Polisi, aibu hii mpaka lini? Mkenya wa Dk. Ulimboka afichua mapya kortini Dar

Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,669
1,791
Soma hapa utetezi wa Joshua Mulundi kabla ya kuhukumiwa:-

"Kabla ya hukumu hiyo, Mulundi aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hilo lilikuwa kosa lake la kwanza. Pia alijitetea kuwa Juni 27, 2012 akiwa Arusha alitekwa na kupelekwa Dar es Salaam ambako alikuwa hana mwenyeji wala hakuwahi kufika.

Alisema kutokana na kutekwa huko alichanginyikiwa hivyo kukubali chochote alichoambiwa afanye kwa kuwa aliyemteka alikuwa na silaha na alimwelekeza mambo ya kuzungumza.

"Mheshimiwa kwa ajili ya vitisho hivyo, nilikwenda Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kwenye eneo la Tanganyika Packers, mbele ya Mchungaji Joseph Malwa Kiliba na kuungama kuwa ni miongoni mwa watu waliomtesa Dk Ulimboka katika Msitu wa Pande," alisema Mulundi.
Huyu alitekwa kweli au anadanganya?

Source: Mwananchi online ya tarehe 1.

HATIMAYE siri ya kutekwa, kupigwa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Steven Ulimboka, imefichuka baada ya raia wa Kenya, Joshua Muhindi, kuiambia mahakama kuwa polisi walimlazimisha kusema uongo juu ya kuhusika na tukio hilo.

Alidai polisi walimpa vitisho vingi ambavyo vilimfanya aseme ili kunusuru maisha yake. Muhindi, alitoa siri hiyo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka kumsomea maelezo ya awali.

Mshtakiwa anadaiwa alifika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Kawe mbele ya Mchungaji Joseph Kiliba kuungama kwa kushirikiana na watu wengine, waliomtesa Dk. Ulimboka katika msitu wa Pande.
Kweka alidai alichukuliwa na kwenda kuhojiwa Oysterbay Polisi, alikubali kufanya kitendo hicho, akapelekwa kwa mlinzi wa amani Mahakama ya Mwanzo, akakataa ndipo alipofunguliwa shtaka la kutoa taarifa ya uongo.

Muhindi alikiri maelezo yote ni sahihi na Kweka aliomba apewe adhabu inayostahili kisheria kwa kuangalia mazingira ya kesi hiyo ilivyojengeka katika jamii na dhima iliyojificha katika jambo hilo.

Hakimu Katemana, alimtaka Muhindi kujitetea ili mahakama iweze kumpunguzia adhabu, mshtakiwa alitumia nafasi hiyo kutoa siri ya sakata zima hadi alipofikishwa mahakamani kwa mashtaka hayo.
"Nilitokea Kenya kuingia Tanzania kwa ajili ya kufanya biashara ya nguo, nikiwa Arusha Juni 27, 2012 nilitekwa, nilihamaki na niliweza kufanya chochote alichokuwa akitaka nifanye aliyeniteka.

"Aliyeniteka alikuwa na silaha, aliniambia kila atakachoniambia nikaseme kwa atakayeniambia nikamwambie, kwa vitisho vyake nilipelekwa hadi Tanga mahali nisipopajua wala sijawahi kufika."Kaniambia mimi ni Mkristo, ananituma kwa Mkristo mwenzangu, alinipa taarifa ambazo zimesomwa hapa mahakamani na Wakili wa Serikali, nilienda kanisani kutokana na vitisho, yule alikuwa mtu wao ningesema vinginevyo angewaambia ikabidi nimpe taarifa mchungaji kama nilivyoambiwa niseme.

"Nilipokubali kosa kwa kuogopa vile vitisho walinitoa pale kanisani na kunipeleka Polisi Oystebay, Polisi waliniambia ukiendelea kusema vile tulivyokwambia tutakurudisha kwenu na kukubadilishia maisha yako."Mimi ni Mkristo, ile kubadilishiwa maisha isingenifanya niseme uongo bali nilisema uongo kwa kuhofia vitisho, Polisi wakubwa walikuja kuniambia tuambie vile vile watu walivyokwambia kusema, walinirekodi nikaona haina haja ya kubishana na Serikali," alidai.

Alidai baada ya kurekodiwa alipelekwa kwa mlinzi wa amani akaeleza vile vile, lakini alishangaa kuona anafikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kujaribu kumteka Dk. Ulimboka."Siilaumu Serikali, Polisi, Mungu wala Wakili wa Serikali kwa kukaa gerezani zaidi ya mwaka, najilaumu mwenyewe kwa sababu hata ningekufa kwa kutokubaliana nao mimi si bora kuliko watu wengi katika nchi hii.

"Suala hili lilileta shida katika Serikali ya Tanzania, naiomba mahakama iniamini kwamba taarifa hizi nilizitoa kwa hiari yangu kwa sababu nilikubaliana nao kwa kuhofia kutendewa vitendo vya kuhatarisha maisha yangu.
"Nimekosa mbele ya Mungu na mahakama, naomba kwa ubinadamu na upendo nifikiriwe adhabu kwa sababu nina miaka 23, sijajipanga kimaisha na mkiwa kama wazazi mfikirie kwani hamjui kitakachokuja watokea watoto wenu, katika adhabu mzingatie hayo," alimaliza kuomba.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Katemana alisema kazingatia maelezo ya pande zote mbili, mshtakiwa alikaa gerezani zaidi ya mwaka, adhabu ya makosa yanayomkabili kisheria ni miezi sita jela au faini ya Sh 1,000.
"Mahakama imezingatia hoja za pande zote mbili, mshtakiwa amekiri kosa hivyo mahakama inamuhukumu kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh 1,000," alisema Hakimu Katemana.]

