Makamanda wa Polisi kupambana na ujambazi kwa maelekezo ya wanasiasa inakupa tafsiri gani?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,408
Je, Polisi wanawaelimishaje Raia namna ya kutoa taarifa za kiuharifu haraka?

Jukumu la kwanza kabisa la polisi ni kulinda Raia na Mali zao. Na hiki ndicho kiapo wanachopewa.

Ujambazi, uporaji na ukabaji unapotukia hauhitaji kabisa kauli ya mwanasiasa yoyote ili polisi watekeleze wajibu wao, VINGINEVYO Kuna shida sehemu.

Inashangaza na kufikilisha sana kusubili kauli ya viongozi wa kisiasa ili kupambana na ujambazi wakati ndiyo jukumu la ajira!

Kwasababu.

Kama hadi RC/Waziri au Rais atoe tamko ndipo ifanyike ambushi maana yake asiposema majambazi hawakamatiki?

Kama kila uharifu utahitaji ODA, inamaana Waliohusika kuteka kina Ben saanane na wenginewe hawatakaa wataftwe kamwe hadi kiongozi atamke?

Kama kila uharifu hadi polisi wasubili reaction ya umma au oda ya viongozi je, wanawajua wahusika?

Inakuaje taarifa ya kiinterijensia Zibaini mikutano ya wanasiasa wa upinzani halafu zishindwe kubaini majambazi wanaopora watu wanaotoka bank yenye system/wahudumu wenye simu, camera n.k?

Polisi hawaoni kwamba inabidi kuongeza kasi ili wawe wanazuia uharifu zaidi ya kutafta waharifu?

Nchi ambayo RAIA hawaruhusiwi kumili Bunduki pasipo kibali cha polisi wanawezaje kujilinda wenyewe bila msaada wa haraka wa polisi?

Je, RAIA wanatambua namna ya kufikisha taarifa za uharifu kwa wakati haraka? Mwenye jukumu la kuwaelimisha watu ni nani?
 
Back
Top Bottom