Poleni waandishi na Polisi, hongereni wanasiasa

Sep 13, 2012
4
0
NASHINDWA kuyazuia machozi yangu yanapobubujika na kudondoa kwenye kope za macho yangu hasa ninapokumbuka kifo cha Mwandishi Daud Mwangosi na watanzania wengine waliokufa na kujeruhiwa kwenye mikutano ya kisiasa hapa nchini kwetu Tanzania.

Nianze kwa kutoa pole kwa wananchi wote wakiwemo wanataaluma wote wakiwemo waandishi wa habari na askari Polisi Tanzania walioumia na wanaotarajiwa kuumizwa katika mikutano ya wanasiasa wetu kupitia ‘’Chama cha Migomo na matatizo yasiyokwisha’’ huku Polisi wakikosa mtu wa kuwasemea na kuendelea kuumizwa na kutukanwa majukwaani.

Sitaki kuorodhesha orodha ndefu ya matukiom ya kisiasa yaliyowahi kutusikitisha wengi hasa wananchi na askari polisi wanapoumizwa na hata vifo kutokea kutokana na ukaidi wa wanasiasa wenye uchu wa madaraka hapa nchini.

Nawapa ‘’Hongera’’ sana wanasiasa mnaaona ni fahari mioyoni mwenu kuona damu za watanzania zinamwagika na wengine wakipa ulemavu katika mikutano yenu ili tu ninyi mpate nafasi ya upangaji pale Ikulu. Hongereni sana lakini mjue kuwa damu hizo zitakuwa juu yenu na watoto wenu.
 
Back
Top Bottom