Poleni sana walimu, wanafunzi na wana jumuiya ya shule ya Sekondari Idodi

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Poleni sana wana Idodi kwa janga lililowapata. Tupo pamoja katika hilo.
Lengo la kuandika hivi ni kutaka kuona ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia wana jumuiya ya Idodi. Tumewapa misaada mingi sana ya kifedha na mali lakiki kuna kitu kikubwa sana tumesahau kutoa kwa ndugu zetu hawa.
Kitu hicho ni msaada wa kisaikolojia. Nilipokua Nairobi kuna shule moja ilipata janga kama hili na baada ya michango yote ya hali na mali walikuja watu walioitwa ma Counselors ambao ni wataalamu wa saikoloji. hawa ma counselor waliweza kuwapa msaada mkubwa sana wa kisaikolojia wana jumuiya yote ya mahali pale hasa wananfunzi na walimu. Nilifanikiwa pia kuiona ripoti yao baada ya kumaliza ile kazi. Kwa kweli walitoa mchango mkubwa sana na kuwafanya wale wanafunzi wajisikie amani na kuendelea na shule kwani wengi waliishaanza kukata tamaa na kutaka kuhama shule.

Ningependa serikali na kwa hapa kwetu kufanya kitu kama hicho ili angalau wanafunzi nao waweze kujisikia na amani na shule yao na wasome bila matatizo. tena wabna bahati sana kwani kwa pale chuo kikuu cha Tumaini wana Kitivo cha Couneling. wito wangu kwa uongozi wa mkoa kushauriana na uongozi wa chuo kikuu cha Tumaini ili waweze kuwasaidia wanafunzi hawa kisaikolojia
 
Ile shule nilienda last week kwa kweli serikali haiko serious.
Unawalaza wanafunzi 460 kwa rooms 24!
Yah mkuu councelling za apa na pale zaitajika ila kwa Tz sizani kama watafanya
 
Back
Top Bottom