Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Kinachoendelea sasa kwa jeshi letu la polisi ni muendelezo tuu wa haya!.

Sisi wanahabari, tulipaswa kuyakemea matendo haya maovu ya polisi wetu tangu kitambo, na sio sasa ndio tunapiga mayowe kwa nguvu as if polisi wetu ndio wameanza leo!, najua kelele zimezidi kwa sababu ni sisi waandishi, ila polisi walipaswa kushukiwa siku nyingi, kwa sababu hizi ndio zao, kila siku wanawafanyia raia vitendo hivi, sisi kama waandishi, kazi yatu ni kutafuta angle nzuri, kupuga picha na kuripoti as if the police were doing the right thing!, mpaka walipotushukia sisi waandishi ndipo tunazinduka!.

Pasco
Shida sio POLISI ni watawala wa nchi.
Rais na PM wakikataza wasiuwe watu wataacha.
Wanafurahisha wakubwa kwa umwagaji wa damu za watu.
Nani awakemee??
 
Hakuna brutality yoyote....ni lazima tujifunze kutii mammlaka....force/nguvu iliyotumika ni reasonable....compared to resistance kutoka kwa raia....usiseme brutality ni kubwa ....sema pia kiwango cha wananchi kukaidi na kutokutii mammlaka kimeongezeka.....action and reaction
Nimeshindwa kukuelewa
 
1b49f584fc802e7a976fc89ade1c19ae.jpg
 
Wanabodi

Nimeangalia ITV news hiyo kamata kamata ya jana ya waunini wa kanisa la Ephata, vijana wako wameonyesha udhaifu mkubwa!.

Baada ya kuwalipua wale waumini kwa mabomu ya machozi na kuwa contain, walitumia risasi za moto za nini kukabiliana na watu wasio na silaha yoyote?.

Kitu cha kusikitisha zaidi ni watuhumiwa hao kuendelea kushushiwa kipigo hata baada ya kuwa mikononi mwa palisi!.

Baada ya vijana wako kuwakamata watuhumiwa kuna sababu gani ya kuendelea kuwashushia kipigo mpaka wakiwa ndani ya defender ya polisi?.

Naomba niwakumbushe tuu baadhi ya visa vya police brutality and no one amechukuliwa hatua zozote!.

Kuna kisa cha watuhumiwa fulani 4 kilichotokea Arusha ambapo watuhuniwa hao walikamatwa toka nyumbani mwao mmoja baada ya mwingine wakiwa wazima huku wakitembea wenyewe siku ya Ijumaa.

Jumamosi ndugu zao wakafika kituo cha polisi kuwaletea ndugu zao chakula, walielezwa watuhumiwa hao wamepelekwa mahali kwa mahojiano.

Kesho yake Jumapili waliporudi polisi walielezwa ndugu zao wamepelekwa hospitali ya Mt. Meru.

Walipofika hospitali waliinyeshwa miili ya watu wanne waliouwawa kinyama na majeraha ya vipigo!. Polisi walipoifikisha miili hiyo hospitalini hapo, waliandikisha kuwa wameiokota eneo la Unga Limited baada ya kupigwa na watu wenye hasira!.
The story ended up there and then!. Hakuna chochote kilicho fuatia hata tuu japo kuulizwa kama ile kesi ya Zombe!.

Kwa nini mtuhumiwa aliyekuwa mzima afie mikononi mwa polisi bila uwajibikaji wowote wa jeshi la polisi?!.

Kamanda Mwema, haya yanatokea kwa sababu mnajua Watanzania hawajui haki zao, polisi wako hawajui haki za binaadamu na kama arrest kama za jana zenye police brutality zimefanywa mbele ya camera, and nobody cares, huko behind bars ni nini haswa kinafanyika?. Si ndio itakuwa worse?!.

Yote haya yanawezekana kwa sababu Watanzania hatujui haki zetu, chochote kinachofanywa na polisi wanajua ndio haki yao tena watu hawajui kabisa kuwa raia wa kawaida anaweza kulishitaki jeshi la polisi!.

No one is above the law, please stop this police brutality inayofanywa wazi wazi and behind closed doors, kuna kitu kinaitwa karma, kitakuja kuwarudi watenda maovu wote na malipo ni hapa hapa duniani!.

Thanks.

