REAGAN C.MABOGO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 1,269
- 1,007
Mtu anapokamatwa, anapaswa afikishwe mahakamani mara moja! Na siyo kumuweka kituoni na kuacha kumpeleka mahakamani! Na pengine,(na hii ni hatari) kuanza kumtesa kwa vipigo na mateso ya kila aina.
Jana tumeambiwa mmemkamata kiongozi mmoja wa CHADEMA huko mkoani Mbeya,mkampiga sana na kumvunja miguu yote! Mbaya zaidi hata huduma hamtaki apate, sijui ili afe?! Au apate kilema?!
Leo tena tunaambiwa kumbe mlimkamata Mbunge wa Arusha Godbless Lema mapema alfajiri.! Cha ajabu na kuuzi ni hiki: muda huo ulikuwa unatosha kumpeleka mahakamani, ni kwa nini hamkumpeleka mahakamani?! Kama hoja yenyewe ya kukamatwa kwake ni hiyo ndogo tu?! (uchochezi).
Ni upelelezi gani unaofanyika kwa kitu kidogo hicho?! WITO, watanzania tudai katiba mpya. Katiba itakayodhibiti madaraka hewa katika nchi yetu. Mnadhani ni sahihi kutomfikisha mahakamani eti tu kwa kuwa saa 24 hazikuwa zimetimia hiyo jana na zimetia leo "wikiendi" ambapo hakuna mahakama?!
Naamini kuna polisi wanaochukizwa na tabia hii ya wenzao.
Tushirikiane kuitokomeza.