Polisi: Marufuku Waandishi na Wananchi kukusanyika Polisi watuhumiwa wakiitwa kuhojiwa

Kuzuia wananchi wasio na kazi kukusanyika vituo vya polisi ilikuwa ni sahihi, ila si kuzuia waandishi wa habari ambao wana vibali vyao vya kufanya kazi
 
Safi sana. Nyerere alikuwa na akili sana yule mzee basi tu kuna baadhi ya mambo alibugi. Ukishaanza kula nyama ya mtu hautaiacha, ukishaanza ubaguzi hautakoma. Hizi movement na matamko na amri zinazotolewa kama kuna watu wanaamini wao watakuwa salama wanajidanganya. Ipo siku Lizaboni, Barbarosa na wenzao wataingia tu kwenye mtego huu.

Dawa ya dhambi ni kuikemea hata kama unahisi wewe haikuathiri. For sure ipo siku itakuathiri tu. Wacha tuendelee kupiga makofi tukidhani wahusika wa mwenendo huu ni akina manji au melo nk. Mtachomolewa mmoja mmoja kama Simba anavyojilia nyumbu vile. Time wil tell.
safi kabisa mkuu umenena vema, kuna mijitu kama hiyo uliyoitaja ni shida utadhani wao hawana ndugu au jamaa ambao kwa namna nyingine wanaweza kuwa waathirika hayo.
 
Katika hili nakubali kabisa acha iwe hivyo , maana kilichofanyika pale central ni kuonesha ulimwengu kuwa hakuna vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania.

Hivyo, acha sasa ieleweke kuwa serikali ina mkono wa kukumata na ina macho ang'avu sana kukuona popote pale ulipo japo, pana nyakati serikali hujifanya kama vile haioni ila inazo taarifa za kila mmoja wetu na tukifanyacho.

Kama , kweli sisi watanzania tungekuwa wazalendo tusinge furahia kile kitendo cha kwanya na washabiki wa mpira kwenda kufanya vitimbwi pale kituo kikuu cha Polisi (central)

Hata, waliokuwa zamu Mwenyezi Mungu, aliwashangaa sana kwa kuwasamehe wale walioenda kufanya kwaya na vihoja pale kituoni.

Maana huyo Mungu, wanaemuimbia ni wa utaratibu na siyo wa fujo kama walizozifanya kwa kelele pale kituoni.

Mimi ni mwamini ila kwa hilo, lilofanywa walipaswa hata kupata kifungo cha chini kama cha miezi 6 hivi ndiyo wajielewe kuwa serikali siyo Kanisa au uwanja wa mpira.

Pia, naona Taifa watu wamengawanyika sana kwa sababu hawaelewi tena misingi ya utaifa wao.

Ila, Rais Magufuli ataweka misisngi ambayo daima tutaelewa na kukumbuka kuwa Rais Magufuli alifanya mambo makubwa sana kwa nchi yetu.

Ieleweke kuwa , sitetei mtuhumiwa hapa, ninachosema ni kuwa ... "wapambe wa watuhumiwa walifanya makosa makubwa pale central"... ila watuhumiwa itajulikana hatima yao.

Ila kwa vitendo vile acha Polisi na vyombo vingine vya ulinzi vifanye kazi zao.

Hamna namna tena, maana haiwezekani serikali ikafanywa kama mwanasesere na kila mtu.

Ikiwa hivyo, hatutafika wala hatutakuwa salama tena.

Ahsanteni.
 
Baada ya sirro kubanwa na Mkuu ...........................eti pale kituoni mnaosha magari? ndio wameamua hivo

Bongo ya leo sio ya jana
 
Yaani wangeanza kususia hata hii habari ingekuwa funzo kwao.
Polisi wanawategemea wananchi na wanahabari ili wafanikiwe kwenye kazi zao. Sasa hiki wanachokifanya ukweli watavuna mabua. Very bad
 
Hawa Polisi wana akili za kuwatosha wao wenyewe, sio kuzitumia kwa watu wengine, Kwani waandishi wa habari wanapokuja Polisi wanaambiana twende tukakusanyike Polisi hadi mseme marufuku kwao kukusanyika Polisi? Si kila mwandishi anaenda kivyake? Ndio maana mnaambiwa hamna uwezo wa kufikiri nje ya kutoa amri. Nina wasiwasi harufu mbaya kwenye vituo vya polisi inaathiri uwezo wa mtu wa kufikiri ukiivuta kwa muda mrefu.
 
