Polisi: Idris Sultan anashikiliwa kwa kujaribu kuharibu ushahidi na makosa mengine ya kimtandao

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,450
3,408
Jeshi la Polisi limesema linaendelea kumshikilia Idris Sultan aliyekamatwa Jumanne iliyopita akihusishwa na tuhuma za makosa ya kimtandao likiwemo la kujaribu kuharibu ushahidi.

Mchekeshaji huyo alikamatwa na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar ambako alihojiwa kwa kutuhuma za uonevu wa Kimtandao ikiwa ni siku chache baada ya kuweka picha ya zamani ya Rais Magufuli iliyoambatana na video yake akicheka.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Tunaendelea kumshikilia kwasababu kubwa mbili; moja ni kuwa baada ya kutakiwa kuripoti Polisi alijaribu kuharibu ushahidi na pili ni katika upelelezi wetu tumebaini makosa mengine ya Kimtandao aliyokuwa akiyafanya”

Pia, ameongeza “Katika mahojiano tuliyofanya naye tulibaini alitumia namba ya simu isiyo yake katika kutenda uhalifu huo hivyo ushirikiano wake ndio utakaomfanya aendelee kukaa kituoni.

Lakini pia Wakili wake, Benedict Ishabakaki amesema baada ya mteja wake kuhojiwa walielezwa kuwa dhamana ipo wazi lakini kila wakifuatiliwa wanazungushwa.
 
Siwezi kuwa na mahaba na kiumbe mwenye kudare kumdhihaki mkuu wa nchi, tena wamweke kwa watukutu wapumlie kisogoni kabisa akitoka huko aseme kama Tundu Lissu kwamba "jail sio kuzuri".

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyoosheni kabisa huyo kiazi.

Sent using Jamii Forums mobile app



Huyo kijana hajitambui anatafuta umaarufu wa mtandaoni kwa kisingizio cha kuigiza
Kuigiza kwenywe hajui

Akawafanyie comedy wazazi wake



Huwaga hamuoni aibu hata mara moja kusupport ujinga?

Huwa mnajiona mpo safe sana kwa kuwa ni wapiga zumari wa CCM ?

I'll be back
 
Siwezi kuwa na mahaba na kiumbe mwenye kudare kumdhihaki mkuu wa nchi, tena wamweke kwa watukutu wapumlie kisogoni kabisa akitoka huko aseme kama Tundu Lissu kwamba "jail sio kuzuri".

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha ungeweza kumsujudia muumba wa mbingu na nchi kama hivi hakika ungekuwa kiumbe makini sana sio mkamilifu hapana maana ukamilifu ni wa Mungu tu ajabu ni kwamba huyo mwanadamu unaemsujudia nae anampigia goti Mungu na ana makandokando tele anaomba msamaha kwa Muumba.
 
Siwezi kuwa na mahaba na kiumbe mwenye kudare kumdhihaki mkuu wa nchi, tena wamweke kwa watukutu wapumlie kisogoni kabisa akitoka huko aseme kama Tundu Lissu kwamba "jail sio kuzuri".

Sent using Jamii Forums mobile app

Duh ni kweli unamapenzi makali kiasi hicho kwa huyo mkuu wa nchi?
Sorry wewe ni Ke au Me?

Mapenzi yako sio salama kwa mke wake you know! Please control your emotions on him utaharibu ndio ya watu
 
Back
Top Bottom