Polisi isigeuke kuwa kundi la kutesa Raia

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,269
1,007
Mtu anapokamatwa, anapaswa afikishwe mahakamani mara moja! Na siyo kumuweka kituoni na kuacha kumpeleka mahakamani! Na pengine,(na hii ni hatari) kuanza kumtesa kwa vipigo na mateso ya kila aina.

Jana tumeambiwa mmemkamata kiongozi mmoja wa CHADEMA huko mkoani Mbeya,mkampiga sana na kumvunja miguu yote! Mbaya zaidi hata huduma hamtaki apate, sijui ili afe?! Au apate kilema?!

Leo tena tunaambiwa kumbe mlimkamata Mbunge wa Arusha Godbless Lema mapema alfajiri.! Cha ajabu na kuuzi ni hiki: muda huo ulikuwa unatosha kumpeleka mahakamani, ni kwa nini hamkumpeleka mahakamani?! Kama hoja yenyewe ya kukamatwa kwake ni hiyo ndogo tu?! (uchochezi).

Ni upelelezi gani unaofanyika kwa kitu kidogo hicho?! WITO, watanzania tudai katiba mpya. Katiba itakayodhibiti madaraka hewa katika nchi yetu. Mnadhani ni sahihi kutomfikisha mahakamani eti tu kwa kuwa saa 24 hazikuwa zimetimia hiyo jana na zimetia leo "wikiendi" ambapo hakuna mahakama?!

Naamini kuna polisi wanaochukizwa na tabia hii ya wenzao.

Tushirikiane kuitokomeza.
 
Uhasama baina ya polisi na raia ni mbaya sana! polisi wanaweza kujiona ni superior kuliko raia pindi wavaapo kadeti na kutundika silaha begani lakini siyo kweli.Unaweza kumtesa mtu ama kumua ndugu yake but kumbuka kuna watu wenye chuki, hasira na kulipiza visasi.Mtu unayemuonea ataweza akakusize ukiwa peke yako, au mkeo, au watoto na akafanya jambo la kukutoa machozi. Raia mnao watesa ndio mnaokunywa nao, wanawazalisha wake zenu na kuwaona watoto wenu so nadhani tunatakiwa kuishi kindugu zaidi.
 
Polisi wanatumwa na baadhi ya viongozi ambao tupo na wao. Nadhani tuanze kuwalaumu viongozi wa kiserikali tukianza na mkuu wa usalama au ulinzi wa mkoa ambaye ni mkuu wa mkoa. Then baada ya hapo tuje kwa mkuu wa Wilaya. Ni upumbavu uliopitiliza endapo mtazidi kufanya aina ya tabia mnayoonesha wananchi. Kwa sababu basi tuliamua kuwa na katiba basi ifuatwe. Apelekwe mahakamani. Mkuu wa mkoa asimamie nafasi yake.
Mkuu wa wilaya hivo hivo. KUJIFANYA UNAZIBA MASKIO WAKATI UKIWA DISCO KUMBUKA UTATOKA TENA NJE. Nimalize na jeshi la polisi, Tunawaomba hata kama mnalinda kula yenu jaribuni kuweka utu mbele duniani sio kwetu. Hatutaondoka na vyeo vyetu baada ya sayari dunia.
 
Uhasama baina ya polisi na raia ni mbaya sana! polisi wanaweza kujiona ni superior kuliko raia pindi wavaapo kadeti na kutundika silaha begani lakini siyo kweli.Unaweza kumtesa mtu ama kumua ndugu yake but kumbuka kuna watu wenye chuki, hasira na kulipiza visasi.Mtu unayemuonea ataweza akakusize ukiwa peke yako, au mkeo, au watoto na akafanya jambo la kukutoa machozi. Raia mnao watesa ndio mnaokunywa nao, wanawazalisha wake zenu na kuwaona watoto wenu so nadhani tunatakiwa kuishi kindugu zaidi.
We jaribu uguse familia ya Soja na masoja wenyewe walivyopinda hivi, atakufuatilia na kumaliza ukoo wako wote mpaka mende kabatini! Bora mtulie huo UKUTA msishikishwe bila kujitambua.
 
We jaribu uguse familia ya Soja na masoja wenyewe walivyopinda hivi, atakufuatilia na kumaliza ukoo wako wote mpaka mende kabatini! Bora mtulie huo UKUTA msishikishwe bila kujitambua.
Nani amesema atagusa familia ya mtu? unafikiri ni wote wenye ukoo? kuna sehemu nimetaja UKUTA? sorry for your defective perception, you 'r ineed of mechanical psychiatrist!
 
MA-UKUTA YANALALAMIKA KAMA MATOTO
tofautisha mtu kulalamika na kusema ukweli. Kwa mtizamo wako

1-Ni Sahihi polisi kumnyima dhamana raia?
2- Ni sahihi polisi kumkamata mtu bila kosa?
3- Ni sahihi polisi kujichukulia kazi za mahakama?
 
tofautisha mtu kulalamika na kusema ukweli. Kwa mtizamo wako

1-Ni Sahihi polisi kumnyima dhamana raia?
2- Ni sahihi polisi kumkamata mtu bila kosa?
3- Ni sahihi polisi kujichukulia kazi za mahakama?
Polisi siyo wapuuzi mpaka kumkamata mtu asekua na kosa...hao wote ulowamention before wanamakosa ambayo unayafahamu....so waache watu wafanye kazi yao...kama wewe unavyofanya yako ya kueneza propaganda
 
Tunatamani sana kuwa na Polisi kwenye weledi mkubwa wa kufanya kazi, elimu nzuri na hofu ya Mungu. Ubabe na ukatili ni urithi mbaya sana toka kwa wakoloni!
 
Uhasama baina ya polisi na raia ni mbaya sana! polisi wanaweza kujiona ni superior kuliko raia pindi wavaapo kadeti na kutundika silaha begani lakini siyo kweli.Unaweza kumtesa mtu ama kumua ndugu yake but kumbuka kuna watu wenye chuki, hasira na kulipiza visasi.Mtu unayemuonea ataweza akakusize ukiwa peke yako, au mkeo, au watoto na akafanya jambo la kukutoa machozi. Raia mnao watesa ndio mnaokunywa nao, wanawazalisha wake zenu na kuwaona watoto wenu so nadhani tunatakiwa kuishi kindugu zaidi.
Hakuna kitu kama hicho. Uhasama ni kati ya majambazi, wachochezi, na polisi.
 
Makonda amewaambia polisi wakikuta watu msituni wao wapige hasa na hao watu wa haki za binadamu wakiuliza waambiwe wakumuulize Makonda.
 
Mungu ibariki chadema , ushahidi wa wazi unaonyesha kwamba HAKUNA MAHALI POPOTE KATIKA DUNIA HII AMBAPO DHULUMA ILIWAHI KUISHINDA HAKI .
 
Back
Top Bottom