Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
MAREHEMU REDEMPTUS ANGELO
(Picha kwa hisani ya blog ya Michuzi)
Wafanyakazi wa Kampuni ya Media Soulutions LTD (chini ya IPP Media) wachapishaji na waendeshaji wa magazeti ya ThisDay na KuliKoni wamekumbwa na msiba mzito wa ghafla wa mfanyakazi mwenzao, Redemptus Angelo ambaye amefariki Jumapili Agosti 01, 2010 Saa 4.00 usiku katika Hospitali ya Mwananyamala.
Marehemu alikuwa ni Mkuu wa kitengo cha Usanifu wa kurasa (Graphics Designer) na alikuwa anategemewa sana na Media Solutions hasa kuelekea katika hatua muhimu na nyeti ambayo kampuni hiyo inajiandaa kuifanya karibuni.
Taarifa za awali (kabla ya uchunguzi rasmi) zinadai kwamba marehemu kafa kwa sumu.
Sisi kama JamiiForums, tunapenda kutoa salaam zetu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na Uongozi mzima wa IPP Media & Media Solutions kwa msiba huu mzito.
Apumzike kwa amani