Polisi Arusha wameaibika..

escober

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
391
98
Waliwaua na kuwapiga wanachadema wa arusha waliokuwa wanaandamana kudai haki yao wakisingizia taarifa za kiintelijensia.jana polisi wakaacha chadema waandamane wenyewe ili waone kama watazua vurugu ili wapate cha kusema. Kwa mshangao wao mashujaa wetu wakaagwa kwa amani bila fujo yoyote.
kwa hili polisi wameumbuka na taarifa zao za kiintelijensia
 
Andengenye na Zuberi wanang'ang'ania nini siwaondoke tu?
Mwema afukuzwe kazi maana akijiuzulu bado kapewa heshima.
 
Waliwaua na kuwapiga wanachadema wa arusha waliokuwa wanaandamana kudai haki yao wakisingizia taarifa za kiintelijensia.jana polisi wakaacha chadema waandamane wenyewe ili waone kama watazua vurugu ili wapate cha kusema. Kwa mshangao wao mashujaa wetu wakaagwa kwa amani bila fujo yoyote.
kwa hili polisi wameumbuka na taarifa zao za kiintelijensia

Aibu kwa polisi na Mfisadi wote CCM miaka mitao hii itakuwa ya moto.
 
Ni heri wangeruhusu tu ule mkutano wa 5th ufanyike, watu wa 12th walikuwa wengi sana kwanza ukizingatia ilikuwa ni siku ya mapumziko na watu walikuwa na hasira sio mchezo kila mtu alisema liwalo na liwe walikuwa wamejitoa muhanga kabisa. Na polisi wamejifunza sidhani kama watarudia kosa tena.
 
chadema waombe polisi wasiwe wanaenda kwenye mikutano yao maana inaonekana kazi yao ni kupeleka fujo tu badala ya kulinda amani
 
Polisi awana haya awa, angalia kiwango cha elimu, hakuna anaeenda polisi kutoka form four mwenye division one wala two wala three. Labda mtoto wa kigogo anayejua god father atamnyanyua. Hiivyo tusiwalaumu. Ni uwezo wa kufikiri na kuamua.
 
si kweli polisi hawana akili mbona wapo wasomi wazuri tu na wenye shahada za uzamili nyingi hata shahada za kwanza zipo nyingi tu na wengine tumesoma nao na kufaulu vizuri sana
 
Namshauri mwema na Andengenye wawe wanavaa rangi nyeusi na kijani kazini pia wafungue tawi la CCM katika ofisi zao, itawafaa zaidi
 
Mwema usitundanganye na intelijensia yako feki...mapolisi wako form IV watajulia wapi intelijensia tena kwa ubora huu wa elimu ndo hakuna kitu,wanatumia matope badala ya ubongo. Hata wewe na mashaka na wewe uelewa wako...wa iyo intelijensia inaonesha wakati wa mafunso ulikremu hukuelewa. omba muda urudi class muzeeee usicheze tena Machaliiiii wa arusha next time askari wako wataona cha moto
 
Waliwaua na kuwapiga wanachadema wa arusha waliokuwa wanaandamana kudai haki yao wakisingizia taarifa za kiintelijensia.jana polisi wakaacha chadema waandamane wenyewe ili waone kama watazua vurugu ili wapate cha kusema. Kwa mshangao wao mashujaa wetu wakaagwa kwa amani bila fujo yoyote.
kwa hili polisi wameumbuka na taarifa zao za kiintelijensia

Na bado aibu itawashika zaidi kwani mabalozi wanasubiri kujua ripoti kamili kwa nini watumie nguvu na kuua, kwenye maandamano
 
Nimesikiliza radio Wapo asubuhi, wanasema polisi walikuwa wanashinikiza kuwa marehemu wawili walifariki kwenye ajali ya pikipiki, lakini baada ya mabishano na uchunguzi ulipofanyika ndipo ilipothibitishwa kuwa wote walifariki kutokana na kupigwa risasi, marehemu mmoja alikuwa na majeraha ya risasi na mwingine alikutwa na ganda la risasi mwilini. Kwa mujibu wa mwandishi wa Wapo radio, ilikuwa tukio lingine la aibu kwa polisi.

Sijajua hawa polisi walipata wapi ujasiri wa kutaka kuupindisha ukweli unaojulikana kwa wakazi wote wa Arusha. Na kama jambo kama hili lililo wazi kabisa polisi wanaweza kupotosha ukweli, je ni mangapi tunayoambiwa kutoka kwao tuamini.
 
Back
Top Bottom