Pasco.
Mbona hukuwahi kuandika kabla? Kaka, hebu acha ndio maana unakosa teuzi.
Mkuu Elli Mshana , karibu pande hizi na uangalie tarehe ya bandiko!.
P
 
Mkuu Elli Mshana , karibu pande hizi na uangalie tarehe ya bandiko!.
P
Mkuu, wala sina wasi wasi na maandiko yako, haya ni baadhi ya maandiko yako na wala sina hofu na hilo ila haya yanaweza kuwa tone la maji kati ya maandiko yako mengi uliyoandika. Hata hivyo ilikua ni angalizo tu na una uamuzi wa kuboresha au kubakia katika mrengo huo huo
 
Wanabodi

Nimeangalia ITV news hiyo kamata kamata ya jana ya waunini wa kanisa la Ephata, vijana wako wameonyesha udhaifu mkubwa!.

Baada ya kuwalipua wale waumini kwa mabomu ya machozi na kuwa contain, walitumia risasi za moto za nini kukabiliana na watu wasio na silaha yoyote?.

Kitu cha kusikitisha zaidi ni watuhumiwa hao kuendelea kushushiwa kipigo hata baada ya kuwa mikononi mwa palisi!.

Baada ya vijana wako kuwakamata watuhumiwa kuna sababu gani ya kuendelea kuwashushia kipigo mpaka wakiwa ndani ya defender ya polisi?.

Naomba niwakumbushe tuu baadhi ya visa vya police brutality and no one amechukuliwa hatua zozote!.

Kuna kisa cha watuhumiwa fulani 4 kilichotokea Arusha ambapo watuhuniwa hao walikamatwa toka nyumbani mwao mmoja baada ya mwingine wakiwa wazima huku wakitembea wenyewe siku ya Ijumaa.

Jumamosi ndugu zao wakafika kituo cha polisi kuwaletea ndugu zao chakula, walielezwa watuhumiwa hao wamepelekwa mahali kwa mahojiano.

Kesho yake Jumapili waliporudi polisi walielezwa ndugu zao wamepelekwa hospitali ya Mt. Meru.

Walipofika hospitali waliinyeshwa miili ya watu wanne waliouwawa kinyama na majeraha ya vipigo!. Polisi walipoifikisha miili hiyo hospitalini hapo, waliandikisha kuwa wameiokota eneo la Unga Limited baada ya kupigwa na watu wenye hasira!.
The story ended up there and then!. Hakuna chochote kilicho fuatia hata tuu japo kuulizwa kama ile kesi ya Zombe!.

Kwa nini mtuhumiwa aliyekuwa mzima afie mikononi mwa polisi bila uwajibikaji wowote wa jeshi la polisi?!.

Kamanda Mwema, haya yanatokea kwa sababu mnajua Watanzania hawajui haki zao, polisi wako hawajui haki za binaadamu na kama arrest kama za jana zenye police brutality zimefanywa mbele ya camera, and nobody cares, huko behind bars ni nini haswa kinafanyika?. Si ndio itakuwa worse?!.

Yote haya yanawezekana kwa sababu Watanzania hatujui haki zetu, chochote kinachofanywa na polisi wanajua ndio haki yao tena watu hawajui kabisa kuwa raia wa kawaida anaweza kulishitaki jeshi la polisi!.

No one is above the law, please stop this police brutality inayofanywa wazi wazi and behind closed doors, kuna kitu kinaitwa karma, kitakuja kuwarudi watenda maovu wote na malipo ni hapa hapa duniani!.

Thanks.

Pasco.

Wanabodi,

Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa haraka haraka" ambapo polisi wameruhusiwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.

Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.

Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia misingi ya haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleka majambazi wanaotumia silaha, mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubiria kupandishwa vyeo!.

Jumamosi Njema.

Paskali
Rejea.
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa .
Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa ..

Hili la polisi kuua panya road, Maelezo ya Polisi kuhusu Panya Road hayaeleweki. Kwanini wanaua na siyo kukamata? Je, ni yale yale ya akina Zombe yanajirudia?
watu wanapiga kelele utadhani haya mauaji ya polisi with impunity hawa polisi ndio wameanza leo!, hawakuanza leo, huu sio mwanzo, na wala huu sio mwisho unless something is done kuzifuta amri batil al-halal kama hii ya kwenye bandiko hili Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
P.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom