Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

mwogopeni anayetafuta madaraka kwa kalamu,akiingia ikulu atatoka kwa risasi....frederick sumaye
 
Ndugu zangu watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii. Kwa takribani miaka minane sasa tumeshuhudia hali ya nchi ikizidi kudhoofu kiuchumi, maisha yamezidi kuwa magumu, hali ya elimu imekuwa ikishuka kiviwango, hali ya usalama wa raia imekuwa mbaya kiasi cha kufikia watu kuuawa na polisi hadharani. Kimsingi ni kwamba uongozi wa kisera umefikia tamati ya uwezo wake kifikra na uwajibikaji. Tuna wajibu mimi na wewe wa kurekebisha hali hii, na kuna namna nyingi za kukomesha mfumo kandamizi. Tulio wengi tungechagua mtindo wa mapinduzi ya umma. Njia hii ni nzuri na ina majibu ya haraka, lakini ina maumivu ya muda mrefu pia.

Nadhani tujadili njia ya kuidhoofisha serikali iliyoko madarakari, ambayo inapata nguvu kubwa kutoka kwetu wenyewe. Magari ya maji ya kuwasha, risasi, mabomu, fimbo, na zana zote za uhalifu wa utu wa mwanadamu zinatokana na kodi zetu. Matumizi ya anasa ya serikali yanatokana na kodi zetu.

Sasa ndugu watanzania, tunaweza kuiadhibu serikali yetu na ikatusikiliza iwapo tu tutainyima mapato. Na hili linawezekana pasipo kuvunja sheria yoyote ya nchi hii, tena ni njia yenye ufanisi wa hali ya juu na isiyo na madhara yoyote ya kiafya kwa tutakaoitumia.
Tuhamasishane kususia unywaji wa pombe na vinywaji jamii ya soda, tuhamasishane kususia uvutaji wa sigara. Hii ina madhara makubwa kwa mapato ya serikali, lakini si kwa uchumi wetu kama taifa, kwani kutatokea substitution effect, isiyo na madhara kwa uchumi lakini yenye madhara kwa serikali kikodi. Badala ya serikali kununua silaha za kupambana na wananchi wake, hicho kidogo itakachokipata italazimika kulipa mishahara ya watumishi wake.

Chaguo sahihi ni kunywa maji, na kula pipi kali (kwa wavuta sigara). Hii itadhoofisha serikali, hivyo itasikiliza kilio cha watu wake.
Napenda kusikia mawazo toka kwenu.
Lakini mkuu mundali usikwepe njia ya amani ya kutatufuta suluhu!Hiyo unayoisema ingewezekana kwa serikali inayojali watu wake lakini siyo hii yetu!Maana kodi ikipungua hawa fisi wataichukua ile iliyopatikana washibishe matumbo yao na mishahara hawatalipa na ikikosekana kabisa wako tayari kuuza hata bandari moja hapa kwetu wapatie fedha ya kujineemesha au umesahau walivotaka kuuza bandari ya mtwara kwa ajili ya kulipia gharama za ndege mbovu air jordan?Kumbuka watanzania maskini ndio wanaohitaji mwalimu,daktari,muhasibu,vyuo nk.wala serikali hii haiwahitaji hawa watu hata kidogo maana hawasomi humu,hawatibiwi humu na hawahitaji kutibiwa humu maana hawana sababu ya kupata huduma humu nchini ila mimi na wewe ndo tunaohitaji haya mambo yote..Hivyo njia sahihi ni kuonyesha kuwa hatuhitaji viongozi wa aina na hawakutokana na sisi hivyo hawawezi kutuongoza tena!!Kwamba sisi ndio tunaoona umuhimu wa kuliweka jeshi lolote na tuwapokonye silaha polisi hawa wa CCM na tuwafukuze kwenye ofisi zetu na nyumba zetu!!Tufukuze raisi maana sio aina ya raisi tunayemtaka na serikali yake!!Tukifute CCM maana sio aina ya chama kinachotufaa!!Sasa haya yote yanagharama zake na miongoni mwao tena gharama rahisi sana kuuwawa na polisi wa serikali tusioitaka!!Au kuwaua polisi wa serikali tusioitaka kama hawataondoka kwa hiari yao wenyewe!!Hivyo ndivyo utavyopata ukombozi wa kweli na kuheshimiana!!ukombozi wowote ni lazima utokane na damu ya watu wanaotaka kukombolewa bila hivyo hawa mnaowaita polisi wataendelea kuua mmoja baada ya mwingine!Wakati umefika sasa kujikomboa kutokana na makucha mabeberu wauaji na wakandamizaji CCM...!!!
 
