Polisi: Kigwangalla hajampiga risasi mlinzi Jumanne

jeshi letu la polisi lina mapungufu mengi tu lakini si kila sehemu tulihukumu, juzi kati kuna kijana alikuwa nyumba ya kulala wageni anakula zake starehe lakini alidanganya kuwa ametekwa. nadhani itakuwa si busara kila wakati kuwahukumu bila kuwa na ushahidi wa kutosha.
 
“Hata hivyo Jumanne alipewa PF3 na kwenda Hospitali ya Wilaya ya kwimba kwa uchunguzi wa kitabibu, Hamisi Kigwangala alihojiwa na kufunguliwa kesi ya shambulio na yupo nje kwa dhamana”

“Uchunguzi umebaini kuwa hakuna jeraha wala mvunjiko wowote wa mfupa katika mwili wa Jumanne na hivyo amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Afisa wa Polisi na kuzua taharuki kwa Jamii kuwa amepigwa risasi, upelelezi wa kesi hizo mbili unaendelea na utakapo kamilika Watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi”

Mbona Contradiction nyingi kwenye taarifa ya polisi? Hakuna Jeraha wala mvunjiko halafu hapo hapo amepewa PF3??

Omary J4 Said siyo mjinga ,HK kampiga risasi ya mguu!
 
Polisi Mkoani Mwanza wametoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni kumhusu Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Mmiliki wa Kiwanda cha kuchakata Pamba kitwacho Mwalujo Ginery kilichopo Kijiji cha Mwalujo, Wilaya ya Kwimba, Hamisi Kingwangala kudaiwa kumpiga risasi Mlinzi wake Jumanne Omary Misango (66) katika mguu wa kulia, ambapo imebainika Jumanne hakupigwa risasi bali haliwaongopea Polisi.

RPC wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema taarifa za awali zinaonesha kulitokea wizi wa mali kiwandani ikiwemo Gear Motor HP Radio made 02, Electrical Motor 05 na nyaya za umeme @ Armored Cable Mita 25 vyote vikiwa na thamani ya Tsh 28,525,000.

“Mei 22, 2023 saa 11:00 jioni Kigwangala alifika kiwandani kwake na kukatokea majibizano kati yake na Mlinzi wake, Mlinzi huyo alitoa taarifa Polisi kuwa alishambuliwa na kupigwa risasi mguu wa kulia, Askari walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi ambapo hakukuonekena viashiria vyovyote vya matumizi ya silaha ya moto”

“Hata hivyo Jumanne alipewa PF3 na kwenda Hospitali ya Wilaya ya kwimba kwa uchunguzi wa kitabibu, Hamisi Kigwangala alihojiwa na kufunguliwa kesi ya shambulio na yupo nje kwa dhamana”

“Uchunguzi umebaini kuwa hakuna jeraha wala mvunjiko wowote wa mfupa katika mwili wa Jumanne na hivyo amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Afisa wa Polisi na kuzua taharuki kwa Jamii kuwa amepigwa risasi, upelelezi wa kesi hizo mbili unaendelea na utakapo kamilika Watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi”

Credit: MillardAyo
yalisemwa na sasa yemetimia
 
Hiyo RUSHWA aliyopokea RPC wa Mwanza kutoka kwa Kigwangalla itamtokea puani. Nakuonya RPC Mutafungwa kuwa UTAFUNGWA, ba careful. Wenzio hupokea Rushwa kwa akili sana lakini ya kwako umepokea kizembe
Sasa naona akili imerudi RPC Mutafungwa
Screenshot_20230528_141813_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom