOLEWA NA MKUU KAMA WEWE) ni watu ambao waliamua kufanya vile baada ya Polisi kushindwa kuzuia mauaji ya ajabu yaliyokuwa yanatokea. ingawa Polisi walipewa taaarifa lakini hakuna juhudi iliyofanyika na vifo viliendelea.

-Afande ukiwa kama mkuu wa mafunzo, tafuta mbinu ili Polisi wajue kuwa kutumia nguvu kubwa siyo kumaliza tatizo. Mfano Polisi wameua na sasa raia wanafikia hatua ya kuua kila mtu wanayemdhania kuwa ni kutoka nchi jirani msumbiji. Ni hatari kwa itaharibu uhusiano kati ya Tanzania na jirani zetu Msumbiji. Sasa hapa Polisi hawajatatua tatizo bali wanaongeza matatizo.

-IEleweke kuwa katika tukio kama hili ni kwamba raia walikuwa wanashurutisha Polisi iwalinde kutokana na mauaji ya ajabu, sasa hapa sidhani kama raia hawa wangeenda kuomba kibali Polisi kuwa "tunataka kuandamana kukushurutisha wewe mkuu wa Polisi mkoa, mbona hutupatii ulinzi!!!!" Sidhani hata ungelikuwa ni wewe Afande Chagonja ndiye Kamanda wa Mkoa waSongea kama ungelitoa hicho kibali unachosema hawakuwa nacho!!!!

Je, kama Polisi wana akili (Kutokana na Kauli) wale waliofyatua Risasi kule Mbeya na kuua mwanafunzi wa Chuo Je, ni akili hiyo unayosema ndio iliwatuma kufyatua risasi? au ni Mgambo wale?. Au Hawakupitia mafunzo? NASHINDWA KUPATA :photo::photo:

Hivyo wakati mwingine tuangalie na mara kwa mara Jeshi la Polisi linatusisitizia Raia tushirikiane na Polisi katika kufichua uhalifu (ULINZI SHIRIKISHI) sasa sidhani kama mtafanikiwa katika kuwashirikisha wananchi endapo:-

-Wakitoa malalamiko yao nyie mnawajibu kisiasa.
-Mtajenga mahusiano mabaya na hawa wananchi.


"JESHI LA POLISI NI WAKATI SASA UMEFIKA KUBADILIKA"


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Jeshi la Polisi la Tanzania ni jeshi la wauaji toka mwaka 2005 Polisi wamekuwa wakiua raia wasio na hatia kila mwezi kati ya 1 - 30 jeshi gani hilo wanaooga kwenye damu za wananchi,jeshi gani hilo ambalo liko juu ya sheria,lililoharaisha kuua kama sehemu rasmi ya operesheni zake za kila siku,
Polisi wanaua raia hakuna hata uchunguzi umewahi kufanya

IGP Mwema anakiuka viapo vyake vya kijeshi amegeuka naye kuwa mwongo,hana tofauti na Jakaya KIkwete,Pinda,Ngereja,Mponda mwongo mwongo mwongo ndio maana nidhamu ya wanachi imeondoka kwa jeshi la Polisi hakuna mwanachi anawaheshimu tena no wonder kila utafiti ukifanywa jeshi linaongoza kwa rushwa

Chagonja ni muongo,mbabe,anatoa vitisho si kiongozi rafiki wa mazingira ya kimugogoro huyu ndie aliyetengeneza CD za propaganda kuhusu mauaji ya Arusha,alindanganya waziri mkuu ni muongo mwananchi gani mpenda haki ataamini neno lolote litokalo kinywani mwa Chagonja ni muongo sana huyo angalia kabla hajafika Songea kula fedha za kodi ya wananchi tayari yeye anaripoti
hakuna Tume ya ukweli wangetaka wangewahusisha wanashelia wa TLS,LHRC, na wananchi wengine kutoka dini,wazee maarufu hapo Songea,viongozi wa kijamii hiyo ndio tungesema ripoti
 
Hapo kuongeza matumizi yasiyo ya lazima na hao polisi wanaohojiwa ni changa la macho, mtanzania gani hajui waliompiga Jenerali Kombe leo wako mtaani, angalia kina Zombe wanasubiri hukumu ya Mungu kama Ditopile.
 
IGP Mwema,
Jitambue kama wewe ndio muhusika wa mauaji yote, yanayofanywa na jeshi la polisi Tanzania.
Tokea risasi ya kwanza iliyotumiwa na askari kutoa roho za Watanzania, hapo tu ilitosha wewe
kuchukua hatua madhubuti za kuzuia mauaji ya raia kwa upande wa jeshi polisi la unaloliongoza.
Reform ilihitajika, nayo ni kuzuia kwa askari wote wanaohusika kulinda maandamano au kuzuia
maandamano ambayo mnayaita yasiyo halali, kutokuwa na silaha za moto kabisa, zaidi ya mabomu
ya moshi, na askari wote wanahitajika wawe na Marungu tu. Kwa sababu waandamanaji siku zote
ni watu wasiokuwa na silaha, na nguvu zinazotumiwa kwa waandamanaji zingefaa kukabiliana na
majambazi. na kila siku polisi wanapoua raia kunakuwa na utetezi wa kutunga,kwa ajili ya wewe
uwe umejisafisha, na hiyo yote ni kujidanganya, kwa sababu uwezi kujisafisha katika kosa la jinai
ulilotenda. Wakati wote unatakiwa upanue uigo wa akili zaidi kujumlisha na kile ulichokisoma,
kuning'iniza shahada ukutani bila kuifanyia vitendo, ni sawa na picha ya kumbukumbu ambayo
usahaulika na kwa nadra uwa inakumbukwa. Sasa huo ndio uhalali wa kuongoza jeshi la polisi,
umeshafika wakati inakubidi upumzike, kwani madoa ni mengi juu yako.
 
Back
Top Bottom