Lakini mkuu mundali usikwepe njia ya amani ya kutatufuta suluhu!Hiyo unayoisema ingewezekana kwa serikali inayojali watu wake lakini siyo hii yetu!Maana kodi ikipungua hawa fisi wataichukua ile iliyopatikana washibishe matumbo yao na mishahara hawatalipa na ikikosekana kabisa wako tayari kuuza hata bandari moja hapa kwetu wapatie fedha ya kujineemesha au umesahau walivotaka kuuza bandari ya mtwara kwa ajili ya kulipia gharama za ndege mbovu air jordan?Kumbuka watanzania maskini ndio wanaohitaji mwalimu,daktari,muhasibu,vyuo nk.wala serikali hii haiwahitaji hawa watu hata kidogo maana hawasomi humu,hawatibiwi humu na hawahitaji kutibiwa humu maana hawana sababu ya kupata huduma humu nchini ila mimi na wewe ndo tunaohitaji haya mambo yote..Hivyo njia sahihi ni kuonyesha kuwa hatuhitaji viongozi wa aina na hawakutokana na sisi hivyo hawawezi kutuongoza tena!!Kwamba sisi ndio tunaoona umuhimu wa kuliweka jeshi lolote na tuwapokonye silaha polisi hawa wa CCM na tuwafukuze kwenye ofisi zetu na nyumba zetu!!Tufukuze raisi maana sio aina ya raisi tunayemtaka na serikali yake!!Tukifute CCM maana sio aina ya chama kinachotufaa!!Sasa haya yote yanagharama zake na miongoni mwao tena gharama rahisi sana kuuwawa na polisi wa serikali tusioitaka!!Au kuwaua polisi wa serikali tusioitaka kama hawataondoka kwa hiari yao wenyewe!!Hivyo ndivyo utavyopata ukombozi wa kweli na kuheshimiana!!ukombozi wowote ni lazima utokane na damu ya watu wanaotaka kukombolewa bila hivyo hawa mnaowaita polisi wataendelea kuua mmoja baada ya mwingine!Wakati umefika sasa kujikomboa kutokana na makucha mabeberu wauaji na wakandamizaji CCM...!!!
Nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa sana Gwakisa, hasa ndilo lengu kuu, kuiondoa madarakani hii serikali dhalimu ya CCM. Lakini kumbuka tuko kwenye jamii iliyojaa watu wazito kufanya maamuzi magumu, kama ya kujitoa mhanga kukabili nguvu za majeshi ya hawa madikteta, wengi wanakuwa na kauli za kukata tamaa kama vile "YOTE TUNAMWACHIA MUNGU" n.k. Lakini tukianza kuwaunganisha katika haya mambo ambayo wanaishi nayo kila siku yenye madhara ya moja kwa moja kwa serikali, itakuwa rahisi sana kwa umoja huo kufanya mapinduzi ya kijamii. Kwa mfano tutumie kauli mbiu kama, "Soda uinywayo ndio risasi ikumalizayo", ama "Ukinywa bia moja unaangamiza watanzania kumi kwa mabom ya machozi".
Hakika ujumbe huu ukisambazwa vema, ndani ya miezi mitatu tu utaona matokeo chanya.
Pia Gwaki, adui mwombee njaa, pale serikali itakaposhindwa kuwalipa mishahara hawa wauaji, unategemea watakuwa na nguvu ya kuendelea kuua? Bila shaka mitutu yao wataigeuza kuelekea kwa watesi wetu.
 
Ni vizuri umejiuliza hayo maswali leo baada ya mzunguko kukufikia!
Ukweli ni kwamba hiyo nchi haipo na wala haijawahi kuwepo, kilichokuwepo na ambacho kipo ni propaganda tu za viongozi tangu mwanzo kujaribu kutuaminisha kwamba tunaishi ktk hiyo nchi uliyoielezea !

