Polisi tafuteni majambazi sio kupiga mabomu wananchi wanaodai haki zao kwa amani!!

Click_and_go

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
451
5
....matukio mengi sana ya maandamano ya amani nchini Tanzania yamegubikwa na fujo ambazo maranyingi husababishwa na polisi kuingilia kati wakidai eti kuna uvunjifu wa amani!!
lakini ukweli ni kwamba polisi huja kuvuruga amani na kusahau jukumu lao la kulinda watu na mali zao!
...tumeshuhudia maandamano mbali mbali ya wanafunzi na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali yakivurugwa na polisi, japokuwa maandamano yao huwa ni ya amani kabisa!!!
....nawaomba polisi watumie nguvu hiyo kubwa katika kusaka wezi, vibaka na majambazi sio kujileta wakati wa maandamano na kufanyia miili ya watu kuwa "specimen" ya kujaribishia mafunzo yao waliyofundishwa huko kwenye kambi zao!!!!
 
Polisi wako kila kona ya nchi hii, acha waendelee na ujinga wao wakujifanya wanapata taarifa za kiintelijensia wakati hakuna lolote. Wakumbuke ipo siku watataarifiwa na ndugu zao kuwa kuna ndugu yake kauwawa na polisi hivyo anatakiwa kwenda kuzika au kuendelea kuzuia maandamano mengine ndiyo tutajua akili zao ziko sawa au ziko alijojo:roll::popcorn::sick:
 
Back
Top Bottom