Polisi Tanzania na Interpol wamkamata aliyowatapeli Watalii waliokuja kupanda Mlima Kilimanjaro

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Jeshi la Polisi Tanzania limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyewatapeli watalii waliokuja nchini kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro huku likibainisha kuwa Tanzania ni nchi salama kwa wageni wa ndani na nje ya Tanzania.
1b78c7c6-448a-4f6a-8d56-88bff57d74ba.jpeg

79851bb1-1d0f-46a0-91f0-47082e4b3170.jpeg
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Maigwa katika lango la mweka ambalo hutumika kushuka kutoka katika Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu barani Afrika, Januari 27, 2024.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi huku akibanisha kuwa mtuhumiwa anatoka nje ya Tanzania, huku akiwaomba watalii hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania.

Amewapongeza watalii hao zaidi ya 30 kwa namna walivyo kitangaza Kituo cha Polisi Utalii na Diplomasia Arusha na Kilimanjaro kwa kupandisha bango linaloaiambia Dunia kuwa Tanzania ni sehemu salama kwa utalii na kutembelea.

Upande wake, Chris Lomas ambae ni Mkurungenzi wa Kampuni ya Hope for Love ameishukuru Serikali na Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wamelifuatilia suala lao hatua moja baada ya nyingine na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliye watapeli.

Nae, Oscar Mosha ambaye Mkurungenzi Msaidizi wa Kampuni ya Utalii ya Tanzania Escapade ambayo inashughulika na kuwapandisha watalii katika Mlima Kilimanjaro amewashukuru watalii hao kwa kuchagua kuja Tanzania na kupanda Mlima Kilimanjaro huku akiwa waambia Tanzania ni sehemu salama kwa utalii.

Franke Alexnder ambaye ni Afisa Mtalii Mkuu Kanda ya Kaskazini amewapa pole kwa kilichotokea huku akiwa wakiwakikishia Tanzania ni salama.

Mkuu wa kituo cha Polisi utalii na Diplomasia Mrakibu wa Polisi SP Waziri Tenga amesema Tanzania ni salama na Kilimanjaro ni salama ambapo amewaambia wasjikie wako salama.
 
Back
Top Bottom