Jeshi la Polisi la Tanzania, kama vilivyo vitu vingi kwenye mfumo wetu, ni lile lile ambalo tumerithi kutoka kwa wakoloni, hatujabadilisha chochote kwa sababu ambazo watawala wetu wanazijua wao, kama ilivyo elimu yetu, kama zilivyo sheria tu nyingi kama sio zote, hivi unajua hata Sare tu za polisi bado zinatoka Uingereza mpaka leo?

Kwa kifupi Jeshi la Polisi au Jeshi la Wananchi (JWTZ) wamekuwa wakitesa na wakiua watu tangu ukoloni na mpaka leo sema tofauti tu ni kwamba labda sasa hivi mzunguko wa mauaji ya Polisi yamekufikia kwa hiyo unaona kama Tanzania uliyokuwa unaijua imebadilika, ukweli ni kwamba hamna jipya, kwetu kuna kambi ya Jeshi wanajeshi wakimaliza tu mafunzo breki ya kwanza Uraiani kupiga na kujeruhi na mara nyingi kuuwa raia, hiyo imekuwa ni kawaida, tangu mimi niko mdogo mpaka leo hii nimekuwa mtu mzima hakuna lililobadilka isipokuwa propaganda tuu!

umesema vyema kaka,,, hii inazidi kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi na itafika siku kila mmoja atakuwa tayari hata kufa maana uvumilivu utafikia kikomo..
 
Kuliko kupoteza muda kila siku kuunda tume za uchunguzi yanapotokea mauaji, undeni tume ya kudumu kwani inaonesha mauaji nayo ni ya kudumu.
 
Nchi yetu ilipitia kipindi kigumu sana ; wakati wa wafuasi wa chama cha wananchi (CUF) na jeshi la polisi.

Nasikitika kuona tunarudi kulekule, Vyama vya siasa kaeni na Jeshi la polisi ;kuepusha mauaji zaidi.

wanasiasa shauri wanachama kufuata maelekezo; Mara nyingi jeshi limekuwa likito taarifa mapema lakini vyama vya siasa

tumekuwa tusikia kimya kuhusu maelekezo ya serikali.

viongozi wa vyama vya siasa wanausika moja kwa moja.
 
Kufuatia vitendo vya mauaji ya kinyama yanayofanywa na jeshi la polisi katika maandamano na mikutano ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), kuna baadhi ya watu wameanza kuonyesha wasiwasi wa kutoweka kwa amani wanayodai ilikuwepo hapa nchini. Kwa maoni yangu nathubutu kusema nchi hii haikuwahi kuwa na amani ya kweli. kilichokuwepo ni utuilvu uliosababishwa na umbumbumbu wetu watanzania wa kutokujua haki zetu, hivyo watawala (serikali) pamoja na mawakala wao kama jeshi la polisi, mahakama, majeshi ya kujenga na kulinda taifa, maafisa watendaji, na wale wenye madaraka serikalini walitumia mwanya huo kututisha na hivyo tukawa waoga. Hapo ndio ikaonekana kama kuna amani, kumbe ni utulivu uliosababishwa na uoga wetu.

Nakumbuka kijijini kwetu, polisi alikuwa anaogopwa mno wakati huo, hata pale mtu alipodhulumiwa alimtegemea polisi kuamua majaliwa yake na sio sheria. leo hii watu wameamka na wengi wanaendelea kujitambua na kuzijua haki zao, wamegundua mambo mengi tu yahusuyo haki zao, kwa hiyo hawapo tayari kuonewa tena, watawala wameligundua hilo, kwa hiyo kuonyesha ubabe wao, wameamua kutuua wanavyotaka wao. ikumbukwe zamazni, tuliwaogopa pasipo sababu za msingi badala ya kuwaheshimu, ndio maana hawakuwa na sababu za kutudhuru, leo tumeelevuka na hatuwaogopi ila tunawaheshimu, wao wanaona hiyo si sawa, cha kufanya ni kutuua bila sababu za msingi ili tuendelee kuwa na hofu kama hapo awali na wao waendelee kufanya wanachotaka bila kuulizwa. LEO HII WATU WANAHOJI UHALALI WA KUZUIA MIKUTANO YA CHADEMA KWA KISINGIZIO CHA ZOEZI LA SENSA, HUKU CCM IKIENDELEA NA SHUGHULI ZAKE ZA MAANDAMANO NA MIKUTANO HUKO ZANZIBAR, WAKATI HUO HUO, TAMASHA LA FIESTA LIKIRUHUSIWA KUENDELEA NA KUKUSANYA IDADI KUBWA YA WATU BILA KUJALI WATOTO WADOGO MPAKA USIKU SAA TATU.