Kwa hiyo zile silaha za maigizo wanazo onyesha kwenye tv kwamba wamepambambana na majambazi wakazishika sasa wao polisi watakuwa wanaenda studio???
Ushauri wangu kwa wana habari nanyi kama taasisi mnatakiwa msusie kuandika habari yoyote mtakayo itwa na polisi. Acheni njaa. Ili na wao waone kama wanaweza kufanya kazi bila nyie. Hata taarifa za usalama barabarani acheni asap!!!!
 
Katika hili nakubali kabisa acha iwe hivyo , maana kilichofanyika pale central ni kuonesha ulimwengu kuwa hakuna vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania.

Hivyo, acha sasa ieleweke kuwa serikali ina mkono wa kukumata na ina macho ang'avu sana kukuona popote pale ulipo japo, pana nyakati serikali hujifanya kama vile haioni ila inazo taarifa za kila mmoja wetu na tukifanyacho.

Kama , kweli sisi watanzania tungekuwa wazalendo tusinge furahia kile kitendo cha kwanya na washabiki wa mpira kwenda kufanya vitimbwi pale kituo kikuu cha Polisi (central)

Hata, waliokuwa zamu Mwenyezi Mungu, aliwashangaa sana kwa kuwasamehe wale walioenda kufanya kwaya na vihoja pale kituoni.

Maana huyo Mungu, wanaemuimbia ni wa utaratibu na siyo wa fujo kama walizozifanya kwa kelele pale kituoni.

Mimi ni mwamini ila kwa hilo, lilofanywa walipaswa hata kupata kifungo cha chini kama cha miezi 6 hivi ndiyo wajielewe kuwa serikali siyo Kanisa au uwanja wa mpira.

Pia, naona Taifa watu wamengawanyika sana kwa sababu hawaelewi tena misingi ya utaifa wao.

Ila, Rais Magufuli ataweka misisngi ambayo daima tutaelewa na kukumbuka kuwa Rais Magufuli alifanya mambo makubwa sana kwa nchi yetu.

Ieleweke kuwa , sitetei mtuhumiwa hapa, ninachosema ni kuwa ... "wapambe wa watuhumiwa walifanya makosa makubwa pale central"... ila watuhumiwa itajulikana hatima yao.

Ila kwa vitendo vile acha Polisi na vyombo vingine vya ulinzi vifanye kazi zao.

Hamna namna tena, maana haiwezekani serikali ikafanywa kama mwanasesere na kila mtu.

Ikiwa hivyo, hatutafika wala hatutakuwa salama tena.

Ahsanteni.
hakuna haja ya kushukuru "Ahsanteni" tumekusoma tumekusikia manake wengine tulikuwa tunasomewa bandiko lako hatuna macho yanayoona.
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania ACP Advera Bulimba ametoa agizo la kuzuia ukusanyikaji wa watu katika vituo vya polisi wakati wa kuhojiwa watu/watuhumiwa maarufu.

Agizo hilo ni kwa waandishi wa habari, vikundi vya watu na wananchi wa kawaida.

Kufuatia agizo hili la polisi,lililotolewa 14/02/2017 na Makao Makuu ya Polisi, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaokiuka agizo hilo.

Agizo hili linaanza kutekelezwa mara moja katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi Tanzania bara na visiwani.

Taarifa hii inakuja siku kadhaa baada ya Rais Magufuli kukemea hali ya wanakwaya wa kanisa la Ufufuo na Uzima kukusanyika na kuimba mapambio wakati wakimsubiri Askofu wa kanisa lao akihojiwa kwa tuhuma za midaharati, huku wafuasi waliokuwa wamevalia sare za klabu moja maarufu ya mpira, nao wakikusanyika na kusubiri mustakabali wa kiongozi wa klabu yao.
Hapo sasa, waandishi wa habari wakapatie wapi taarifa sijui
 
Hiyo ni hatua nzuri maana kama walitegemea watapata kazi ya kulinda viwanda wameula wa chuya, hadi sasa miezi 16 hakuna hata kiwanda kimoja kimejengwa na hii serikali ya awamu ya tano. Milioni 50 kila kijiji nazo hakuna kwa hiyo polisi hata kazi ya ku escort hela wanaikosa. Bora wafanye siasa tu
Unamsubiri nani akujengee kiwanda?
 
Ile dhana ya polisi jamii, ushirikiano kati ya wananchi na polisi inakufa baada ya sizonje kutamani kuwa polisi mkuu
Polisi jamii haimaanishi kwenda kurundikana polisi kwa ajili ya mtuhumiwa mmoja,mnaweza kwenda wachache na si kuchukua sarakabo yote eti kumsindikiza mtu mmoja km mnaenda kuzika.
 
Back
Top Bottom