Muhindi aliyefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 2012, alikuwa hana fedha ya kulipa faini hiyo hivyo mwandishi wa Redio Times FM, Chipangule Nandule, alitoa Sh 1,000 kwa ajili ya kumnusuru kwenda jela miezi sita.

Source: Rai leo 01/10/2013


Kama hii ni kweli basi ni aibu kubwa kwa Polisi ya Tanzania. Aibu kubwa kwa mlinda sheria kuongoza uvunjaji wake kwa kuteka mtu, kulazimisha kusema uwongo na kushikilia kinyume cha taratibu.* Na kama hii ni kweli kuwa polisi ndiyo ilimteka Joshu, sijui ni nani atanifanya mimi nisisaminni kuwa ni vyombo hivyohivyo vya dola vilimteka na Dr. Ulimboka kwani kama ninavyoona ni mchezo wa kawaida! No wonder mhusika hapatikani mpaka leo.
 
Utawala unapofika Ukingoni hujitahidi kujinasua kwa njia za kipumbavu kama hizi.
Mahosipitalini huduma ni duni Rais Jakaya Mrisho Kikwete, unamteka Dr. Ulimboka unamtesa, unamteka MKENYA unamlisha maneno ili nini? Au kwa kufanya hivyo ndiyo kusema huduma bora zitakuwa zinapatikana mahospitalini???
Nani amewaloga nyie viongozi.??
Nanu amewatoa akili nyie viongozi??
Mtafanya mengi sana kabla ya kukata roho.
 
Jeshi la Polisi la Tanzania ni kikundi cha Kigaidi kinachoshirikiana na Serikali iliyopo madarakani ya CCM...! Jeshi hili livunjwe liundwe upya!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi hawa polisi wataendelea kutumika na ccm mpaka lini? Wasipoangalia itafika mahali watatumika mpaka malalio yao!
 
Sasa tunamsubiri kamanda Kova atuambie ni nani aliyemteka Dkt. Ulimboka baada ya hii movie ya mkenya kufika ukingoni!

Mwita una uhakika kuwa hapa ni ukingoni? Movie zinazotengenezwa nchini kwetu hata sterling akifa na kuzikwa huwa anafufuka toka kaburini na kuanza mashambulizi upya...
 
Soma hapa utetezi wa Joshua Mulundi kabla ya kuhukumiwa:-
"Kabla ya hukumu hiyo, Mulundi aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hilo lilikuwa kosa lake la kwanza. Pia alijitetea kuwa Juni 27, 2012 akiwa Arusha alitekwa na kupelekwa Dar es Salaam ambako alikuwa hana mwenyeji wala hakuwahi kufika.


Alisema kutokana na kutekwa huko alichanginyikiwa hivyo kukubali chochote alichoambiwa afanye kwa kuwa aliyemteka alikuwa na silaha na alimwelekeza mambo ya kuzungumza.

"Mheshimiwa kwa ajili ya vitisho hivyo, nilikwenda Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kwenye eneo la Tanganyika Packers, mbele ya Mchungaji Joseph Malwa Kiliba na kuungama kuwa ni miongoni mwa watu waliomtesa Dk Ulimboka katika Msitu wa Pande," alisema Mulundi. Huyu alitekwa kweli au anadanganya?


Source Mwananchi online ya tarehe 1.
Tukisema haya maneno aliyoyasema wakati wa hukumu ndiyo ameambiwa akaongee hivyo tutakuwa tunakosea?
 
Kova akili yake ina makengeza kama macho yake. No wonder alicheza hii movie ya kijinga.

Mwanahalisi ilishatoboa mhusika na mtekaji wa Ulimboka ni Ramadhani Ighondi alias Abeid Afisa wa Ikulu. Kwanini Polisi hawataki kumfikisha mahakamani akajitetee huko.

Ninashawishika kuamina kwamba Ramadhani Ighondi alitumwa na IKULU (read JK and his cronies)
 
Eeh Mungu wape wape adhabu wanayostahiki kova, chagonja, mwema, manumba n.k
 
Kova akili yake ina makengeza kama macho yake. No wonder alicheza hii movie ya kijinga.

Mwanahalisi ilishatoboa mhusika na mtekaji wa Ulimboka ni Ramadhani Ighondi alias Abeid Afisa wa Ikulu. Kwanini Polisi hawataki kumfikisha mahakamani akajitetee huko.

Ninashawishika kuamina kwamba Ramadhani Ighondi alitumwa na IKULU (read JK and his cronies)

Inawezekana huyu mkenya ndiyo Ramadhani Ighondu mwenyewe na bila shaka ni mtu wa kubadili badili majina, si hata wale Al-shaabab wa Nairobi na Wakenya walikuwemo.
 
Mwita una uhakika kuwa hapa ni ukingoni? Movie zinazotengenezwa nchini kwetu hata sterling akifa na kuzikwa huwa anafufuka toka kaburini na kuanza mashambulizi upya...

hata ulimboka mwenyewe hajui aliyemteka.
 
Back
Top Bottom