MAONI YANGU: TANZANIA KAMA SEHEMU YA DUNIA, IMEBADILIKA SANA, NA HAYA MABADILIKO HAYAEPUKIKI, NI ZAMU YA WATAWALA KUTAMBUA KUWA TUNAHITAJI, KUHESHIMIANA, NA SIO KUTISHANA. NA KAMWE WASIFIKIRIE TENA KAMA WATANZANIA TUTARUDI NYUMA, TUNATAKA HAKI ZETU. NA WAACHE KUTOA MAJIBU MEPESI KWENYE HOJA MAKINI. KWANI IMEDHIHIRIKA JINSI WALIVYO NA UWEZO NA BUSARA KIDOGO TOFAUTI NA MAJUKUMU WALIYONAYO. NA HII HAISHANGAZI KUKUTA AFISA WA JESHI LOLOTE LIWE LA POLISI, JKT AU HATA SERIKALINI KUWA NI FORM FOUR FAILURE, MAANA MARA NYINGI MAJIBU, BUSARA NA MAAMUZI YAO YANADHIHIRISHA WASIVYO NA UPEO MPANA WA KUPAMBANUA MAMBO.
 
tatizo letu watanzania tunaamini kuwa tatizo la mwenzako sio lako,ila tatizo lako ni la mwenzako pia hapo ndipo tunapokosea kwa mtazamo wangu.Bado tunamatarajio hata tatizo kubwa linapotokea sio jukumu letu kulitatua ila ni jukumu la mtu fulani
tunapenda kutumia neno kama
ipo siku kitanuka tu,
wanaharakati waungane,
madaktari wasikubali,
wananchi wamewachoka,

swali: ndugu zangu hali hii mpaka lini hawa watu kila siku wanatuletea matukio mapya yenye uafadhali wa jana.

maanake nishaona tukio hili nalo linaachwa kwa wanahabari kama lao peke yao kumbe ni lakila mtanzania mpenda haki,mimi , wewe na yule.
Obama alisema Yes together we can
tukitengana,tukigawanywa imekula kwetu
 
walianza na JENERALI ULIMWENGU kwa kumpa skendo ya uraia wakashindwa, wakaja kwa SAID KUBENEA kwa kutumia Tindikali wakashindwa, wakaja kwa JERY MURO kwa kumbambika kesi ya uongo wakashindwa, na hata kwa Dkt. STEPHEN ULIMBOKA mpango ulikuwa ni mauwaji wakashindwa, kwa bahati mbaya wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanikisha mauaji ya mwanahabari DAUDI MWANGOSI... Haya yote ndani yake kunaSECRET PLOT, haya mauaji si bure! WATANZANIA TUMECHOKA, JESHI LA POLISI NI JESHI LA MAJAMBAZI, SI JESHI LA USALAMA WA RAIA KAMA WANAVYODANGANYA WATANZANIA!

Endelea................
 
Dear board members, I'm suggesting POMICT TO TAKE THE NAME OF POLICE.POMICT IS PEOPLE OF MABWEPANDE INVESTIGATING CHADEMA IN TANZANIA INSTEAD OF PEOPLE OF LUNCUSHIRE INVESTIGATING CRIMINALS IN ENGLAND[POLICE].I SUBMIT
 
Hakuna polisi atayekusikiliza wewe. Kama una uchungu nenda ofisini kwa Mwema ukaongee naye. Watu wengine bwana.
 
Police msitufanye tukate tamaa kama raia wa somalia.wananchi nasi tukichukua sheria mikononi itakuwaje mtaishi sayari gani?mnavyofanya ndio usalama wa raia?kama ndiyo endeleeni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom